Prof. Mbarawa: Treni hii ya Tanzania siyo high speed train kama zile za vichwa vilivyochongoka, Wananchi eleweni hilo

Prof. Mbarawa: Treni hii ya Tanzania siyo high speed train kama zile za vichwa vilivyochongoka, Wananchi eleweni hilo

Ni SGR mkuu, aliyewaambia ni high speed (Bullet train) aliwadanganya mchana kweupe, hii ya kwetu inaweza hata isifike 180km/hr..... nadhani itakuwa between 100 and 150km/hr max
Jamaa zetu hata hawajui, high speed train ina reli yake mahususi,,, ukiweka kwenye reli hii ya SGR haiwezi
 
Sijategemea kupata maelezo yasiyoeleweka kama haya, nataka kitu mayai basi, iende vipi hainihusu!
 
Hatimae Treni ya Masafa marefu yaanza kuwasili
FB_IMG_16694675854507282.jpg
FB_IMG_16694675817786724.jpg
FB_IMG_16694675777072909.jpg
FB_IMG_16694675886319505.jpg
 
Ni kweli..lakini mbona kwenye picha zao za mwanzo hao TRC walituonesha kitu tofauti na tulicholetewa?
Kadogosa chief architect & prominent member wa Sukuma Gang akili yake iliharibiwa sana na Magufuli
 
Ni kweli..lakini mbona kwenye picha zao za mwanzo hao TRC walituonesha kitu tofauti na tulicholetewa?
Mliwekewa picha za EMU, mshaambiwa EMU mkataba wao na hyundai rotem vitaletwa kuanzia mwakani mpka 2024, mbona mnakuwa sio waelewa watanzania?

Emu zinakuja kwa set (jozi) yaan kichwa ila kichwa chake huwa na madirisha ya abilia, kichwa chake huwa mbele na nyuma, kuweni wapole
 
johnthebaptist hii nchi ni shida. Viongozi hutuona watanzania hatuna akili. Kulikuwa na sababu gani kutudanganya hapo mwanzo na picha za vichwa mchongoko?? Ila tukumbuke kilikuwa kipindi cha bwana yule, ambaye kudanganya ilikuwa ni sifa nzuri.
Angekuwepo ndio tungemuhukumu ,ila waliopo Sasa kuwaamini ni ngumu sana
 
Hapanaa hapanaaa, Mambo yamebadilishwa hapa mwishoni..huoni reli iko vizuri tuu?
Umejuaje kuwa "reli iko vizuri tu" mkuu 'Kakijana'? Umefanya majaribio yoyote juu ya reli hiyo kabla ya kufikia hitimisho hili?
 
Mliwekewa picha za EMU, mshaambiwa EMU mkataba wao na hyundai rotem vitaletwa kuanzia mwakani mpka 2024, mbona mnakuwa sio waelewa watanzania?

Emu zinakuja kwa set (jozi) yaan kichwa ila kichwa chake huwa na madirisha ya abilia, kichwa chake huwa mbele na nyuma, kuweni wapole
Hii habari ipo wapi mkuu 'Mr DIY', nami nikajiridhishe kwa kuisoma. Hebu nielekeze tafadhali.
 
Kama tuliamua kujenga reli ya SGR yenye kasi ya Km 160/180 kwa saa, basi tungefikiria na design ya mabehewa yanayovutia kwa nje na ndani, yanayompa starehe abiria kulingana na thamani ya pesa aliyotoa, yanayoruhusu kukaa bila kubanana.
Hapa chini ni treni inayopita kwenye reli inayofanana na hii ya kwetu, inafanya safari zake kati ya Malmo-Sweden hadi Copenhagen-Denmark. Tujiulize kwa nini sisi tulipofanya manunuzi hatukufikiria kununua mabehawa kama haya yanayoonekana kwenye video hii fupi?.https://youtu.be/FaRIcadXWyc
 
Hii sasa kitaalamu tunaita Chenga ya mwili
Hahaha..

“Kwa kutumia Reli hii mtu atasafiri kutoka Dar es Salaam hadi hapa Dodoma kwa saa 3 tu ikilinganishwa na saa 5 hadi 6 zinazotumika hivi sasa kusafiri kwa gari na pia mtu atasafiri kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa saa 9 ikilinganishwa na saa 36 anazotumia hivi sasa kusafiri kwa Treni”.... amesema Rais Magufuli na kuongeza kuwa Reli hiyo itakuwa na uwezo wa kusafirisha Tani milioni 17 za Mizigo kwa Mwaka ikilinganishwa na ya sasa yenye uwezo wa kusafirisha Tani milioni 5 tu.
 
Maneno ya waziri ukiyasikiliza unaona kama Trab na Trat zinaendelea, ukiangalia hizo behewa za masafa marefu halafu ukarudi ukatazama safari ya Dar Kigoma, Mwanza na Mpanda, Utagundua:
  1. Watu wa zamani walikuwa na akili na uwezo mkubwa wa kujua mambo na kutatua shida halisi za watu,
  2. Pili utaona hawa wa sasa akili zao ni copy and paste zaidi, safari ya kukaa kwa muda mrefu behewa za zamani ni bora kuliko hizi sababu watu waliweza ku stretch miguu, kujinyoosha na hata kukaa kwa nafasi na ndio raha ya train, sasa wameweka mabasi juu ya reli, wajomba zangu waha mizigo yao wataweka wapi???
  3. Serikali ipo kulinda viongozi na kauli zao hata kama wanakosea bado wanaamini fikra za mwenyekiti ndio sahihi na wapambe na machawa ndio washauri wa viongozi wetu, na
  4. Bei tunazotajiwa za vitu kama hawaongezi sifuri basi viongozi wasio na fikra wanatupigisha short.
Hii train kama wenye mabasi hawatabanwa na watapewa uhuru wa kushindana basi tutalipa deni lisilo na faida.
 
Back
Top Bottom