Prof. Mbarawa: Abiria waliotumia usafiri wa anga waliongezeka na kufikia Milioni 6.81

Prof. Mbarawa: Abiria waliotumia usafiri wa anga waliongezeka na kufikia Milioni 6.81

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amebaisnisha mafanikio ya sekta ya usafiri wa anga kwa kipindi cha kuanzia Julai 2025 hadi Machi 2026, ikionyesha ukuaji mkubwa wa idadi ya abiria na usafirishaji wa mizigo nchini.

Akizungumza bungeni leo Mei 13, 2026, Prof. Mbarawa amebainisha kuwa katika kipindi hicho, sekta hiyo imeshuhudia ongezeko la abiria kufikia milioni 6.81, ikiwa ni ukuaji wa 12.63% ikilinganishwa na abiria milioni 6.037 waliosafiri katika kipindi kama hicho cha mwaka wa fedha 2024/2025. Ongezeko hili linatajwa kuchangiwa na kuimarika kwa huduma na miundombinu ya anga nchini.

Aidha, Prof. Mbarawa ameeleza kuwa usafirishaji wa mizigo umepata mafanikio, ambapo jumla ya tani 34,750.2 zimesafirishwa ndani na nje ya nchi. Katika kuhakikisha usalama wa anga, jumla ya ndege 189 zilifanyiwa ukaguzi wa kina na kupewa vyeti vya ubora, hatua inayothibitisha utayari wa Tanzania katika kutoa huduma za usafiri wa anga zinazozingatia viwango vya kimataifa.


 
Kuongezeka kwa hiyo idadi kunasaidia nini iwapo kila mwaka shirika linatengeneza hasara ya billion of shillings!
 
Siku hizi hadi abiria wanahesabiwa na kuwa sehemu ya kujivumia maendeleo.
 
Siku hizi hadi abiria wanahesabiwa na kuwa sehemu ya kujivumia maendeleo.
Mimi sio shabiki wa serikali ila maendeleo au progess kwenye sector yoyote huwa inapimwa kwa takwimu. Hata planning inahitaji takwimu, sio suala la kubeza.
 
Back
Top Bottom