Prof. Kitila Mkumbo: Ushauri wa Kishujaa umesababisha Tanzania ishtakiwe katika Mahakama za Kimataifa. Wasomi wetu waliwadanganya Viongozi

Mkuu, niseme hivi:
Hilo la "ni lazima aondoke", hilo siwezi kamwe kulisemea hapa, na kama ilikuwa bahati yao hao "waondoshaji" akapatikana COVID-19 aliyewawahi, lengo lao litakuwa limetimia.

Hili la "daktari au hospitali" sina uwezo wa kulijibu, hasa katika mazingira ya nchi zetu hizi, tofauti kabisa na huko kwingine ambako labda tungedai vipimo vifanyike kujua kama marehemu alikuwa na vimelea vya COVID-19 mwilini mwake alipoaga dunia.

Kisichohojiwa hapa kitaaluma ni huo uhusiano wa ugonjwa huo wa moyo kuwa kiichocheo cha kuathiriwa na COVID-19.

Ukiniuliza kuhusu Mwinyi, sijui kama naye aliguswa na COVID-19 au haikumgusa kabisa.
Na hapo hapo ni muhimu ujue kwamba siyo lazima kwa kila mgonjwa wa moyo kusababishiwa na kifo; kama ilivyokuwa wengi wa walioambukizwa na ugonjwa huo walipona, lakini kuna wengine ambao hawakupona.

Niseme hivi: Kuna ushahidi mkubwa zaidi wa kwamba watu waliokuwa na tatizo la ugonjwa wa moyo, waliathiriwa zaidi na COVID-19, hii haina maana kwamba wote walikufa. Hii ndiyo sayansi ya kitibabu, hakuna ugonjwa wowote unaoweza kuathiri watu wote kwa namna moja.
Kuna watakaoguswa kidogo tu na kuondoka; baadhi wanaguswa kwa nguvu kabisa, lakini wanapona.

Ni sawa na malaria tu, au flu, kuna wanaokuwa hoi kabisa, na kuna wenginewanaendelea na shughuli zao pamoja na kwamba wanajisikia vibaya.
 
Sasa ulidhani Magufuli angeishi muda anaotaka yeye, au kifo cha lazima kimeandikiwa baadhi ila wengine wanakufa muda wanaotaka wao?
Kila mmoja wetu ataonja mauti siku yake ikifika, hii haina maana tusijiulize kilichosababisha. Kuna viongozi walipewa sumu kina Mwakyembe mpaka makamu mwenyekiti wa CCM mzee Mang'ula umewahi kusikia upepelezi ukifanyika! Je, ni kosa kuuliza?
 
Una hakika gani kama JPM aliguswa na Covid -19? Mkuu huyu ni President of Tanzania! Wameugua kina Trump na viongozi kibao tumeona wakipelekwa hospital na wakapona. Huyu hata hospital hatujui kaugua lini na alipelekwa wapi!

Kisha viongozi walokufa Afrika ni wale walopinga kufunga nchi, sii suala la kukataa ugonjwa. Magu hakupinga Ckvid -19 hilo uongo, tuliweka tahadhali kubwa kuliko wakati wowote ule, ila JPM alipinga Chanjo! Baada ya kifo chake tukakubali chanjo na Covid iliisha ghafla kama haikuwepo..
 
Tutajua mengi sana. Hii ni moja ya pande katika vipande tutakavyovisikia.

Kuhusu mada, its a Vindication.

Ila, wapo wale ambao hawakubali tathmini ya Kitila Mkumbo. Yaani wangefurahi zaidi kama Kitila Mkumbo angesema 'Mkuu alikataa ushauri', kitu ambacho wamekuwa wakikikalia kidedea katika uwasilishaji wa hoja zao kuhusu mustakabali wa Nchi.

Hatahivyo, maoni hayo yanaondowa madoa yaliyowekwa na "Wahujumu" "Wasaliti" na maharamia wakiongozwa na Mamluki wa Makampuni yaliyoingia vita na Serikali.
 
..wewe huendi na facts.

..unatuburuza tu hapa.

..hii kesi unayoinukuu iliamuliwa ktk mahakama ya Afrika Kusini, sio ICSID.
Naenda na fact kwa sababu kuna jamaa kamzungumia huyo mzungu kuhusiana na ndege yetu kukamatwa Canada. Tatizo lenu mnachanganya mada iwe kesi hizi 7 au kwa nini ndege zetu zilikamatwa. Kesi hizi zinasomwa mahakama tofauti sii lazima nchi moja
 
"Kul nafsi zaikatul maut"
 
Magufuli alichagua mtu wa kumsikiliza
Kabudi
Mruma
Makonda zero breini
Sabaya ugoro mtupu
Hakuna Kiongozi aliyeweka safi ya Wasomi katika wizara zote nchini kama JPM- HAKUNA.. Watu kama Kijazi na Mahiga hakuna mfanO wake. Mama kisha teua wateule tunakaribia 200 kwa miaka miwili tu, lakini wapi watu wanachonga mizinga. Mama wa watu kachoka anaomba 2025 ifike haraka autue mzigo huu..
 
