Prof. Muhongo amuunga mkono Prof. Mwandosya, TCU kimya!

Prof. Muhongo amuunga mkono Prof. Mwandosya, TCU kimya!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Prof. Muhongo amewalima akina Doto Biteko na cohort nzima ya PhD ( P engine h ana D egree. Someni wenyewe hapa chini:

"Naomba niwasaidie: comments za Prof Mwandosya zichukuliwe kwa uzito wake unaostahili. Tuko kimya siyo kwamba hatujui ukweli wa ukweli.

Kwanini msiombe yafuatayo:

1. Abstract of the PhD thesis/dissertation

2. Conclusions or Concluding Remarks of the PhD thesis/dissertation

Mkisoma hayo mtafanya uamuzi wa ubora wa PhD mnazozijadili.

Vilevile, mnaweza kupenda kuwafahamu:

3. Supervisor(s), who is (are) the Internal Supervisor(s)

4. External Examiner(s)

Muhimu zaidi, PhD nzuri itatoa publications kwenye International journals zenye measurable IMPACT FACTORS (IF) ambazo zinaheshimika zitakuwa na range ya O.75-10. Manuscripts zipelekwe huko ziwe published kwenye journals zenye hadhi hiyo ya average to good Impact Factor (IF) or Citation Index (IC).

Mengine yote yako nje ya "the realm of academia."

S Muhongo
17.12.2021"

MY TAKE:
Haya sasa TCU wako kimya kama maji ya mtungi.

Vigezo vya PhD vinabakwa mchana kweupe, wao kimyaaa!

IMG-20211219-WA0023.jpg

Kwa maprofesa nguli kama hawa kuhoji, kuna kitu nyuma ya pazia! Ni jukumu sasa la mamlaka ya udhibiti wa elimu ya juu nchini (TCU) kutoa majibu fasaha. Kama kuna michezo wanasiasa wanafanya kuchezea elimu angalau wawili watatu wawe mifano kukomesha hali hii for good!

Wekeni hizo abstracts, conclusions, na supervisors online watu wapitie; hata hizo theses hazitakiwi kuwa siri. Ziwekwe public pengine watafiti wengine wangependa "kuanzia walipoishia" kwenye tafiti mpya.
 
... kwa maprofesa nguli kama hawa kuhoji, kuna kitu nyuma ya pazia! Ni jukumu sasa la mamlaka ya udhibiti wa elimu ya juu nchini (TCU) kutoa majibu fasaha. Kama kuna michezo wanasiasa wanafanya kuchezea elimu angalau wawili watatu wawe mifano kukomesha hali hii for good!
Dr Mwigullu

Dr Makamba

Dr Jaffo

Dr Biteko

Dr Nchimbi

Dr Makonda

Dr Gwajima

Dr Slaa

Dr Msukuma
 
Kwa mara ya kwanza Muhongo kaongea point. Point kubwa na ya msingi ni kwamba akina Sospeter wangebaki vyuoni kama maprofesa wangekuwa useful zaidi kwenye jamii kuliko walivyoingia kwenye siasa.
Mkuu siasa ni tamu sana kuliko lubaki chuo unakimbizana na remote director
 
Prof. Muhongo amewalima akina Doto Biteko na cohort nzima ya PhD ( P engine h ana D egree. Someni wenyewe hapa chini:

"Naomba niwasaidie: comments za Prof Mwandosya zichukuliwe kwa uzito wake unaostahili. Tuko kimya siyo kwamba hatujui ukweli wa ukweli.

Kwa nini msiombe yafuatayo:

1. Abstract of the PhD thesis/dissertation

2. Conclusions or Concluding Remarks of the PhD thesis/dissertation

Mkisoma hayo mtafanya uamuzi wa ubora wa PhD mnazozijadili.

Vilevile, mnaweza kupenda kuwafahamu:

3. Supervisor(s), who is (are) the Internal Supervisor(s)

4. External Examiner(s)

Muhimu zaidi, PhD nzuri itatoa publications kwenye International journals zenye measurable IMPACT FACTORS (IF) ambazo zinaheshimika zitakuwa na range ya O.75-10. Manuscripts zipelekwe huko ziwe published kwenye journals zenye hadhi hiyo ya average to good Impact Factor (IF) or Citation Index (IC).

Mengine yote yako nje ya "the realm of academia."

S Muhongo
17.12.2021"

MY TAKE:
Haya sasa TCU wako kimya kama maji ya mtungi.
Vigezo vya PhD vinabakwa mchana kweupe, wao kimyaaa!
Ni vitu vya kushangaza sana. Musukuma tunaelewa hiyo takataka ameipata toka kwenye takataka huko India.

Yaani huyu Biteko na Jafo, ambao hata ukijadiliana nao, ni vigumu kufikiria wana viwango hata vya shahada za pili, leo eti wana PhD.

Kwa hili, UDOM imeonekana ni chuo takataka. Hata hao lecturers na professors wa UDOM, kuna taarifa pia hawana viwango vinavyotakiwa. Waligawana uprofesa na udokta kama mahindi ya kuchoma.

Kwanza wachunguzwe hao lecturers, pili hawa waliopewa PhD za michongo waundiwe tume ya kitaluma. Chuo kitazamwe upya, na kufanyiwa marekebisho makubwa ili kitoe elimu yenye ubora.
 
Back
Top Bottom