Prof. Mukandala: Meli ya MV Bukoba ilifanya kazi Tanzania kwa miaka 17 bila kusajiliwa na haikupaswa kuletwa nchini

Bado umeamua kuendelea kudanganya

Mkandala,amejikita kupitia hoja zilizoibuliwa na jaji kisanga,hilomosi

Pili, tume,inaonesha tanzania hakuna tenda imewahi tangazwa kununua hiyomeli ila Belgium tenda ilitangzwa

Tatu ,inakuwaje meli iserereke majini

Mwisho ,hoja ni mabadiliko yakatiba na kupunguza maagizo yamtu mmoja kuathiri watanzania
 
Uzuri ni kuwa inaonesha umeandika tu ila huielewi historia ya Profesa Rwekaza Sympho Mukandala hata kidogo.
Msimshangae ,inaonesha walisubiria mwanafunzi wao Tundu lisu awe mwanasiasa na aseme ubovu wakatiba ili waibue hojazaon
 
Ulimuelewa alipogusia Dola na soko?
...........................................
Rudia kusikiliza tena utapata majibu kwa nini alihitimisha na mabadiliko ya katiba. Mkuu ile inaitwa " inaugural lecture" hawakurupuki hata kidogo pale ndugu yangu.
Fact juu ya fact.
 
Sitaki kurudia yaleyale,jenerali ulimwengu kamaliza kazi ,kwamba mawaziri mkopale kwajili yanini ,wakati kichwa panzi kimoja kinaweza amua kilakitu hivyo hata meli hiyo inaweza ikawa ilinunuliwa kwa kauli ya mtu mmoja tu na ikaua watu 2000.... nani alilipwa fidia ? Yatima wangapi malengo yao duniani hayakutimia kisa ajali

Harafu unambie mambo ya soko , kweli soko hilo lilizingatia utaratibu ,tenda ilitangazwa wapi nchini
 
Uzuri ni kuwa inaonesha umeandika tu ila huielewi historia ya Profesa Rwekaza Sympho Mukandala hata kidogo.
Nahitaji kujua historia ya mkandala ? Au nijikite kwenye tafakuri yake namwelewa in-out sijui wewe unayekuja na maneno ya jumla....
 
Wanajadili jambo hili kulalamikia ununuzi wa meli hiyo kama vile meli hununuliwa kwenye boksi ikiwa imeshafungwa. Meli hiyo ya MV Bukoba ilijengwa pale Mwanza South kuanzia bati la kwanza hadi la mwisho na shughuli zote za ujenzi wake zilisimamiwa pamoja na vyombo vingine TRL ambao ndio walikuwa wamiiki wake.

Hapa kuna ktafuta mwanya wa kupindisha ukweli ilin isomeke kwamva meli ilinunuliwa ikiwa mbovu au haifai, wakati ukweli halisi ni kuwa ilizama kutokana na unedeshaji na usimamizi mbovu. Tatizo la Management hapa Tanzania ni jadi yetu. Huwezi kujaza meli iliyoundwa kubeba watu 500 wewe ukajaza watu 1300 na mizigo halafu utafutae mchawi kwa Nyerere.

Kukosekana kwa ballast tanks kwenye meli siyo ubovu wa meli au rushwa kwenye ununuzi wa meli hiyo, bali huo ni uendeshaji mbovu tu; kama kuendesha roli bila kuwa na spare tyre. Ballast tanks ni detachable, zinawekwa na kuondolewa wakati wowote na mtumiaji. kuna maorofesa wanakosa mada za maana za kuelezea umma, wanakimbilia cheap conclusions za mambo wasiyokuwa na uelewa nayo.
 
Jenerali Ulimwengu hakumaliza ila alikazia rejea aliposema "Imperial President" ni kama alivyowahi kusema "Godfathers". Kwa kifupi mhadhara ndiyo uliomaliza.
 
