Prof Kitila: Serikali Imepokea Ushauri wa Kujenga Daraja kati ya Dar-Zanzibar

Hiyo fedha iingizwe kwenye Maji safi na salama kwa wote kwanza hapo ni bora aletwe mwekezaji wa Ferry kubwa zenye kubeba hadi Malori.
Hilo nalo neno
Ila hawa watu huwa wanaona maji na vyoo kama havina maana
Lakini umepiga pale pale boss
Kweli kabisa ila maji ya Lake Victoria yameishia wapi
Ila mdogo mdogo tutafika
Wenzetu ukiona treni zinazobeba magari na containers utashangaa urefu wake
Tutafanikisha kama viongozi wataamua na wananchi kutoa maoni na kelele kila wakati
Hawa bilakukumbushwa hawashtuki
 
Daraja na Zanzibar ni kupoteza fedha, tuwekeze miundombinu kwenda Congo DRC huku kuna biashara kubwa. Yaani tujenge daraja la kwenda kuuza viazi na shanga Zanzibar? Hii biashara kichaa tuachane nayo.
 
Wewe nyumbu,China imejenga sana miradi kama hii.

Huu mradi utakuwa wa PPP na wawekezaji wamekuwa wakitoa hili pendekwzo siku nyingi sana.

Maelfu ya Watalii watashika Dar au Zanzibar then wata cross Kwa Barabara via hii so itakuwa poa sana
Huu ujinga huu uishie huko tusiusikie huko, kuna watalii wanashindwa kuja bara kutoka Zanzibar kisa hakuna daraja?
 
Inatakiwa Maji safi na Salama kwa wote hilo Daraja sidhani kama litatumiwa na watu wengi kama maji safi na salama.
 
Sioni umuhim wa daraja hili ndugu Mkumbo ,kama tupo na muungano wa namna hii, wakati ndugu Kitila anawaza daraja binafsi nawaza Muungano ufe kesho kama sivyo twende na serikali 3, au moja watanganyika tumechoka sasa
 
Halina tija kabisa hilo daraja, ni mawazo ya chawa kujipendekeza tu kwa mama!
Yaani nchi ipate hasara kujitumbukiza kwsnye miradi ya kipuuzi kwa faida ya chura kiziwi.
 
Inatakiwa Maji safi na Salama kwa wote hilo Daraja sidhani kama litatumiwa na watu wengi kama maji safi na salama.
Mkuu unafikiri ni NGOs ngapi na misaada mingapi inatumwa kila mwaka kwa ajili ya maji, madawa na hela taslimu?
Kama wangekuwa na wema leo tatizo la maji lingekuwa limeisha zamani sana
Upigaji hata za misaada
Yaani laana itatuandama sana
 
Mkuu unafikiri ni NGOs ngapi na misaada mingapi inatumwa kila mwaka kwa ajili ya maji, madawa na hela taslimu?
Kama wangekuwa na wema leo tatizo la maji lingekuwa limeisha zamani sana
Upigaji hata za misaada
Yaani laana itatuandama sana
Hilo Daraja la Tanganyika to Zanziba linaweza kufikia Billioni 10 US Dollars hebu fikiria hizo fedha zikiingizwa kwenye vipaumbele muhimu?
 
NUKUU: Mtu mwenye akili,akikuambia Jambo la kijinga na wewe ukamkubali, atakudharau.".Mwl.Julius Kambarage Nyerere



Sasa waziri wa uwekezaji na tume ya mipango Tanzania mheshimiwa Profesa Kitila Mkumbo ( (Mb), kukubali kutenga fedha na muda wa wataalamu wa wizara yako ili kufanya ubembuzi yakinifu (feasilibility studies) tayari dunia nzima ya watu wenye ufahamu watakuwa tayari wanatia shaka uwezo wa hata kumshauri bosi wako kuhusu mipango na uwekezaji unaofaa kwa nchi yetu Tanzania
 
Kuna shida gani?
Daraja la kwenda Zanzibar lina umbali gani, litafanya biashara gani, litagharimu kiasi gani, return on investment itarudishwa muda gani, litatatua tatizo gani, meli zitapitaje, katika nchi hii yenye matatizo mengi, kwa nini hili liwe kipaumbele?
 
mpeni bi Kizimkazi muone gharama za daraja zitabadirishana na mlima kilimanjaro.
 
Daraja la kwenda Zanzibar lina umbali gani, litafanya biashara gani, litagharimu kiasi gani, return on investment itarudishwa muda gani, litatatua tatizo gani, meli zitapitaje, katika nchi hii yenye matatizo mengi, kwa nini hili liwe kipaumbele?
Huyo ChoiceVariable achana naye! Uchawa tu, hana lolote kichwani
 
Hivi Kwa hali ya Uchumi wetu tutaweza kweli hizo gharama za Ujenzi?

Labda kama tutajenga Kwa njia ya PPP then tukawa tunatumia Kwa kulipia kama ilivyo daraja la Mwalimu Nyerere - Kigamboni

Ni wazo zuri kulitekeleza kama Kuna hiyo nafasi
Yes tutaweza, it called mkopo
 
Daraja la kazi gani ilihali watanzania bara wanabaguliwa huko?
 
Kujenga daraja hilo kutapoteza ladha ya ya Dr- Zanzibar maana kusafiri kwa boti ni moja ya utalii wa baharini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…