Prof. Mkenda, Waziri bora na wa mfano

Prof. Mkenda, Waziri bora na wa mfano

Kaachivu Jambo gani ambalo limeleta matokeo chanya katika kilimo,maana Nasikia pembejeo za kilimo zimepanda Bei Sana.Naomba mnisaidie maana Tanzania akitokea mwanasiasa akawa anajua Sana kujieleza basi anakua bora,naomba ufafanuzi
Tanzanians proffessionals not practical oriented,not results oriented,not measured on achievements,not strategic.
Only talkings then you become the best leader/expert.
Lol[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo sio kuongeza bajeti ya fedha, miaka mingi fedha zinatolewa lkn hakuna cha maana zaidi ya kula fedha za umma.
tunataka wataalamu wetu.wawe wazalendo wa kweli kwa nchi yao, wajitume vilivyo hata kama pesa ni kidogo, kuna maeneo wala hayahitaji pesa bali yanatakiwa kujituma tu.
tuache porojo tuchape kazi kwa manufaa ya Taifa letu.

..Nakubaliana na wewe 100%.

..moja ya matatizo ya wakulima wetu ni uzalishaji mdogo per hectare.

..kwa mfano chikichi tunazalisha tani 2 mpaka 5 per hectare wakati washindani wetu kama Malaysia wanazalisha mpaka tani 10 per hectare.

..mpaka hapo utaona kwamba tunahitaji mbegu bora ili kuongeza uzalishaji.

..sasa ili upate mbegu bora lazima uwekeze ktk UTAFITI / RESEARCH.

..Tunatakiwa tuwekeze ktk mafunzo, vifaa, maabara, na mashamba ya mbegu.
 
Ni mnyenyekevu
Msomi
Hajikwezi
Mchapakazi.
Anayebisha asikilize kipindi cha dk.45 ITV na radio one leo hii.
Huyu waziri kwa kweli yupo vizuri kwenye kazi yake na angefaa kwenye nafasi kubwa zaidi sio hawa akina bi kidude wasioeleweka.
 
Maafisa kilimo wameajiriwa kibao, wapo ktk kila halmashauri za nchi hii lkn wanakula mshara na kulima mashamba yao tu, wala hawana mpango wa kutumia taaluma yao kukuza uzalishaji wa kilimo kwa wakulima wa maeneo husika.
wakurugenzi wapo, ma das wapo, ma DC wapo ma rc wapo hakuna mwenye uchungu kila mmoja anahangaika na tumbo lake
 
Maafisa kilimo wameajiriwa kibao, wapo ktk kila halmashauri za nchi hii lkn wanakula mshara na kulima mashamba yao tu, wala hawana mpango wa kutumia taaluma yao kukuza uzalishaji wa kilimo kwa wakulima wa maeneo husika.
wakurugenzi wapo, ma das wapo, ma DC wapo ma rc wapo hakuna mwenye uchungu kila mmoja anahangaika na tumbo lake
Unataka walime mashamba ya nani?
 
Hamzidi jiwe kwa akili bana
jiwe alikuwa anajua idadi ya samaki na mayai yake kwenye kila ziwa. Anajenga gorofa lenye floor nne pale UD kwa 50m. Huyo Propesa atawezaaa
Yaaah jiwe alikuwa na akili sana. Pia alijenga uwanja wa ndege kijijini kwake kwa pesa ya walipa kodi. Siku hizi tunaona watii wengi wakienda Chato kupumzika!
 
DAP tulkuwa tunanunua kwa 55,000 kwa mfuko. Siku hizi ni 90,000. Bado unasema wizara ina mawaziri wazuri. Usinidanganye.
Wameshindwa kuuthibiti mfumo wa uagizaji wa pamoja, eti wamewaachia wafanyabiashara washindane? Binafsi sijawahi kuona kama wafanyabiashara wa sekta moja wanaweza wakaachwa washindine wao kwa wao. Hayo ndiyo matokea yake, wafanyabiashara wanajiamlia bei za kuuza mbolea. Mfuko umetoka 55,000/= hadi 90,000/=.
Halafu ngonjera wanazokuja nazo ni eti kiwanda kinajengwa. Nani awekeze kujenga kiwanda wakati anaweza kuagiza mbolea kokote na akaiuza kwa bei yoyote?
Toka nimewafahamu wafanyabiashara sijawahi kujua kama wafanyabiashara wanaweza kushindana wao kwa wao.
 