Captain,Chief Officer, meneja wa shirika La meli wote walikuwa wazoefu na wana elimu na ujuzi mkubwa wa mambo ya meli
 
Jenerali Ulimwengu hakumaliza ila alikazia rejea aliposema "Imperial President" ni kama alivyowahi kusema "Godfathers". Kwa kifupi mhadhara ndiyo uliomaliza.
Mlaki

Wewe nimchaga, iko hivi yoooote,ishu ni katiba mpya kama alivyomaliza mkandala ,mkuu wa chuo alikuwepo pake jakaya Sinia,mbunge mstaafu wa bunge la G-55 ndg Jenerali ulimwengu ambao ndo wabunge waliodai kurejrshwa kwa tanganyika

Tafsiri yake,kwamba wabunge hao ,waligomea mtu mmoja kuiingiza tanganyika majaribunu

Tujisahihishe
 
Huenda Mimi nautazama huu Muhadhara kwa namna tofauti na wengine.
Leo ,binafsi nimejifunza dai katiba mpya limekuja kwanjia mpya kupitia wasomi

Hoja ya mkandala ,kwamba nchi hii mtu mmoja anaweza fanya jambo kwaniaba ya watu million 60 bila kujali madhara ,kwahiyo katiba mpya ni suluhu ,sasa mkandala akajikita kwenye meli hiyo ,maamuzi yake yalikuwa ya mtu mmoja bila utaratibu wa tenda ,nk
 
hivyo unataka tuamini kuwa maelezo yake kuhusu Mv Bukoba yote ni taaarifa za tume Jaji Kisanga? Hata za yule Nahodha wa Kenya aliyenukuliwa na magazeti ya Kenya? Umejiridhisja hata google? Si Prof huyu ambaye amesema amepitia taarifa kutoka vyanzo mbalimbali?

Suala la Tanzania kununua meli hiyo bila tenda kutangazwa. Kwanini umechaguliwa mfano wa Mv Bikoba pekee? Je awamu zilizofuata mpaka hii ya Dp world tenda zinatangazwa wapi, kwanini Nyerere?
Kama mnajadili mabadiliko ya katiba fanyeni hivyo kwa nia njema, acheni ajenda zenu au pia mziweke wazi ili tukisoma tujuie hili linatokana na suala hili.

kama mdau mmoja aivyoeleza hapo juu, meli haikupinduka na kuzama kwa kununuliwa bila tenda, Je ni tenda na Nyerere walioagiza ibebe abiria na mizigo kuliko uwezo wake?

Mnasema Nyerere aliweza vipi kuwaburuza mawaziri na viongozi wengine waandamizi wakati mlikuwepo na wengine wa kundi la G 55 ambao na wingi wao hoja yao ilizimwa pia lakini hawatwambii kilitokea nini.
 
Makuli waliopakia mzigo ndo hawakuwa na weledi(kitengo hicho) kwamba mzigo umezidi na hawaelewi
Melini anayesimamia zoezi la upakiaji mzigo na kuandaa Stowage plan ni Chief officer na anakuwa kila baada ya muda fulani anasoma Draft mark za meli kujua mzigo upo kiasi gani na wapakie upande upi ili kuweka usawa katika meli
 
Melini anayesimamia zoezi la upakiaji mzigo na kuandaa Stowage plan ni Chief officer na anakuwa kila baada ya muda fulani anasoma Draft mark za meli kujua mzigo upo kiasi gani na wapakie upande upi ili kuweka usawa katika meli
Pamoja na hayo ilizima na mwisho wa siku ,moja ya sababu meli kuzama ilikuwa kuzidisha mzigo na abiria hayoyote kwenye draft mark ,mtaalam hakuona
 
Sio watu wa kujifunza huko serikalini kwenye jukwaa la habari kuna mada mtambo umelipuka huko Mtibwa kwenye kiwanda cha sukari na kuuwa watu 11.

