kina kirefu
JF-Expert Member
- Dec 14, 2018
- 15,188
- 18,583
Bado umeamua kuendelea kudanganyaMhadhara wa Prof. Huyu umenikumbusha mambo yalivyokuwa kipindi cha wakati na baada ya ajali iiyo ya kusikitisha kuwahi kutokea katika ziwa Victoria.
Prof. Kaeleza mambo mengi kuzunguka ajali hiyo ambayo mengine labda hakukaririwa vyema au yana malengo fulani ambayo yatajulikana kadri muda unavyokwenda.
Mimi ni mhitimu wa darasa la saba b, hivyo mambo ya kisomi nawaachia wenye sifa hizo.
kwa mtazamo wangu mhadhara huu wa prof hasa katika suala la Mv Bukoba una mapungufu na uko sawa na tunayoifanya huku mtaani na kusikiliza wachambuzi wa sasa wa soka kwenye radio zetu, kama bado zina sifa ya kuitwa hivyo.
Nilikuwa Mwnza mjino siku ya ajali na muda mwingi baada ya ajali hiyo na story nyingi za vijiweni zilisambaa kama anavyoeleza prof.
Story kwamba, mmiliki wa vivuko vinavyotoa huduma kati ya mwanza na kamanga, kuzuiliwa kutumia meli zake kuivuta Mv Bukoba ili isizame, mkuu wa mkoa wa wakati huo methew( sina uhakina na jina la kwanza) Luhanga, kuagiza meli kutobolewa ili kuwakoa walioko hai ndani ya meli nk.
Nilihudhuria vikao kadhaa vya kesi ya Mv Bukoba ambapo Jaji Jaxton Mlay wakati akiwaapisha wazee washauri alisisitiza kuwa wasikilize na kutoa maamuzi yao kulingana na kitakachotokea mahakamani na sio walichosikia mitaani.
Kulinganna na Prof. Kuna mambo kadhaa naomba niyaeleze.
1. Meli haikusajiliwa. Hapa kuna utata. Ingawa ni kweli meli ilikuwa na tatizo la uwiano majini. Lakini, IMO ilitoa namba 763611 kwa chombo gani? Hukumu ya jaji Mlay inaeleza Mv Bukoba ilikuwa na Usajili au Prof ana eleza juu ya certficate of sea worthness? Mv Bukoba haikuwa nayo?
2. Nahodha alijiokoa kwanza kabla ya abiria. Sijui kama Prof anafahamu hiyo meli ilipinduka na haikuzama, maana kwenye kuzama taratibu nyingi zinaweza kufuatwa lakini kupinduka ni tendo la ghafla. Sidhani kama amewahi kusikia kuwa kuna abiria walirushwa kutoka kwenye meli hiyo na kujikuta ziwani ambako walijiiokoa kwa mikungu ya ndizi.
Vinginevyo, kwanini hawa wazamiaji wa ndani nje walishindwa kuitoa miili yote ndani Mv Bukoba?
3. Manahodha hawakuwa na ujuzi. Tuchukulie anasema ujuzi wa kazi yao. Shahidi wa kwanza wa upande wa serikali katika kesi hiyo, aliimbia mahakama kuu kuwa, Nahodha Jumanne Rume Mwiru amemfahamu kwa zaidi ya miaka 10 akifanya kazi ya unahodha kwa muda wote huo.
4. Taasisi ya maji ya Denmark ilikagua meli hiyo. Pengine amenukuliwa vibaya. Lakini maelezo rasmi yaliyotolewa mahakamani ni "wataalamu" kutoka Denmark. Hawa wataalamu wa maji ndio waliokagua meli ndio nimewasikia kwa Prof. Kulingana na taarifa za mahakama ambazo kila mmoja anaweza kuzi ona kupitia. Www.tanzlii.org, ukaguzi wa mwisho ulifanywa na kampuni ya Ubelgiji mwezi may 1996 kabla ya ajali na haikutoa taarifa yake.
5. Meli iilikuwa ikiserereka majini. Hii naomba niache hivyo.
6. Meli ilijengwa na watu 63. Hapa sijui alitaka kusema nini. Idadi ya watu inahusikaje? Walikuwa wengi au wachache? Hawakuwa na sifa. Ujenzi wa meli unahusisha watu wangapi na wenye taaluma zipi?
7. Hakuna hatua zilizochukuliwa licha ya meli kubainika kuwa na kasoro. Hapa Prof anajikanganya. Awali anasema kuna wataalamu wa maji waliikagua lakini anabadilika na kusema hakuna hatua zilizochukuliwa.
Samahani kwa kuwachosha na pia nimwombe radhi Prof kuwa haya ndio sisi wa darasa la saba b, tunayafahamu hayo mengine ya kisomi endeleeni ninyi.
Mkandala,amejikita kupitia hoja zilizoibuliwa na jaji kisanga,hilomosi
Pili, tume,inaonesha tanzania hakuna tenda imewahi tangazwa kununua hiyomeli ila Belgium tenda ilitangzwa
Tatu ,inakuwaje meli iserereke majini
Mwisho ,hoja ni mabadiliko yakatiba na kupunguza maagizo yamtu mmoja kuathiri watanzania