Prof. Lipumba: Rais Samia Kadanganywa na Kikosi kazi cha Demokrasia, hatukukubaliana vile

Prof. Lipumba: Rais Samia Kadanganywa na Kikosi kazi cha Demokrasia, hatukukubaliana vile

Huyu nae si akae kimya tu maana unafiki wake tumeshauchoka mda mrefu sana
Binadamu hukengeuka, baadaye hujirekebisha na kutubu..

Hata wewe bila shaka kuna wakati ulikuwa mnafiki lakini ulipoona unafiki hauilipi, ulitubu na kubadilika..

We can't judge you referring your past after repentance..!

Sasa kwanini wewe unamhukumu Lipumba? Sikiliza na soma hoja zake, tujadili hizo. Acha kushambulia personality yake..
 
Mzee wa kupepesa ulimi kama Nyoka mbele ya yai viza...

Huyu nae ni mtu wa hovyo sana mbele ya pesa... amejaa tamaa isiyomithilika hapo mate yanamtoka kwa miposho wanayolamba akina Zitto si kingine.

Hopeless!!
Nadhani Zitto aje akanushe ya Prof au akubaliane naye. Kukaa kimya haitasaidia

JokaKuu Fundi Mchundo
Kama alichosema Lipumba kina ukweli, Zitto atakuwa amejipaka matope.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa Prof. Ibrahim Haruna Lipumba ameoneshwa kusikitishwa na baadhi ya masuala yaliyowasilishwa na Kikosi Kazi cha kuratibu Maoni ya Wadau...
Tumsubiri Zitto ze double dealer
 
Kama alichosema Lipumba kina ukweli, Zitto atakuwa amejipaka matope.
Lipumba ni mmoja wa watu waliopoteza credibility hata hivyo ametusaidia sana kujua walichokubaliana. Kwa mantiki hiyo Zitto akikaa kimya atathibitisha shaka iliyokuwepo kuhusu 'kununuliwa''. Kuna namna Tatu za yeye kufanya.

1. Kujitokeza na kukanusha maneno ya Prof

2. Kujitokeza na kuafiki maneno ya Prof

3. Kukaa kimya na kuacha jamii ithibitishe dhana

JokaKuu
 
Lipumba ni mmoja wa watu waliopoteza credibility hata hivyo ametusaidia sana kujua walichokubaliana. Kwa mantiki hiyo Zitto akikaa kimya atathibitisha shaka iliyokuwepo kuhusu 'kununuliwa''. Kuna namna Tatu za yeye kufanya....
Inawezekana hilo la kusogeza katiba mpya baada ya uchaguzi wa 2025 ni maoni binafsi ya hicho kikosi na sio wadau kama kina Lipumba.

Hivi wanaohitaji katiba mpya wanataka kipi kifanyike maana bunge la katiba lilishaijadili rasimu ya warioba, je wanataka kura ya maoni ya kuidhinisha ile katiba?, Au mchakato uanze upya (kujadili upya rasimu ya warioba) ?

Ila kwa aina ya wabunge waliopo hapo Dodoma (ukizingatia walivyopatikana mwaka 2020) ni bora huo mchakato usogezwe mbele tu.
 
Mzee wa kupepesa ulimi kama Nyoka mbele ya yai viza...

Huyu nae ni mtu wa hovyo sana mbele ya pesa... amejaa tamaa isiyomithilika hapo mate yanamtoka kwa miposho wanayolamba akina Zitto si kingine.

Hopeless!!
Haaa
 
Maswali yanazuka, ikiwa anachosema Lipumba ni kweli, Zitto alikwendaje Ikulu na kamati?

Mkutano wa TCD ulikuwa na agenda tofauti na iliyopelekwa kwa mujibu wa Prof hapa ndipo Zitto anaingia

Lakini si Zitto kama Raia ni Zitto kiongozi wa ACT Wazalendo, chama cha Marehemu Maalim Seif kilichopigania katiba mpya ! ACT Wazalendo wajiulize hli na Umma una haki ya kujua nini kilitokea
 
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa Prof. Ibrahim Haruna Lipumba ameoneshwa kusikitishwa na baadhi ya masuala yaliyowasilishwa na Kikosi Kazi cha kuratibu Maoni ya Wadau ...
Arudishe posho za watu basi!
Ah!
 