Sasa sio rocket science uchunguzi ukikamilika tutakujua kuambiwa mashine ilikuwa chakavu, na kutumia ilikuwa ni ajali ambayo inasubiri kutokea.

Worst kama repair ya mtambo itachukua muda badala ya body ya sukari kuanza mikakati ya kufidia production shortage inayofuata. Wao watasubiri mpaka upatikanaji wa sukari uwe shida, ulanguzi uanze, serikali ivamie maghala ya watu, kutafuta mbuzi wa kafara ndio wafikirie kuagiza. Huko nako kuna siasa nani apewe kibali cha kuagiza.

Hapo hapo wanatuambia kuna mwarabu anataka kuleta mabasi 400 kwa mpigo, wapi unaweza kwenda kununua idadi hiyo bila ya kutoa order kwanza na kusubiri mwaka mmoja hadi miwili. Maana yake huyo mwekezaji kama anayo mabasi 400 kwa sasa chances are ni reconditioned, halafu wenyewe wanakwambia akirudisha hela yake anawaachia serikali hayo, hapo anaacha nini zaidi ya mikweche ya kupeleka scrap yard.

Only in Tanzania
 
Umeifanya siku yangu kuwa muruwa sana.
 
Umeifanya siku yangu kuwa muruwa sana.
Kila nikirejea alichosema kukisikiliza

Naweza fikili kwamba ile ajali ya meli ,haina tofauti na mauji ya chakechake pemba zanzibar

Ila ,tofauti yake mwanza hayakuwa ya mkono wachuma(bunduki), mkapa anakili wazi kwamba mpaka anaandika kitabu chake moja ya vitu kumuumiza ukiachana na wizi wadola 1000 uliofanywa ikulu nawahuni waliomshawishi

KINGINe
Nimauwaji ya chakechake ,alitoa amri akiwa jeniva ila anajitetea kwamba hakuwaagiza vyombo hivyo kuua raia ,sasa ikatokea wameua

LAKINI
Kutokana na nguvu mudawote kutoka kwamtummoja Dodoma chamwino , x-president Dr karume jr aliwakatalia ccm katakata kwamba sasa tunahitaji zanzibar katiba mpya,machafuko ya chakechake na maswahibu mengine inside zanzibar na upinzani imara wa maalim seif (cuf),ukapelekea kupatikana katiba yao ya serikali ya umoja wa kitaifa ,japo imetibu mengi mengine yamebakia washenzi tu kung'ang'ana ila yataenda mwisho

Ndomana sasa

Ukifatilia ile hotuba ya mkandala ,utangundua mambo mawili makuu ambayo ni dola na soko......... ukichimba zaidi Tanzania dola ndo inamiliki soko ,lakini maamuzi yadola yako dhaifu kwasababu yanategemea nguvu ya mtu mmoja ndomana soko pia linakuwa dhaifu

Kwa mauaji yale kwanjia ya meli ,ilitakiwa serikali ijiuzulu ila serikali ilikimbilia mahakamani yenyewe kumbe udhaifu wote wameli ile ,nizao la katiba

Tuanzie ,hapo na mikutano ya chadema nchizima ,LISU anaweza kutumia hoja zamkandala kuitawanya ccm

UVCCM wajipange mana kwenye muungano ,wameambulia patupu kujibu hoja
 
Meli ilijengwa 1979, ikazama 1996, maana yake imefanya kazi miaka 17, sidhani kama ingeweza kusurvive 17yrs kama ingekuwa ina big manufacturer errors

Ujinga ujinga wetu na mizaha ndio vilivyozamisha Ile meli.
 
Meli ilijengwa 1979, ikazama 1996, maana yake imefanya kazi miaka 17, sidhani kama ingeweza kusurvive 17yrs kama ingekuwa ina big manufacturer errors

Ujinga ujinga wetu na mizaha ndio vilivyozamisha Ile meli.
Naam!...haswaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…