Prof. Mkumbo: Kila Mtu amlinde mtoto wake, kuna watu kwa tamaa wanawateka watoto

Prof. Mkumbo: Kila Mtu amlinde mtoto wake, kuna watu kwa tamaa wanawateka watoto

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
1721756420371.png

Prof. Mkumbo

Kufuatia hali ya sintofahamu iliyoripotiwa kutokea eneo la shule ya msingi iliyopo Mburahati Kata ya Mkurumla iliyopo Wilaya ya Ubungo kwa wazazi na walezi kukusanyika kwenye eneo la shule kutokana na hofu ya madai ya watoto kutekwa, Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo amefanya mkutano kwenye Kata hiyo huku akiwahasa wananchi kuchukua tahadhari kuwalinda watoto wao.

"Kuna watu wachache katika jamii yetu kwa kuwa na tamaa aidha ya kupata mali kwa njia za mkato wanateka watoto, kila Mtu amlinde mtoto wake” amesema Prof. Kitila Mkumbo

Aidha Prof. Mkumbo ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa vyuombo vya dola ili jambo hilo kama lipo liweze kudhibitiwa na kuondoa hofu.

Jana Julai 22, 2024 baada ya sintofahamu iliyotokea Mburahati, Jeshi la Polisi kuipitia Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam Jumanne Muliro alitoa taarifa akidai kuwa madai ya watoto kutekwa kwenye eneo hilo hayakuwa na ukweli, huku akitaka watoto kuendelea na masomo bila hofo.

Hata hivyo baadhi ya shule jijini Dar es salaam imeshuhudiwa wazazi na walezi wakiwapeleka na kuwafuata watoto wao mashuleni ikielezwa kuwa chanzo ni sintofahamu ambayo imekuwepo.

Chanzo: Wasafi FM
 
Hivi haya mambo ya watoto kutekwa ni kweli au ni porojo za mitandaoni?
 
Back
Top Bottom