Inawezekana hilo la kusogeza katiba mpya baada ya uchaguzi wa 2025 ni maoni binafsi ya hicho kikosi na sio wadau kama kina Lipumba.

Hivi wanaohitaji katiba mpya wanataka kipi kifanyike maana bunge la katiba lilishaijadili rasimu ya warioba, je wanataka kura ya maoni ya kuidhinisha ile katiba?, Au mchakato uanze upya (kujadili upya rasimu ya warioba) ?

Ila kwa aina ya wabunge waliopo hapo Dodoma (ukizingatia walivyopatikana mwaka 2020) ni bora huo mchakato usogezwe mbele tu.
Kama ni maoni binafsi inaonekana Lipumba wa CUF haafiki kama chama.
Hapa ndipo Zitto anahitajika kutoa ufafanuzi

Kuhusu katiba, hoja hapa ni kurejea kwa Rasimu ya Warioba.
Katiba pendekezwa iliondoa 3/4 ya maoni ya wananchi hivyo haina uhalali.

Kinachotakiwa ni kurejea rasimu, kupitia upya tatizo lililojitokeza wakati ule na kuunda sheria itakayounda Bunge maalum la katiba.

Bunge maalum la katiba halihusishi Wabunge wa sasa, bali utaratibu utakaowekwa wa kuwapata wabunge. Kuna challenge kwamba lazima sheria ibadilishwe na Bunge la sasa, kwa mantiki hiyo kunahitajika ''political will''. Je ni ngumu, hapana! kukiwa na nguvu ya umma inawezekana.
 
Inawezekana hilo la kusogeza katiba mpya baada ya uchaguzi wa 2025 ni maoni binafsi ya hicho kikosi na sio wadau kama kina Lipumba.

Hivi wanaohitaji katiba mpya wanataka kipi kifanyike maana bunge la katiba lilishaijadili rasimu ya warioba, je wanataka kura ya maoni ya kuidhinisha ile katiba?, Au mchakato uanze upya (kujadili upya rasimu ya warioba) ?

Ila kwa aina ya wabunge waliopo hapo Dodoma (ukizingatia walivyopatikana mwaka 2020) ni bora huo mchakato usogezwe mbele tu.
Kusogezwa mbele siamini kama ni nasuluhu,ila kikubwa ni kuwa na dhamira ya kweli kwenye kupatikana kwake,kwani wanakijani hola zao ni za kiwango Cha kuitwa animal na SII watu🤔.

Kumbuka mnyama hata anapojidai rafiki bado hafai kuaminika.Angalia chui au thimba😂 anapocheza na katoto kamnyama iwe swala,nyumbu au ngiri vile anavyojidai anacheza na mwisho wa siku nini kinafuata kama SII kuliwa kikatili Tena Kwa matendo🤭🤭🤭🤭🤭🤭🤭🤭
 
Binadamu hukengeuka, baadaye hujirekebisha na kutubu..

Hata wewe bila shaka kuna wakati ulikuwa mnafiki lakini ulipoona unafiki hauilipi, ulitubu na kubadilika..

We can't judge you referring your past after repentance..!

Sasa kwanini wewe unamhukumu Lipumba? Sikiliza na soma hoja zake, tujadili hizo. Acha kushambulia personality yake..

Uko sahihi kabisa, ila haaminiki. Tumsamehe lakini tumempuuza hata kama this time atakuwa anasema kweli. Kwa maneno marahisi atalipia gharama ya usaliti wake.
 
Mbowe alisemaje kutoshiriki hicho kikao? Studio lete ukweli
 
Yeye na kikosi kazi hawana tofauti yoyote.
 
Back
Top Bottom