#COVID19 Prof. Makubi: Wanasayansi Wazalendo wanakaribia kutengeneza Chanjo ya Corona ya Kitanzania

#COVID19 Prof. Makubi: Wanasayansi Wazalendo wanakaribia kutengeneza Chanjo ya Corona ya Kitanzania

Katibu mkuu wa wizara ya afya Prof Makubi amesema kama taifa tunakaribia kupata chanjo yetu ya Corona...

Mwendelezo ule ule wa kufanya siasa kwenye gonjwa linalouwa.

Hatuwezi kutengeneza hata sindano ya kushonea nguo tunataka kutengeneza rover kwenda Jupiter?!

Habari hii ni kwa madhumuni ya kuwatoa watu kwenye reli kuwa mtaani hali ni mbaya na vifo vinazidi kuongezeka.

Hata ipite miaka 20, hadithi zitaendelea kuwa zile zile kuwa sasa chanjo yetu ina karibia sana. Kwamba vifaranga wa kuku si wangali wanasubiria nyonyo wapate nao kunyonyeshwa maziwa?

Timu hii ya mwendazake wizara ya afya bila ya maboresho ya msingi, ni suala la muda tu kurudi tena Mkapa stadium.
 
Ujinga ujinga tu, hadi sasa watu wanajifanya kulalamika kwamba mbona chanjo imetumia muda mdogo kutengenezwa, tena hapo tunahoji wataalam wabobevu walioendelea na wenye vifaa vya kisasa kabisa.

Sasa hii tunaipigia debe kwa sababu ni ya kwetu au tumejiridhisha imetumia muda wa kutosha kufanyiwa utafiti kama tunavyodai?

Huu upupu ndio unazidi kumpaisha mchungaji na wafuasi wake, tumejaza siasa kwenye mambo ya kitaalam.
 
Yani Hiyo chanjo yao ndo tutakimbia mpaka visigino viguse visogo
 
Ujinga ujinga tu, hadi sasa watu wanajifanya kulalamika kwamba mbona chanjo imetumia muda mdogo kutengenezwa, tena hapo tunahoji wataalam wabobevu walioendelea na wenye vifaa vya kisasa kabisa...
Watakachofanya ni kutafuta package mpya ila dawa ni ile ile ya JJ. Chezea watanzania kwa magumashi
 
Watakachofanya ni kutafuta package mpya ila dawa ni ile ile ya JJ. Chezea watanzania kwa magumashi

Watawaambia nini raia ambao wanahoji muda uliotumika kuifanyia utafiti na majaribio?
Inabidi wabadili sababu ya kuzikataa hizi zilizopo kwamba sio za kwetu na hatuziamini, tunaziamini tulizotengeneza wenyewe.

Hapo ndio utaibuka utata mwingine kuhusu zoezi la kuendelea kuchanja hizi tunazopokea kutoka nje.
 
Hivi si ni hawa hawa wataalamu wetu waliopima mbuzi, kuku na mapapai na kukuta yana virusi vya corona? Kama ni hao hao hizo chanjo waanze kuzijaribisha kwanza kwenye mapapai, kuku na mbuzi. Mapapai, kuku na mbuzi yakipona wahamie kwa products za mikesha ya mwenge na tupo tayari kuwapa orodha ya wahusika.
 
Naomba kujua mchango wa wanasayansi nchini katika kutengeneza Chanjo ya Corona (COVID Vaccine). Asante
 
Ule mzigo wa Madagascar naskia waligawana wenyewe na haukufua dafu. Wakaondoka tele. Kufanya masihara na pendemic ni hatari. Corona sio Chadema ebo😂😂😂😂
 
Makubi na chanjo ya kitanzania. Nakumbuka wakina Gwajiboy na kauli ooh chanjo imechukua muda mfupi mno kwa hiyo ya kibongo itachukua muda gani bwana. Ili kuhakikisha efficacy yako bro, mnaanza lini kuijaribu kwa nyani au wapi. Msituletee miti shamba hapa mkatuulia watu wetu.
 
Katibu mkuu wa wizara ya afya Prof. Makubi amesema kama taifa tunakaribia kupata chanjo yetu ya Corona.

Prof Makubi amesema wanasayansi wazalendo hawajalala katika utafiti na wako mbioni kutupatia chanjo ya Corona ambayo itakuwa ni ya kwetu wenyewe.

Source: ITV habari

=============
Katibu mkuu wa wizara ya afya, Prof. Abel Makubi wakati wa mkutano na viongozi wa dini jijini Dar es Salaam ameongelea Tanzania ilipofikia katika kutengeneza chanjo yake yenyewe kujikinga na Covid-19

Prof. Makubi: Sasa hivi kuna suala la chanjo, chanjo hii sisi hapa mheshimiwa Rais ameshaagiza kwamba tuanze kutengeneza chanjo na huo mchakato umeshaanza, kwahiyo sasa hivi tuko katika hatua za kutumia wazalendo kutengeneza chanjo.

Kuna watu ambao wanaweza wakatengeneza chanjo, watanzania, kwahiyo tuko katika mchakato huo, lazima tujivunie kwamba tuna watanzania ambao wameshafika hatua nzuri.


Nae waziri wa Afya Godwin Molell amesema hakuna haja ya watu kuogopa kuhusu chanjo ya sasa ya Corona

Godwin Molell: Kama tulikubali ARV na leo tunakubali na ilituonyesha ilivyofanya kazi, leo kwanini tunasuasua kwenye Corona. Serikali yetu haikuwahi kukataa, serikali yetu hata hii ya ARV imejiridhisha, leo tunaipokea baada ya michakato mbalimbali hata Corona imekuwa hivyo hivyo, ni kwasababu tu ya mapokeo tofauti

Tujiwekeze kwenye elimu ya kujitambua na kubadili tabia, wakati tunafanya hizi zingine lakini nguvu kubwa iende kwenye kujitambua wasiende huko

4B6CCD63-5921-4B63-9307-BE2249A087E4.jpeg
 
Back
Top Bottom