Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 20,561
- 24,428
Mara kadhaa Serikali imesisitiza kuwa suala la malipo ya michango ya ziada ni suala la makubaliano kati ya Shule na Wazazi au Walezi wa Watoto, hilo linaangukia pia kwenye suala la chakula kwa Wanafunzi, ambapo utaratibu ulivyo umekuwa kero kwa wengi wetu.
Utaratibu ulivyo kwa sasa kila shule imekuwa na bei zake, mfano ni Tsh. 1,000 hadi 1,500 kila asubuhi.
- Mwanafunzi anapokuwa hana fedha ambalo siyo kosa lake bali ni ufinyu wa kipato kwa Wazazi/Walezi basi adhabu ya fimbo itamwangukia Mwanafunzi huyo na pengine kukatazwa asihudhurie masomo kisa ameshindwa kutoa fedha ya chakula.
- Kiwango cha chakula wapewacho ni kidogo kiasi kwamba kuna baadhi huwa wanapewa si zaidi ya vijiko vitatu vikubwa vya chakula.
- Upo uwezekano mkubwa kwa hasira ambazo Walimu huwa nazo huu huwa mradi wao, + wapewa tender!
- Serikali ipange kiasi sahihi ambacho Mwanafunzi atatakiwa kukilipa kisichozidi Tsh. 500/- aidha kila Mtoto awe anachangia 10,000 kwa mwezi, ili kupata stock ya Jumla kuliko hivi kwa mafungu ambayo kuna muda mambo yakiwa magumu, unamvuruga mtoto.
- Haya nimeyaona katika shule fulani, yakanisikitisha sana!,
-Vipato vya wazazi wengi havipo sawa kuna, wajane wanasomesha, mama ntilie, wabibi walioyelekezewa wajukuu na wengi tu ndani ya jamii yetu,
-Serikali ije na mwarobaini wa tatizo hili la sivyo Walimu watakuja leta maafa wa watoto wasio na hatia yoyote!
Adios amigo!