Ni hivi ngoja nikuambie Africa tunafanywa nyumbu na watu weupe Kwa Sababu nimemshuhudia moina mara kadhaa analalamika serikali au wasomi wetu kushindwa kuchukua hatua za kuwalipisha wawekezaji Kwa ucheweleshaji miradi au kufanya kinyume cha mkataba.
mambo haya ni Kwa Sababu ya tunaamini kumpiga faini mwekezaji ni kumfukuza lakini wanatufanyia Mambo ya ovyo sana na unyanyasaji Kwa Sababu hatuna wataalamu.
Magufuli namtolea mfano hapa kwamba yeye kama mwanadamu alikuwa anaumia kuona watanzania tunafanywa kama wajinga japo mikataba tuliyoingia nayo hizo kampuni ni ya kinyonyaji.
Ni Sawa na umempangisha mpangaji kwenye nyumba unayoishi alafu amekulipa Kodi ya mwaka alafu anafanya matendo ambayo yanakuudhi Ila ukivunja mkataba unatakiwa umlipe fidia na ukimuacha anazidi kukuharibia familia anatembea na mkeo na watoto hivi utasubiri mkataba uishe au utafukuza kulinda hadhi yako.
Mikataba mingi ya madini Ni ya kinyonyaji na moja ya masharti ya unapomlazimisha au kumshawishi mwekezaji ni kwamba mikataba itakuwa ni Siri haiwekwi hadharani wala kujadiliwa .
Jambo ili serikalini hawataki kuliweka wazi lakini ndio ukweli kwamba wawekezaji wanatoa sharti kwamba kama unataka niwekeze Tanzania mikataba haitojadiliwa mpaka tutakaposainishana wakilenga kwamba kitendo cha kujadiliwa na WANANCHI kutaleta sintofahamu au kukataliwa .