Prof. Mbarawa: Tukipata muwekezaji mahiri bandarini, 67% ya bajeti itatoka bandari ya Dar na kuacha kutembeza bakuli

Siungi mkono ubinafsishaji wa bandari usio na manufaa hata hivyo ufanisi Serikalini katika biashara hauwezi kutatuliwa na Jeshi.

Dunia inahama kwa kasi sana kutoka kwenye sera za uchumi wa kuzilinda biashara za nchi kwa mabavu kwenda kwenye teknolojia za kisasa na mbinu sahihi.
 
Muulizeni kwa ule mkataba wa hovyo aliosaini yeye, akawapa waarabu bandari zetu zote Tanganyika milele, tena mkataba usioonesha mwarabu amewekeza kiasi gani kwenye uwekezaji wake, hiyo 67% anayoizungumzia ya bajeti yetu itatoka wapi?

Mbarawa ni mwongo mpuuzi.
 
Hilo ni liprofesa la ovyo ni maongo ni mpumbavu tu ataamini ujinga anaoongea.
 
Ni madude ya hovyo yasiyo aminika.
 
Mbarawa unatuona kama wajinga wapumbavu au…..?
Hatutaki mkataba wenu mbovu
Acheni Tanganyika iamue yenyewe sio ninyi. 67% mmebebezane nao muende kisiwani hapa Tanganyika msituzoee
 
YES....Kama kuna ulazima wa kuleta mwekezaji....NA....Iwe kwa mkataba usiokuwa na makandokando !!!
 
Hata gas mlituambia hivyohivyo. Poleni watanganyika, mtambue Sasa Nguvu ya Raisi ipoje. Mwendazake akatuambia watu wanataka maji, umeme , chakula, Wala hakuna atakayekula Katiba.
 
Hizo ahadi za Kipumbavu kuwa asilimia 67% ya bajeti bandari ndio itaendeshwa tunaomba iwe ya kimaandishi na iwe sheria na isipokuwa hivyo awajibishwe na kufilisiwa na kunyongwa huyu Mbawala na regime yake... Kuwafanya Watanganyika wapumbavu ni uhaini... WANASHERIA WETU WAZALENDO TUNAOMBA MSAADA WA KUANDIKA MKATABA KATI YETU NA MBAWALA - Tuanzishe hizi sheria iwe mwisho wa kufanyana wapumbavu...
 
TATIZO SIO MAKUSANYO TATIZO NI VIONGOZI MAFISADI NA MATUMIZI YA HOVYO YA SERIKALI
 
tunachekesha sana, kama tunajua bandari inaweza kutupa 67% ya budget kwanini miaka yote hiyo tusiweke macho yetu pale huku tuna vyombo lukuki vya usalama kila mahala mpaka tuone ubinafsishaji pekee ndio solution?

yaani miaka yoote tunakopa na kutembeza bakuri huku tukiiletea mzaha bandari na tulikuwa tunawaambiaga na mpaka Rais mmoja wa nchi jirani akatuambia tukamuona adui, leo hii mnatuambia tubibafsishe tuongeze ufanisi, inamaana huo ufanisi unapatikana kwa kubinafsisha tu?

Hivi RAIS leo akisema nataka 67% ya budget itoke pale mbele ya TISS director, CDF, IGP, bosi wa bandari na wafanyakazi wote wa TPA, Itashindikana?
 
Miaka zaidi ya 60 hatukufanya na bado mnaamini tutaweza
 
PITA HAPA UONE!
Angalieni huu ukurasa wa sahihi kwa karibu sana!
Mnaona hapo kwa upande wa shahidi kuna sahihi ya Mbarawa ilianza alafu haikuisha - akaweka mtu mwingine! Aisee Alafu mashahidi wote wawili hawana majina na huyo wa Dubai hata cheo hatujui ni nani!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WAZIRI wa Uchukuzi Bw MBAWALA anadai BANDARI ikipata MWEKEZAJI Makini Bandari itachangia Asilimia 67 Ya BAJETI na "HATUTATEMBEZA BAKULI."

BINAFSI NAMPINGA kwa sababu MFUMO uliopo Hayo MAKUSANYO yatapigwa na WAHUNI na HAWATAFANYWA chochote kwani SHERIA zilizopo ZINAWALINDA WEZI na MAFISADI hivyo TUSIDANGANYANE.

Viongozi na Watendaji Wamekuwa WAKIIBA FEDHA za SERIKALI kama REPORT ya CAG inavyoonyesha lakini HAKUNA HATUA wala UTHUBUTU wa KUWACHUKULIA HATUA Umeonyeshwa na VYOMBO VYOTE sio BUNGE TAKUKURU wala SERIKALI hivyo na Hayo MAKUSANYO ya BANDARI YATAIBIWA TU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…