Yaaah jiwe alikuwa na akili sana. Pia alijenga uwanja wa ndege kijijini kwake kwa pesa ya walipa kodi. Siku hizi tunaona watii wengi wakienda Chato kupumzika!
Hivi Tanzania tunafanya maendeleo kwa ajili ya akina nani?
 
ila anapenda sana kujionyesha kwenye tv.
aache show of, achape kazi, wananchi wanataka kuona matokeo sio maneno mengi na kuonekana kwenye tv.
bado safari ni ndefu, muda wa kujipongeza bado sana.
Hivi uliiona ile picha anakulana kiss na mkewe kisa anaenda kuwasilisha hotuba ya bajeti?
 
inawezekana akawa bora kwenye kujenga hoja na mikakati kem kem lkn hiyo pekee haitoshi kumpa sifa, tunacho taka ni kufanikisha kile unacho kipanga kilete mabadiliko ktk sekta ya kilimo.
bado usimamizi wake ni mbovu.
nasema maafisa kilimo wapo kila wilaya na hakuna impact yoyote kwenye kilimo.

wiki iliyo pita takribani tani 20 ya viyatilifu ilikamatwa huko mtwara ikitokea dsm, wakulima wanalalamika hawapati pembejeo kwa wakati na zenye kutosheleza mahitaji, wakulima hadi leo bado hawana masoko ya uhakika ya kuuza mazao yao. n.k.
sasa eti unamsifia waziri yuko vizuri sana.
 
Nakubaliana na wewe ni waziri mzuri lakini siyo kwa sifa za kijinga kama hizo ulizoweka hapo.

Hata msaidizi wake ni waziri mzuri.
Safari hii Kilimo kimepata mawaziri wenye hadhi stahiki kwa wizara hiyo muhimu sana.
Mpaka sasa mbolea imepanda bei kwa asilimia mia moja.

Je hiki ndiyo kipimo cha ubora wa huyu waziri ?
 
DAP tulkuwa tunanunua kwa 55,000 kwa mfuko. Siku hizi ni 90,000. Bado unasema wizara ina mawaziri wazuri. Usinidanganye.
Wanaomsifia yawezekana siyo wakulima wanasikiliza maneno matupu hawajui wakulima wanapitia nini katika kipindi hiki.
 
DAP tulkuwa tunanunua kwa 55,000 kwa mfuko. Siku hizi ni 90,000. Bado unasema wizara ina mawaziri wazuri. Usinidanganye.
Waziri aliyefanya vizuri kwenye wizara ya kilimo ni mzee Steven Wassira tu na waziri aliyemalizia wakati wa mzee Kikwete.

Chini ya Magufuli wizara ya kilimo haijawahi kuwa na waziri ilikuwa na wazururaji tu.
 
DAP tulkuwa tunanunua kwa 55,000 kwa mfuko. Siku hizi ni 90,000. Bado unasema wizara ina mawaziri wazuri. Usinidanganye.
Mkuu 'Lihanga', Waziri hana mamlaka juu ya soko la mbolea duniani. Umekwishacheki bei ya DAP ilivyopanda duniani? Unataka aweke 'subsidy'au...! Lakini si kuna zile mbadala zitakazouzwa kwa bei ile ile ya msimu uliopita, au kuna kasoro juu ya hizo mbolea mbili za kupandia?

Hili linabidi tuzungumzie kiwanda chetu cha mbolea Lindi. Unakikumbuka? Kilizungumziwa toka gesi ugundulike huko, lakini hadi leo ni hadithi tupu!
Soko la mbolea Afrika nzima tungelishika kama kiwanda hicho kingekuwa tayari kinafanya kazi. Siku hizi hata kukizungumzia tu ni aibu!
 
Mpaka sasa mbolea imepanda bei kwa asilimia mia moja.

Je hiki ndiyo kipimo cha ubora wa huyu waziri ?
Hiki ndio kiwe kipimo cha utendaji wa waziri ndani ya wizara?
Bei ikipanda maradufu kama ilivyo sasa hivi duniani, waziri afanye nini, atoe 'subsidy'? Mbona huu sio uamzi wa waziri pekee yake!
 
Wanaomsifia yawezekana siyo wakulima wanasikiliza maneno matupu hawajui wakulima wanapitia nini katika kipindi hiki.

..tofauti na wanasiasa wengine nadhani Mkenda na Bashe wako open minded.

..nimewasikia mara kwa mara wakisema wako tayari kuwasiliza wadau wa kilimo ili kutatua changamoto zao.

..binafsi I want to see them implement kile walichoahidi tuone kama kitatoa matokeo mazuri.
 
Yupo vizuri sana. Ila hana Kiki ndio maana sio maarufu. Jamaa anafaa sana kuwa Rais wa Tanzania. Changamoto hana Kiki.
Kwa Tanzania hii ya leo, kiongozi yoyote aliyetulia, mnyenyekevu, asiye na ma-scandal ni dalili nzuri. Kuna huyu waziri wa Ulinzi aliyefariki. Naye anaonekana alikuwa kiongozi mtulivu. Unyenyekevu, utulivu, kutojikweza imekuwa bidhaa adimu sana kwa viongozi wengi wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom