Prof. Muhongo amuunga mkono Prof. Mwandosya, TCU kimya!

Prof. Muhongo amuunga mkono Prof. Mwandosya, TCU kimya!

Prof. Muhongo amewalima akina Doto Biteko na cohort nzima ya PhD ( P engine h ana D egree. Someni wenyewe hapa chini:

"Naomba niwasaidie: comments za Prof Mwandosya zichukuliwe kwa uzito wake unaostahili. Tuko kimya siyo kwamba hatujui ukweli wa ukweli.

Kwanini msiombe yafuatayo:

1. Abstract of the PhD thesis/dissertation

2. Conclusions or Concluding Remarks of the PhD thesis/dissertation

Mkisoma hayo mtafanya uamuzi wa ubora wa PhD mnazozijadili.

Vilevile, mnaweza kupenda kuwafahamu:

3. Supervisor(s), who is (are) the Internal Supervisor(s)

4. External Examiner(s)

Muhimu zaidi, PhD nzuri itatoa publications kwenye International journals zenye measurable IMPACT FACTORS (IF) ambazo zinaheshimika zitakuwa na range ya O.75-10. Manuscripts zipelekwe huko ziwe published kwenye journals zenye hadhi hiyo ya average to good Impact Factor (IF) or Citation Index (IC).

Mengine yote yako nje ya "the realm of academia."

S Muhongo
17.12.2021"


MY TAKE:
Haya sasa TCU wako kimya kama maji ya mtungi.

Vigezo vya PhD vinabakwa mchana kweupe, wao kimyaaa!

View attachment 2050012

Pengine atatizo yote yanaanzia hapa:

1639982595489.png


Toka website ya UDOM
Huyu Hon. Stargomena Lawrence Tax ndiye CHANCELLOR.
Ana Dr.Phil ya Japan

1639982784190.png

Huyu Hon. Gaudentia Mugosi Kabaka
Huyu ndiye CHAIRMAN (au Chairperson)of the University Council.
Preoffesion: Teacher, Graduate wa Kleruu TTC, Chairperson wa Umoja wa Wanawake CCM


JF I rest my case!
 
Pengine atatizo yote yanaanzia hapa:

View attachment 2050754

Toka website ya UDOM
Huyu Hon. Stargomena Lawrence Tax ndiye CHANCELLOR.
Ana Dr.Phil ya Japan

View attachment 2050758
Huyu Hon. Gaudentia Mugosi Kabaka
Huyu ndiye CHAIRMAN (au Chairperson)of the University Council.
Preoffesion: Teacher, Graduate wa Kleruu TTC, Chairperson wa Umoja wa Wanawake CCM


JF I rest my case!
Du...watu mnachimba!
Mwalimu wa sekondari ni mwenyekiti wa Univerdity Council na Umoja wa Wanawake CCM!
 
Suluhisho hapa ni kupata katiba bora ambayo itaweka maslahi bora ya wataalam wetu kuliko maslahi ya wanasiasa hilo litachochea ushindani kwenye elimu yetu na kupata viwango vya elimu vyenye hadhi ya juu kabisa.
Hilo la kuheshimu wataalamu na kuwalipa istahilivyo wala halihitaji katiba mpya ni suala la common sense tu. Kwani
 
Wahitimu wa ukweli kwa levels zote hapa Tanzania waliishia miaka ya 1990s.

Wahitinu wa kuanzia mwaka 2000 wengi wao hawaendani ata na walichokisoma eg.unakuta mtu graduate hajui ata kuandika barua na cv achilia mbali kujibu maswali kwenye interview.
Yote hayo ni matokeo ya nchi kutoweza kutambua talent na kuretain talents. Kipindi niko undergraduate kuna daktari mmoja wa falsafa aliajiriwa na udsm kutoka mashirika fulani ya kimataifa lakini alitufundisha semester moja tu. Siku moja (hiyo ilikuwa 2005) nilimsikia akisema walau saa hivi lecturer udsm wanalipwa vizuri ndiyo maana ameshawishika kurudi nyumbani but haikuchukua muda akajisepa maana alipata dau bora zaidi. Aliyekuja kutufundisha badala yake simtaji lakini ukilinganisha quality za hawa watu wawili you can imagine kwa nini nchi inabidi iwekeze katika kutambua watu bora na kuwaretain katika nchi hii.
 
Naelewa vibaya au kichwa changu ndiyo kibovu.Kwamva study ni Garisa Kenya badala ya Kisarawe Pwani.Au ni comperison study.Kuna haja ya kuweka hizo abstract ya hizo studies tuzielewe
Na wao hawataki kuziweka hizo kazi zao online Ili watu wajiridhishe ukute wanatuhumiwa kihisia, hafu huwa nawaza kwanini tafiti za wasomi wa Tanzania huwa hawaziweki online watu wazisome tofauti na nchi ka ya Nigeria na Kenya ni Rahisi kupata different studies zao tofauti na bongo, huku tuna kwama wapi?
 
