TANZIA Prof. Mathew Luhanga, aliyekuwa Makamu Mkuu wa UDSM kuanzia 1991 hadi 2006 afariki dunia

TANZIA Prof. Mathew Luhanga, aliyekuwa Makamu Mkuu wa UDSM kuanzia 1991 hadi 2006 afariki dunia

RIP Professor Matthew Luhanga. Ulikuwa na ndoto nyingi za kuandika vitabu vingi.

Kutoka maktaba:
29 Juni 2021
PROF MATTHEW LUHANGA - MAKAMU MKUU MSTAAFU WA UDSM NA MAPINDUZI YA ELIMU NCHINI


Profesa Matthew Luhanga ni Makamu Mkuu mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) aliyehudumu kwa mafanikio makubwa chuoni hapo. Mbali ya wadhifa huo pia ni mtaalamu mbobezi wa uhandisi. Jaafar Mponda amezungumza nae kwenye ZUMARI ili kufahamu mengi ikiwemo mchango wake katika kuwasaidia vijana kielimu kupitia falsafa mbalimbali ambazo yeye (Profesa Luhanga) anaziamini.
Source : Azam TV
N.B
Wazee wabadilishe kawaida yao, waandike vitabu mapema wakiwa in their 40s
 
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye anasikitika kutangaza kifo cha PROF. MATTHEW LUHANGA, aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia 1991 hadi 2006, kilichotokea jioni ya leo tarehe 16.09. 2021. Tunatoa pole kwa familia, Chuo chetu na Tanzania kwa ujumla. Taarifa zaidi tutaendelea kujulishana. Tumwombee apumzike kwa Amani. Amina.

Dkt. Dotto P. Kuhenga, Mratibu wa Mawasiliano na Habari, UDSM.

View attachment 1941008

=======

Professor Matthew Luhanga ndie Mwanasayansi wa Zama hizi mwenye historia iliyotukuka duniani
Alafu hii familia nahisi wote ni ma genius kuna mwenzake alikuwa Tanesco. RIP Prof
 
Back
Top Bottom