Udhaifu ule ule tunaousema hapa kumhusu yeye.

Ile tu kukubali kwamba gonjwa hilo lipo nchini, jamaa kang'aka!

Yule binti yake Malicela aliondolewa kwenye ukurugenzi, kwa vile tu kaeleza, tena kisomi tu kwamba kuna tatizo la ugonjwa fulani nchini. Habari hizo Magufuli alidhani zitaharibu Utalii!

Jambo baya kabisa alilofanya Magufuli, ni kukataa ushauri wa wataalam wa magonjwa ya mlipuko.
Kuna taratibu zinazofuatwa katika kushughulikia magonjwa ya aina hiyo ili kuzuia yasisambae haraka sana ndani ya jamii.

Sijui ni kitu gani kilichomfanya abadili mwelekeo baada ya mwanzo kukubali mapendekezo yote, kama ya kunawa mikono, kuojazana kwenye magari n.k.
Gonjwa lenyewe lilikuwa ni jpya, halifahamiki. Yeye katika akili yake alitazama tu kuathirika kwa uchumi, basi!

Kama ni huko kutotaka kufunga nchi, angekubali hizo hatua za kuzuia maambukizi zifuatwe kwa karibu zaidi. Badala yake yeye kaudharau ugonjwa moja kwa moja na kuuita 'mafua'. Hili ni moja ya makosa ya ajabu sana aliyoyafanya.
Ingetokea hili likawa gonjwa lenye nguvu kabisa kama lilivyoanza huko kwingine, Tanzania tungelia vibaya sana.
Tumshukuru Mwenyezi Mungu aliepusha janga.

Hili swala la kukiuka taratibu hata katika maswala ambayo hayajui, iliharibu sana sifa zake.
 
Hayo makampuni yalingoja mpaka mwamba aondoke ndio wafungue mashtaka ya kuvunja mikataba ya madini ??!! Wakati akiwa Hai aliyevunja mikataba walikuwa wanamuogopa kumshitaki ??!! Ukistaajabu ya Musa ……….. !! Michongo inakuja !!
Halafu huyu Mkumbo hivi anajitambua kweli? Aliwahi kusimulia jinsi alivyoingizwa UDSM kuwa mwalimu BILA qualifications. It is a shame. Kisa alipokuwa rais wa serikali ya wanafunzi pale UD aliwasaliti wenzie kwenye mgomo.

BILA AIBU yeye anadai eti kiongozi fulani pale UD alimgundua kuwa ni talented. Shame shame shame
 
Ni kweli.
Lakini ndiyo haya tunayojadili hapa ya wasomi kutofuata usomi unavyowaelekeza, badala yake wanafanya anayotaka aliyewateua.

Ni hili niseme halikuanza na Magufuli, kwa wasomi kuweka akili zao pembeni wanapopewa nafasi ya uongozi.
Ukihesabu idadi ya maprofesa waliowahi kushika nyadhifa tokea uhuru utaona kwamba hakuna yeyote aliyetumia usomi wake kuleta mabadiliko yoyote katika nafasi aliyoitumikia.
 
Mkuu yule alikuwa mtu wangu sana RIP, lakini alikosea maana protokali hutakiwi daktari kutangaza kitu wakati hujaitaarifu mamlaka. Ebu jiulize, Ugojwa ule uliishia wapi mbona baada ya kukataliwa na kuvuliwa nao ulipotea!

Mkuu Magu hakupendwa toka anaingia madarakani. Kama unakumbuka 2015, UKAWA wote walitoka nje ya Ukumbi wa Bunge akabakia Zitto, naye akalauniwa sana. Kosa kubwa alofanya JPM ni kuwageuka wenzake!

Alipoanza kutaka kuonyesha yeye Mzelendo kuliko wao hapo akaunda maadui wa ndani na lilipokuja swala na Wawekezaji ndio kajichimbia kaburi kabisa.
Anyway, nimerudi JF kutaka.kuirudisha JF ile ya 2006 - 2010. Kwikwikwi.. Nyani Ngabu yuko wapi?
 
Kila Waziri ni mwajiliwa wa rais na Kila Mbunge ni mwajiriwa wa Chama! Hili neno Mtumishi wa Umma ni kwa makalani..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…