Prof. Kitila: Watanzania Masikini wamepungua kwa 25%

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, amesema takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha umaskini wa mahitaji ya msingi Nchini Tanzania Bara kimeendelea kupungua kwa miaka ya hivi karibuni kutoka asilimia 34.4 (mwaka 2007) hadi asilimia 25.1 (mwaka 2025).

Akiwasilisha Bungeni taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2025 pamoja na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2026/2027 Prof. Mkumbo amesema kiwango hicho kimeshuka kutoka asilimia 34.4 mwaka 2007, asilimia 28.2 mwaka 2012, asilimia 26.4 mwaka 2018 na kufikia asilimia 25.1 mwaka 2025.

Hata hivyo, amesema bado kuna haja ya kuongeza juhudi katika kupunguza umaskini ili kasi yake iendane na ukuaji wa uchumi wa Taifa kama ilivyoainishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Prof. Mkumbo amesema Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (OCGS) pamoja na wadau wengine, imekamilisha Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi (HBS) wa mwaka 2025.

“Huu ni utafiti wa saba kwa Tanzania Bara na utafiti wa nne kwa Tanzania Zanzibar, na ni utafiti wa kwanza ukihusisha pande zote za Muungano kwa wakati mmoja, matokeo ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania 2025 yanaonesha kuwa Watanzania wanaishi katika umaskini wa mahitaji ya msingi ambapo kwa Tanzania Bara ni asilimia 25.1”

Ngoja nikae kimya tajiri mie wa 25% nisome tu comments za walio bado masikini.
 
Huwa wanaongea na kaya gani hawa mazafakas?
 
Wamepungua Kwenye Makaratasi Yake
Ukweli Na Hali Inavyoonekana Hali Ni Tete Sana Kama Mji Faruja Kule Iraq Wakati Wa Vita
 
Back
Top Bottom