KERO Prof. Mkenda suala la chakula Shuleni, limekuwa mateso na mzigo kwa Wazazi / Walezi, bora kipangwe kiasi fulani cha fedha kwa wote

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kwani wakati haya màmbo yamepigwa marufuku watoto walikuwa hawasomi?
Waalimu wamepata mradi wa kuwingizia pesa, serikali iangalie maàna sasa ni kama rushwa kwa traffic.
Wanaadhibiwa watoto wasio na hatia.
 
We huna akili yaani uzae we mtoto serikali ndio imlishe?

Ada uwekewe Bure, na chakula ushindwe?

Utaomba serikali ikupe Hadi mafuta ukatafunwe vizuri
 
Serikali ya ccm imejaa viongozi wapumbavu walio tukuka ...vyakula mashuleni avijaleta tija yoyote ni kama upumbavu wa vazi la hijabu mashuleni hakuna tija yoyote ndiyo kwanza umalaya umeongezeka .....serikali pumbavu ya ccm ifute mambo ya chakula mashuleni isipokuwa shule za bweni tu ....tumetoka kwenye upumbavu wa serikali na upumbavu wa walimu wa kuwabebesha kila siku wanafunzi fangio na na kidumu ...kila siku nenda nacho rudi nacho bila ya sababu za msingi ...kwani walimu walishindwa nini kusema kila mwanafunzi aje na kidumu na fagio nq kuandikishwa kuwa amesha kujanavyo kisha wiwe mali ya shule viifadhiwe mashuleni badala ya mwanafunzi kila siku kubeba fangio chafu na dumu chafu kutoka nymbani na kurudi nalo nyumbani...na kusababisha madhara ya kisaikolojia au mwanafunzi kupigwa viboko kisa kasahau fangio au kusababisha mambo ya wizi na kujenga tabia za wizi maana wanafunzi wataanza kuibiana mafagio kutokana na kukaguliwa kila siku kama wamekuja na mafagio ...nakumbuka wakati ninasoma shule ya msingi kuna wanafunzi kazi zao zilikuwa ni kuiba mafagio tu kwa wenzao na kujanayo kesho wao awapigi fimbo anaye pigwa fimbo ni yule aliye ibiwa fagio ...huu pumbavu sasa tuna wabebesha wanafunzi mabakuri ya vyakula kwenye mabegi .
 
Huwa siwaelewi watu wanaowapinga na kuwacheka rungwe na mbunge kishimba, anyway ubwabwa kwanza!!!
 
Kama hamna uwezo mnazaa watoto wanini? Yaani mpewe Ada bure bado kulipia chakula mnalia lia??
 
Walimu wa shule za serikali ni watu wa ajabu sana, mfano mtoto darasa la tatu madaftari kumi na mbili sijui yanini, michango isiyoisha kila uchao, yaan wamewageuza wazazi ni migodi yao,

Bora serikali iweke ada shule za serikali tujue moja wazazi.
 
yani hutaki kutoa 30,000 kwa mwezi ili mwanao apate chakula ? kwahio ashinde njaa shuleni ?
 
Mimi siyo mwalimu, ila tutumie logic ya kawaida tu, kama Serikali haitoi msaada wa chakula cha watoto, unadhani kama siyo mzazi/mlezi nani atamchangia mtoto chakula?
Hatupingi chakula hapana, ispokuwa kuwe na mpango sahihi... Jumiushi utakaosaidia wazazi wote bila kujali hali zao za kiuchumi.
 
Binafsi sijawahi sikia watoto wakichapwa au kufukuzwa shuleni kisa mchango wa chakula, ila nimeona watoto wakishinda njaa kutwa nzima bila msaada kisa hawajachangia chakula.
Yanatokea hayo fanya utafiti kabla kukimbilia ku comment.Hata kwenye michango mwingine Walimu wanasumbua sana Wanafunzi Viongozi huishia kupiga kelele tu huko nje lakini Walimu wala hawajali wanasumbua sana Wanafunzi,labda inaweza kuwa sio shule zote ila nyingi zina huo ukatili.Niliwahi kuandika kisa hiki humuhumu,siku moja asubuhi nilikutana na Mtoto (wa kayumba)asubuhi, wa darasa kati ya la kwanza au la tatu ,analia sana nikamuuliza kwa nini analia akasema, amemwambia Mama ampe mia tano amekataa na akifika shuleni bila mia tano Mwalimu atamchapa,nikampa mia tano. lakini vaa viatu vya Mtoto yule ambaye nyumbani anatolewa kwa fimbo kwa sababu hataki kuondoka analilia mia tano na Shuleni anajua anaenda kukutana fimbo ya Mwalimu,Mtoto wa miaka saba au name tu.Kuna tatizo.
 
-Kiwango cha chakula wapewacho huwa si zaidi ya vijiko vitatu vikubwa vya chakula

Daah! be serious aisee hata kama tunawachukia hao walimu, hv vijiko vitatu unavijua kweli?
 
Offside nyingi za umma zinegeuka kuwa vitega uchumi vya watu binafsi,acha walimu wafurahie maisha ya utumishi wao
 
Hakuna anayepinga bali uwekwe utaratibu bora zaidi na affordable kwa umma wote!
-Tunazungumzia maswala ya umma, hatuzungumzii maswala ya mtu mmoja mmoja!
Naamini Serikali kupitia sera yao ya Elimu Bure wana uwezo wa kufadhili chakula Bure Kwa shule zote nchini. Tatizo ni vipaumbele tu, Pesa nyingi zinaishia kwenye mambo ya hovyo yasiyo na tija kwa taifa
 
-Kiwango cha chakula wapewacho huwa si zaidi ya vijiko vitatu vikubwa vya chakula

Daah! be serious aisee hata kama tunawachukia hao walimu, hv vijiko vitatu unavijua kweli?
Facts!, am not joking!,
 
Wapite kwenye mashule mbalimbali hojini wanafunzi fanyeni udadisi ndipo waje hapa.
 
Suala la chakula ni muhimu sana kwa ukuaji wa mtoto. Serikali ikae chini na wazazi na kukubaliana kuhusu hilo suala. Kujidanganya kuwa elimu ni bure ni kuzidi kujididimiza kwenye umaskini. Wazazi wakilipa kiasi fulani kwa jumla ni bora kuliko hiyo Tsh 1500 kila siku. Wale wazazi wanaokwepa hata kununua sare za shule wakisingizia umaskini wakamatwe na kupigwa faini.
 
Jamaa mmesmshambulia hadi kafuta comment yake. Alaniwe
 
Uko sahihi, maana suala hili limekuwa KERO mbaya sana !
 
Tatizo ni kubwa hasa viongozi wa kitaifa wanakuwa kama vipofu ni fedheha,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…