Na wao hawataki kuziweka hizo kazi zao online Ili watu wajiridhishe ukute wanatuhumiwa kihisia, hafu huwa nawaza kwanini tafiti za wasomi wa Tanzania huwa hawaziweki online watu wazisome tofauti na nchi ka ya Nigeria na Kenya ni Rahisi kupata different studies zao tofauti na bongo, huku tuna kwama wapi?
Mkuu aziweke thesis za mchongo online halafu waadhirike wote waliohusika kutoa nadudu?
Vitu vya rushwa vinafanywa gizani!
 
Kama Prof. Muhongo hajasoma abstract zao, kama hajasoma conclusions, kama hajui internal supervisor(s) ni akina nani, kama hajui external examiner(s) ni akina nani na kama hajui wamepublish wapi papers zao zilizowasaidia kugraduate anapata wapi sababu ya kuwa na wasiwasi na PhD za hao waheshimiwa? Hapo ni kama ule msemo wa Waingereza wa "jumping the gun". Lakini pia anayesema TCU iko kimya, sidhani kama ni sahihi. Kazi ya TCU ni kutoa ithibati ya program lakini Senate za vyuo husika ndio zina wajibu wa kuhakikisha wanatoa PhD zenye viwango. TCU hawasimamii wanafunzi wa PhD bali wahadhiri walioidhinishwa na Senate. Maswali ya kujiuliza ni je hao waheshimiwa wamepitia michakato yote ya kupata PhD zao? Senate wameridhika kuwa kilichofanyika kinakidhi viwango vya PhD? Wamepublish kwenye majarida yanayotambuliwa na UDOM? Kama jibu ni ndio, huu wasiwasi wa maprofesa wenzangu unatoka wapi? Kwamba kupata PhD ni mchakato mgumu na hivyo waziri ambaye yuko busy na shughuli za kiofisi hawezi ni hoja isiyo na mashiko.
Unabisha utumbo tu. Hakuna Thesis za hawa Wana siasa kwenye website za vyuo husika. Full PhD Thesis ya Graduates inapaswa kuwa online. Pili, Dotto ana publication 1 tu online. Wakati matakwa ya PhD ni 2 ili u graduate. Tatu, PhD una paswa u publish paper yako ktk international Journal siyo Local tena ya Chuo cha MoCU.
Pia hawa inasadikika walianza chuo 2018/2019 as part time student. Uwe Waziri na Mbunge u graduate PhD 2021. Haiwezekani huenda chuo cha Uganga!!
 
Na wao hawataki kuziweka hizo kazi zao online Ili watu wajiridhishe ukute wanatuhumiwa kihisia, hafu huwa nawaza kwanini tafiti za wasomi wa Tanzania huwa hawaziweki online watu wazisome tofauti na nchi ka ya Nigeria na Kenya ni Rahisi kupata different studies zao tofauti na bongo, huku tuna kwama wapi?
hawaweki kazi public kwa sababu ni copy paste zaidi kuliko mawazo mapya.yaani hakuna contributio to new knwoledege.repeatiom of what others have already said
 
Kuna shida kabisa hapa. Nimependa interventions za maprof wetu wakongwe. Tunaona elimu yetu inabakwa mchana kweupe na wanasiasa. Nahili naona linachimbuko toka Era iliyopita kwa kuwachagua maprof/PHD wengi kwenye siasa, sasa kila mtu anaona PHD ndio qualifications for polical post nakuzitafuta kwa udi na uvumba hata kwa njia za panya. Serikali iiingilie kati otherwise University zetu zitakuwa blacklisted for issuing fake PHDs.
 
hawaweki kazi public kwa sababu ni copy paste zaidi kuliko mawazo mapya.yaani hakuna contributio to new knwoledege.repeatiom of what others have already said
Inasikitisha sana Yani ma Prof wabobevu ni nadra kukuta wamepost online, Bora ma Prof wa SUA ni rahisi ku access tafiti zao na ziko online hata ukiingia kwenye academia, au research gate kiurahisi.
Waziri wa elimu aje na mikakati mizuri ya kuhakikisha elimu yetu inaboreka zaidi
 
Umesahau huyu:
Dr Ndugai [emoji849]
Nimeshangaa ni kwanini Ndugai hajachukua PhD yake pale UDOM hadi sasa.
Wakati kwa sasa ile kazi yake tu anapata PhD.
Kama alivyo pata Dr. Msukuma kwa kazi yake ya Usafirishaji abiria kwa usalama.
 
Back
Top Bottom