Prof. Lipumba: Bajeti iliyosomwa ni mbovu haijawahi kutokea tangu tupate uhuru. Takwimu nyingi haziko sahihi

Kwa hiyo hicho kilichoandikwa hapo ndio uchambuzi wa Professor Mbobezi na nguli wa uchumi!? Au mmepunguza alichosema? Maana sioni Hizo takwimu (facts and figures) alizotoa hapo!
 
Waziri wa fedha amechemka. Maana hata takwimu alizotoa hazilandani na kilichomo kwenye bajeti.

Na hii bajeti haikufakyiwa utafiti
Profesa Lipumba: Bajeti ya Serikali mbovu kuwahi kutokea.
===
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ameikosoa bajeti ya Serikali akisema ni mbovu kuwahi kutokea tangu apate uzoefu wa kuzichambua bajeti zinazowasilishwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Kutokana na kasoro alizodai kuwemo katika bajeti hiyo, Profesa Lipumba ambaye ni mtaalamu wa uchumi, ameishauri Serikali kujenga utamaduni wa kufanya utafiti wa kina wa sera za kodi ili kutengeneza mipango ya kukuza maendeleo na kuongeza ajira kwa vijana na kutokomeza umaskini.

Ameyasema hayo leo Juni 19 jijini hapa wakati akiichambua bajeti ya Serikali iliyosomwa bungeni Juni 14, akifafanua kuwa bajeti hiyo imeshindwa kuakisi malengo ya Rais Samia Suluhu Hassan likiwemo la kuanzisha Tume huru ya uchaguzi.

"Hotuba hiyo ilikuwa mbovu mbovu kuwahi kutokea kwa Waziri wa Wizara ya fedha tangu kupata uzoefu wangu wa kupitia na kuzichambua bajeti zote," amesema.

Ametoa mfano wa taarifa za Wizara ya Mifugo akisema hazioani na kitabu cha hali ya uchumi.

“Ukirejea kwenye kitabu cha uchumi wa taifa hazipo, napata wasiwasi. Naomba kabla ya kwenda kusoma bajeti ni vizuri zipitiwe na wataalamu kuhakikiwa tarakimu kabla ya kwenda kusomwa zifanane na zile zilizopo kwenye kitabu cha hali ya ukuaji uchumi wa taifa," amesema.

Kuhusu mfumuko wa bei amesema Watanzania wanalalamika kuongezeka kwa gharama za maisha. Kila kitu hasa vyakula na nishati vimepanda bei, lakini taarifa ya Serikali inaeleza kuwa bei zimeongezeka kwa asilimia 4 tu jambo ambalo alilodai kuwa si kweli.

"Vitu ulivyonunua kwa Sh100,000 Mei 2021, watu kwa sasa wanatumia Sh104,000 tu Mei 2022. inashangaza kuona takwimu za Serikali gharama za maisha nchini zimeongezeka kwa kasi ya chini kuliko gharama za maisha Marekani na nchi za Ulaya," amesema.

Kuhusu elimu bila malipo, Profesa Lipumba amesema katika bajeti hiyo Serikali imetangaza kufuta ada za kidato cha tano na sitana kujigamba kuwa sasa Tanzania ina elimu bure toka darasa la kwanza hadi kidato cha sita. lakini ukweli ni kwamba ada ni sehemu ndogo chini ya asilimia 10 kwa kidato cha tano na sita za gharama ambazo mzazi ana wajibika kulipa ili mwanae aenendelee na masomo.

Kuhusu sera za kodi, alisema Waziri huyo amefanya makosa kuunganisha vitambulisho vya taifa na ulipaji wa kodi hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali haijakamilisha zoezi la kuwapatia vitambulisho vya taifa watanzania wote baada ya zaidi ya miaka kumi toka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) kuanzishwa.

"Ni muhimu Serikali ikajikita kuharakisha Wananchi kupata vitambulisho vyao, lakini wakiendelea kuongelea suala hilo wanaweza kusababisha watu wasijisajili wakijua kufanya hivyo watatozwa kodi," amesema.

CREDIT: Mwananchi
Ni ukweli mtupu.
Mwigulu ni msomi wa uchumi ila ana uwezo wa kwenye vitabu tu syo ktk nyanja za kuweza kuvitendea kazi
 
Lipumba kalinganisha may na June hayo yako ya Ukraine vita ya Ukraine iliyoanza February baki nayo mwenyewe
Wapi kwenye uzi kumeandikwa May na June.!? Hapo imeandikwa May 2021 na May 2022. Kwani hata hizo takwimu zimechukuliwa kabla ya bajeti kusomwa. Kwa hiyo Lipumba kaeleza facts kulingana na time frame hiyo. Wewe unakuja kuleta vioja vya time frame ya May na June ya mwaka huu...Ujinga huu kawaeleze wajinga wenzako mnaolipwa posho kutoka ikulu..
 
Mwigulu anaandaa bajeti ili kumfurahisha bosi wake bila kuihusianisha na mipango, matokeo yake ndio haya ametengeneza bomu asilojua alitegue vipi.

Matokeo yake kila akitolea ufafanuzi wa jambo anazidi kuongeza maswali badala ya kutamaliza.
Wampe mbunge wa vunjo hiyo chance, dr Chaaz Kimei
 
Lakini hata mimi naunga mkono kuwa hii bajeti nadhani ni ya ovyo kwa maana serikali yetu kutenga trilioni moja na kichele kwa ajili ya maendeleo AF trilioni 13 kwa matumizi ya kawaida hilo jambo linatia wasiwasi sana
 
Mwingilu Nchemba kila kitu kwake ni Siasa tu.

