Prof. Mussa Assad: Nilipokuwa ofisini niliomba nyaraka za SGR, Air Tanzania na mradi wa Stiegler's Gorge lakini sikupewa hata moja

Prof. Mussa Assad: Nilipokuwa ofisini niliomba nyaraka za SGR, Air Tanzania na mradi wa Stiegler's Gorge lakini sikupewa hata moja

Anaongea baada hayati hayupo? Ni unafiki siku zote alikuwa wapi? Au hayati awezi kujitetea huko alipo basi nae kahamu kutafuta kick?
Na siku zote nani alienda kumuuliza na leo kajipeleka kwenye vyombo vya habari ama vimemfuata!?
 
Kawaida ukishastaafu au kuondoka kwenye nafasi yako usipende kuongelea mambo ya ofisi uliyokuwa.

Ulishamalizana nao basi sababu wakikubana ukasema una ushahidi ukienda ofisini kuomba hata barua labda hawakupi. Si sahihi sana ukishatoka kuongelea mambo ya ofisi ulikokuwa achana nayo endelea na maisha mengine.
Asiendelee kufuchua....maana anatutia aibu
 
Mbona alikuwa kmy muda wote, kumbe naye mnafiki kama wengine

Huyu jamaa (CAG) mstaafu kabisa siyo mzalendo, angalikuwa mzalendo angalikuwa na msimamo na hata ni kutupwa gerezani kwa faida ya taifa kwahiyo viongozi kama hawa, wanafiki, hawafai na ni hatari kwa taifa, anagawa wa Tanzania kwa uonga wake. Angalikuwa kama Dr Tuntemeka Sanga aliyekuwa (banished) zuiliwa kijijini kwake enzi hizo kwa kutaka makuu kwa kujiona kasoma kuliko Mtanzania yeyote!! He should have spoken his mind according to his profession and patriotic mind. He let Tanzanians down by not speaking the truth loudly. Kwa sasa tunachukulia kuwa anatafuta kitu kwa faida yake binafsi! Hili ni wazo langu binafsi! I stand to be corrected.
 
Profesa Assad amefichua kuwa aliomba nyaraka za ununuzi wa ndege, reli ya SGR pamoja na Bandari ya Bagamoyo kwa kutumia technical reason lakini mkuu wa nchi wa wakati huo alikataa kuzitoa akawa anamtafutia sababu ya kumtoa ofisini.

Prof Assad amesisitiza kuna muda watu wanavunja katiba waziwazi lakini Taifa linashindwa kuwakosoa kutokana na hofu na uwoga.

Prof Assad amesisitiza kwa kukaa kwake ofsini alizihitaji sana hizo nyaraka ili azisome na atoe ushauri wa kibiashara kwani amefanya kazi hizo kwa miaka mingi kabla ya kuwa CAG kabla ya kuzikagua.

Prof Assad ametoa ushauri ni muda muafaka wa serikali kuweka nyaraka wazi kwa Raia wake ili wazichambue na kuboresha mapungufu kuliko Kuzificha Ikulu.

===

Wakati nipo ofisini, katika vitu ambavyo ni vitu vitatu: niliomba SGR, niliomba document ya Air Tanzania upya na niliomba project ya Stiegler's Gorge -- feasibility studies. Na sikupewa hata moja. Nilichopata ilikuwa ni barua kwamba mwaka haujamalizika na kwahiyo ukaguzi wa hesabu si wakati wake.

Na kila mtu mwenye akili alikuwa anajua nilichokuwa nataka kufanya si ukaguzi wa hesabu, lakini ilikuwa ni technical response ya kusogeza muda na kuniondoa katika reli tu. Kwahiyo, mpaka nimeondoka ofisini I never got that information na mpaka sasa hivi sijatafuta na sijasoma.

Wewe ni kama mimi. I'm a private citizen now. Ikitokea taarifa hii ipo wazi, tutaisoma na tutatoa commentary.
Please; we only want to hear about LEGACY 😛😛😛😛😛
 
Duuh!!, wewe ni kichwa, hujaacha hata moja!!! Umeweza kueleza kiufasaha na mifano dhahiri
Asante Ndugu. Lazima hizi kumbukumbu tuziweke vizuri ili vizazi na vizazi vije kujua huyu dhalimu alikuwa ni mtu wa namna gani?
 
Kuna meli moja bwan mkubwa mwenda zake alisimamia alinunua akiwa Waziri wa ujenzi na uchukuzi alipokuwa Rais ili meli ile isisemwe sana kuwa ni mbovu aliikabidhi kwa jeshi-JWTZ, akasema kwa sasa meli hii ni sawa sawa na vifaru vya jeshi atakayeiongelea shauri zake
Bora hiyo ripoti nayo ikabidhiwe Jeshi....maana kuna watu hawaitaki...
 
Kuna kitu hakiingii akilini. Unaposema aliomba maana yake ni nini? Huwa hatuombi nyaraka, huwa tunapewa nyaraja kufanya audit. Ukishaanza audit utakuwa uneshapewa kika unachohitaji, kimeandaliwa kabla hujaja. Wao pia ni wahasibu kama wewe, wanajua mahitaji. Isitoshe tayari una data za mwaka jana na mwaka juzi hii si audit mpya. Kama angesema aliomba nyaraja za SGR, zipi, akanyimwa ningeelewa, lakini alipisema aliomba za SGR NA za ndege NA za barabara nikajua si kweli, these are different audits. Na hasemi ni nyaraka gani, kwa sababu hata jina ni nyaraka, bajeti ni nyaraja, bank statement ni nyaraka, invoice ni nyaraka na risiti ni nyaraka unapewa moja kwa moja kutoka benki au kwa creditor hupitii kwa Magu. Na pale anaposema ana uzoefu na hayo mambo si kweli, ni wa chuo kikuu mtu wa library. Sitashangaa kama hata train hajapanda si mtu wa Bara.
Huu ni utetezi? Au maoni?
 
Alikuwepo Baba wa Taifa. Alilitumikia Taifa kwa muda mrefu kuliko Rais yeyote. Alikuwepo Mkapa, na wengineo kama mzee Kawawa, Aboud Jumbe, Abdul Wakili - wote wametangulia mbele za haki. Lakini hakuna ambaye baada ya kuondoka kwake, maneno yalikuwa hivi!!
Mkuu kuna kitu kimekukwaza? Hukutaka kisemwe....
 
Mbona alikuwa kmy muda wote, kumbe naye mnafiki kama wengine

kama kusema tu 1.5t haipo alitolewa kimagumash hili je si angepelekewa watu kama TL nyie hamwelewi ? Tukiwaambia majitu ya ccm majiz hamwamini ? angalia wanavyokamatana uchawi kudadeki
 
Ahaa si alisema Bunge ni dhaifu halina uwezo wa kusimamia serikali

na ndungai akabisha lakin ye mwenyewe katuonyesha kuwa bunge ni dhaifu alikuwa anajua mikataba ni mibovu lakini hawez kusema sababu anamwogopa magufuli huo pia ni udhaifu
 
Kuna meli moja bwan mkubwa mwenda zake alisimamia alinunua akiwa Waziri wa ujenzi na uchukuzi alipokuwa Rais ili meli ile isisemwe sana kuwa ni mbovu aliikabidhi kwa jeshi-JWTZ, akasema kwa sasa meli hii ni sawa sawa na vifaru vya jeshi atakayeiongelea shauri zake

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom