#COVID19 Prof. Makubi: Wanasayansi Wazalendo wanakaribia kutengeneza Chanjo ya Corona ya Kitanzania

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Katibu mkuu wa wizara ya afya Prof. Makubi amesema kama taifa tunakaribia kupata chanjo yetu ya Corona.

Prof Makubi amesema wanasayansi wazalendo hawajalala katika utafiti na wako mbioni kutupatia chanjo ya Corona ambayo itakuwa ni ya kwetu wenyewe.

Source: ITV habari

=============
Katibu mkuu wa wizara ya afya, Prof. Abel Makubi wakati wa mkutano na viongozi wa dini jijini Dar es Salaam ameongelea Tanzania ilipofikia katika kutengeneza chanjo yake yenyewe kujikinga na Covid-19

Prof. Makubi: Sasa hivi kuna suala la chanjo, chanjo hii sisi hapa mheshimiwa Rais ameshaagiza kwamba tuanze kutengeneza chanjo na huo mchakato umeshaanza, kwahiyo sasa hivi tuko katika hatua za kutumia wazalendo kutengeneza chanjo.

Kuna watu ambao wanaweza wakatengeneza chanjo, watanzania, kwahiyo tuko katika mchakato huo, lazima tujivunie kwamba tuna watanzania ambao wameshafika hatua nzuri.



Nae waziri wa Afya Godwin Molell amesema hakuna haja ya watu kuogopa kuhusu chanjo ya sasa ya Corona

Godwin Molell: Kama tulikubali ARV na leo tunakubali na ilituonyesha ilivyofanya kazi, leo kwanini tunasuasua kwenye Corona. Serikali yetu haikuwahi kukataa, serikali yetu hata hii ya ARV imejiridhisha, leo tunaipokea baada ya michakato mbalimbali hata Corona imekuwa hivyo hivyo, ni kwasababu tu ya mapokeo tofauti

Tujiwekeze kwenye elimu ya kujitambua na kubadili tabia, wakati tunafanya hizi zingine lakini nguvu kubwa iende kwenye kujitambua wasiende huko
 
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 

Hizi ndizo habari tunataka kusikia, sio ujinga ujinga tu kama vingwendu.
 
Nani ataithibitisha?
 
πŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ‘πŸ½
Tunapendekeza ajaribishie chanjo kwa mtoto wake kwanza
 
Kwa hiyo chanjo, na mimi nitachanja! Bila hivyo sichanji.
 
Watamchoma Gwajima?
 
Ile juisi ya wizara kwa hisani ya Dr. Gwajima & husband imefeli kwani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…