Mkuu, niseme hivi:Taarifa hii imetoka kwa daktari gani au hospital gani? Hilo Tatizo la Moyo wangapi wana tatizo hilo Tanzania? hata Mzee Mwinyi analo miaka na Covid imepita, yule pale mzimaaa!
Ukweli ni kwamba jamaa alikuwa lazima aondolewe kwa sababu alikuwa na maadui wengi nje na ndani kutokana na Maslahi tu. Awamu hii wanajua na ndio maana kutwa ni kumkana JPM kama kwamba wamelazimishwa kusema wewe upo upande gani? Wote hawa ni Mtandao hawana msimamo ni WAOGA kupitiliza.
Hilo la "ni lazima aondoke", hilo siwezi kamwe kulisemea hapa, na kama ilikuwa bahati yao hao "waondoshaji" akapatikana COVID-19 aliyewawahi, lengo lao litakuwa limetimia.
Hili la "daktari au hospitali" sina uwezo wa kulijibu, hasa katika mazingira ya nchi zetu hizi, tofauti kabisa na huko kwingine ambako labda tungedai vipimo vifanyike kujua kama marehemu alikuwa na vimelea vya COVID-19 mwilini mwake alipoaga dunia.
Kisichohojiwa hapa kitaaluma ni huo uhusiano wa ugonjwa huo wa moyo kuwa kiichocheo cha kuathiriwa na COVID-19.
Ukiniuliza kuhusu Mwinyi, sijui kama naye aliguswa na COVID-19 au haikumgusa kabisa.
Na hapo hapo ni muhimu ujue kwamba siyo lazima kwa kila mgonjwa wa moyo kusababishiwa na kifo; kama ilivyokuwa wengi wa walioambukizwa na ugonjwa huo walipona, lakini kuna wengine ambao hawakupona.
Niseme hivi: Kuna ushahidi mkubwa zaidi wa kwamba watu waliokuwa na tatizo la ugonjwa wa moyo, waliathiriwa zaidi na COVID-19, hii haina maana kwamba wote walikufa. Hii ndiyo sayansi ya kitibabu, hakuna ugonjwa wowote unaoweza kuathiri watu wote kwa namna moja.
Kuna watakaoguswa kidogo tu na kuondoka; baadhi wanaguswa kwa nguvu kabisa, lakini wanapona.
Ni sawa na malaria tu, au flu, kuna wanaokuwa hoi kabisa, na kuna wenginewanaendelea na shughuli zao pamoja na kwamba wanajisikia vibaya.