Prof. Mkenda: Shule nne zilizofanya Udanganyifu Mtihani kidato cha nne 2022 zichunguzwe na hatua zichukuliwe

Prof. Mkenda: Shule nne zilizofanya Udanganyifu Mtihani kidato cha nne 2022 zichunguzwe na hatua zichukuliwe

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Na WyEST
MWANZA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Profesa Adolf Mkenda amemuagiza Kamishna wa Elimu kufanya uchunguzi wa kina kwa Shule nne zilizobainika kufanya udanganyifu mkubwa katika mtihani wa kidato cha nne mwaka 2022.

Prof. Mkenda amesema hayo alipokutana na Wazazi na walezi wa Wanafunzi waliofutiwa matokeo ya Mtihani wa Kidato nne 2022 wa Shule ya Sekondari Thaqaafa ya Jijini Mwanza kwa ajili ya kuwasikiliza.

Amezitaja shule hizo kuwa ni Cornelius ya Kinondoni Dar es Salaam, Thaqaafa ya Mwanza, Mnemonic ya Zanzibar na Twibhoki iliyoko Mara na kumtaka Kamishna huyo kuchukua hatua kali kulingana na ripoti ya uchunguzi huo.

Mkenda amesisitiza wazazi kuwalea watoto katika maadili ili watambue kuwa udanganyifu si mzuri na una madhara makubwa katika upande wa haki, maadili na uweledi.

"Tunapowapeleka watoto shule tunataka wajifunze waelewe ili baadae waje watumikie taifa. Sasa mtu anakuja kuwa daktari au mhandisi au rubani kwa kuiba mtihani, madhara yake ni makubwa sana," ameongeza Mkenda.

Mkenda amewapa pole wazazi na kuwataarifu kuwa mitihani hiyo imefutwa na hivyo kilichopo ni kurudia mitihani.

"Kuhusu kurudia mtihani tumewasikiliza maombi yenu, ninashukuru kuwa hamna anayesema ameonewa sote tunakubaliana kuwa kulikuwa na udanganyifu na hivyo niseme matokeo yamefutwa na kikubwa ni maombi ya kurudia mtihani. Hili tunalichukua tutawasiliana nanyi baada ya kulifanyia kazi kwani ni suala la kibajeti pia," amefafanua Mkenda.

Naye Adam Malima, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akiwa katika kikao hicho amesema Serikali haitalea shule zinazofanya udanganyifu wa mitihani na kuongeza kuwa wanafunzi wanatakiwa wapimwe kwa uwezo na sio kwa kudanganya.

Katika maelezo yao yaliyotolewa kupitia Mwenyekiti wa wazazi hao, Patrick Msagati wameomba Serikali kuwahurumia na kuruhusu matokeo kuachiliwa au kuwapa nafasi ya kurudia mtihani.

"Tunaomba Serikali ichukue hatua kali kwa shule kama hizi kwani zimetusababishia madhara makubwa sisi kama wazazi na watoto pia. Ikiwezekana shule hizi zifungiwe," amesema Michael Zayumba, mmoja wa wazazi.

IMG-20230219-WA0020.jpg
IMG-20230219-WA0015.jpg
IMG-20230219-WA0024.jpg
 
Vijana wa allah wanaiba mtihani? Tuwakate mikono kama wanavyolilia mahkama ya qadhi
 
Jana tulimtuma mwl kuiba kura. Na wewe unajua hata kura zako siyo halali. Lakini wewe ni mmbunge halali wa serekali wa serekali isiyokuwa na kura halali. Tumepeleka watoto shuleni kusoma siyo kuiba mitihani. Wezi wa mitihani ni wale wenye uzoefu wa kuiba kura. Sasa wamehamia kwenye mitihani. Fungeni wezi wa kura kwanza wezi wa mitihani watatoweka.Tendeni haki jamani dunia hii ni mapito tu.
 
Jana tulimtuma mwl kuiba kura. Na wewe unajua hata kura zako siyo halali. Lakini wewe ni mmbunge halali wa serekali wa serekali isiyokuwa na kura halali.Tumepeleka watoto shuleni kusoma siyo kuiba mitihani. Wezi wa mitihani ni wale wenye uzoefu wa kuiba kura. Sasa wamehamia kwenye mitihani. Fungeni wezi wa kura kwanza wezi wa mitihani watatoweka.Tendeni haki jamani dunia hii ni mapito tuuuu
SAPOTI!
 
Wewe angalia safari ya mwanasiasa yoyote iliyoanzia Kwenye Wizi wa mitihani au Jina la mwanafumzi mwingine ni lazima atakuwa mwizi wa kura

Mifano ni Mingi hasa Kwenye vyama vikuu vya Upinzani Chadema na ACT Wazalendo

Naunga mkono 100% kauli ya Prof Mkenda kwamba Wizi wa mitihani ni hasara kubwa sana kwa Taifa

Usiibe, amri ya Mungu wa mbinguni!
 
Back
Top Bottom