Cc
Kalamu pita hapa, hoja hii hii nilisema juu ya Mpina.
Katika watu ninaowaheshimu humu jukwaani, ni pamoja na huyu mkuu 'macho', sina shaka naye kuhusu misimamo yake hata kidogo.
Na niseme wazi, hata nikitofautiana na haya aliyoyasema hapa; ambayo ni sawa na uliyoyasema wewe, haina maana kwamba kuna sehemu tunaweza kubaliana katika jambo hili hili, tukielezana vizuri.
Sasa ngoja nikukumbushe pia, kwa vile nawe umenikumbusha.
Nilishasema humu JF, kwamba hali ya nchi yetu ilivyo sasa, hasa kwa hawa tunaowaita wanasiasa wetu, ni wachache sana kati yao walio na uwezo wa kusimama na kulitetea jambo lolote wakijua kwamba kutetea huko kutawanyiama chakula chao kinachopatikana kupitia kwa ufadhiri wa chama au kiongozi mkuu wa chama.
Naomba mtu yeyote anayeweza kunipa mfano, kwa mfano wa kundi lile la akina Njeru Kasaka kwa sasa hivi, ni nani ndani ya CCM, au hata ndani ya CHADEMA?. Ni nani? Ningemhesabu Lissu katika kundi hilo, lakini hali yake ninaielewa, siwezi kumlaumu.
Na baada ya kuyasema hayo kumhusu huyu Bwana anayeongelewa hapa nikasema kuwa nipo tayari kumsikiliza yeyote anayepaza sauti kwa sasa hivi, bila kujali alifanya nini huko nyuma wakati wa Magufuli, iwe ni kwa woga wakati huo, au iwe ni kwa kutafuta fursa ya uteuzi wakati huu, nipo tayari kumsikiliza mtu huyo kama sauti yake inatetea maslahi ya waTanzania.
Kwa hiyo, kwa sasa hivi, bila kujali anachokitafuta Luhaga Mpina, nitamsikiliza, kwa sababu sisikii sauti nyingine yoyote, na zaidi zaidi kwa masikitiko makubwa hata toka kule kwa CHADEMA, ambayo tulidhani ndio mbadala ttuliobaki nao. Lakini CHADEMA imetekwa, sasa tutafanyaje.
Natumaini nimejieleza vya kutosha.
Kama nimechanganya humo ndani, naomba msamaha, kwa sababu nilitiririka tu, sikurudi nyuma kuhariri chochote.
Cc
Kalamu pita hapa, hoja hii hii nilisema juu ya Mpina.