Mwaka Jana alikuja na Tozo zisizo kuwa na kichwa Wala miguu hadi sipik n Wabunge na Rais na Mawaziri wakashangaa wakati bajeti ishapita.

Hata sasa tutegemee maumivu.
 
Nilijua nyie sisiemu wenzety mna mfumo mwingine wa kifedha? kumbe ndio huu huu wa watanzania wote?
 
Kuhusu sera za kodi, alisema Waziri huyo amefanya makosa kuunganisha vitambulisho vya taifa na ulipaji wa kodi hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali haijakamilisha zoezi la kuwapatia vitambulisho vya taifa watanzania wote baada ya zaidi ya miaka kumi toka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) kuanzishwa.

"Ni muhimu Serikali ikajikita kuharakisha Wananchi kupata vitambulisho vyao, lakini wakiendelea kuongelea suala hilo wanaweza kusababisha watu wasijisajili wakijua kufanya hivyo watatozwa kodi," amesema.
Hapo Mwigulu Nchemba kabugi.
Kuunganisha vitambulisho vya taifa na kodi ni upuuzi🤔
 
Waziri wa fedha amechemka. Maana hata takwimu alizotoa hazilandani na kilichomo kwenye bajeti.

Na hii bajeti haikufanyiwa utafiti
Profesa Lipumba: Bajeti ya Serikali mbovu kuwahi kutokea.
===
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ameikosoa bajeti ya Serikali akisema ni mbovu kuwahi kutokea tangu apate uzoefu wa kuzichambua bajeti zinazowasilishwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Kutokana na kasoro alizodai kuwemo katika bajeti hiyo, Profesa Lipumba ambaye ni mtaalamu wa uchumi, ameishauri Serikali kujenga utamaduni wa kufanya utafiti wa kina wa sera za kodi ili kutengeneza mipango ya kukuza maendeleo na kuongeza ajira kwa vijana na kutokomeza umaskini.

Ameyasema hayo leo Juni 19 jijini hapa wakati akiichambua bajeti ya Serikali iliyosomwa bungeni Juni 14, akifafanua kuwa bajeti hiyo imeshindwa kuakisi malengo ya Rais Samia Suluhu Hassan likiwemo la kuanzisha Tume huru ya uchaguzi.

"Hotuba hiyo ilikuwa mbovu mbovu kuwahi kutokea kwa Waziri wa Wizara ya fedha tangu kupata uzoefu wangu wa kupitia na kuzichambua bajeti zote," amesema.

Ametoa mfano wa taarifa za Wizara ya Mifugo akisema hazioani na kitabu cha hali ya uchumi.

“Ukirejea kwenye kitabu cha uchumi wa taifa hazipo, napata wasiwasi. Naomba kabla ya kwenda kusoma bajeti ni vizuri zipitiwe na wataalamu kuhakikiwa tarakimu kabla ya kwenda kusomwa zifanane na zile zilizopo kwenye kitabu cha hali ya ukuaji uchumi wa taifa," amesema.

Kuhusu mfumuko wa bei amesema Watanzania wanalalamika kuongezeka kwa gharama za maisha. Kila kitu hasa vyakula na nishati vimepanda bei, lakini taarifa ya Serikali inaeleza kuwa bei zimeongezeka kwa asilimia 4 tu jambo ambalo alilodai kuwa si kweli.

"Vitu ulivyonunua kwa Sh100,000 Mei 2021, watu kwa sasa wanatumia Sh104,000 tu Mei 2022. inashangaza kuona takwimu za Serikali gharama za maisha nchini zimeongezeka kwa kasi ya chini kuliko gharama za maisha Marekani na nchi za Ulaya," amesema.

Kuhusu elimu bila malipo, Profesa Lipumba amesema katika bajeti hiyo Serikali imetangaza kufuta ada za kidato cha tano na sitana kujigamba kuwa sasa Tanzania ina elimu bure toka darasa la kwanza hadi kidato cha sita. lakini ukweli ni kwamba ada ni sehemu ndogo chini ya asilimia 10 kwa kidato cha tano na sita za gharama ambazo mzazi ana wajibika kulipa ili mwanae aenendelee na masomo.

Kuhusu sera za kodi, alisema Waziri huyo amefanya makosa kuunganisha vitambulisho vya taifa na ulipaji wa kodi hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali haijakamilisha zoezi la kuwapatia vitambulisho vya taifa watanzania wote baada ya zaidi ya miaka kumi toka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) kuanzishwa.

"Ni muhimu Serikali ikajikita kuharakisha Wananchi kupata vitambulisho vyao, lakini wakiendelea kuongelea suala hilo wanaweza kusababisha watu wasijisajili wakijua kufanya hivyo watatozwa kodi," amesema.

CREDIT: Mwananchi
Umenena vyema Professor Lipumba, waziri aliyepo kiti kimempwaya, anawaza kuchora Jina lake tena juu ya mawe Nchi nzima.

Dr Charles KIMEI atatufaa Kwa nafasi hiyo. Amen
 
Aisee...

Ajabu
 
Back
Top Bottom