Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ila sio kwa msiba wa dhalimu.
Nasikia coro imefanya yake kama yule dhalimu wakoMzee huu nilikuwa namkubali sana kwa siasa zake za Kisomi. RIP mzee wangu
Poleni sana wanachadema na familia nzima, jamaa, na marafiki wa Prof. Baregu. Mungu aipumzishe roho ya marehemu pema peponi. Aminah.View attachment 1816939
Ni habari mbaya ambayo imetokea muda si mrefu.
Aliyekuwa Mhadhiri wa Vyuo Vikuu mbalimbali nchini, Prof. Mwesiga Baregu amefariki dunia mapema leo.
Prof. Baregu alikuwa pia Mjumbe wa Kamati kuu ya CHADEMA.
Pia Soma: Prof. Baregu alifukuzwa UDSM kwa sababu za kisiasa, huku Bashiru akiachwa kwakuwa ni CCM
View attachment 1817281
Dar es Salaam. Mwanachama wa Chadema na mwanazuoni, Profesa Mwesiga Baregu amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumapili Juni 13, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma Muhimbili, Aminiel Aligaesha amesema, “amefariki saa tano usiku wa kuamkia leo akiwa ICU (chumba cha uangalizi maalum) na alikuwa hapo kwa takribani siku 15.”
Akizungumza na Mwananchi Digital leo Mkurugenzi wa Itikadi na Uhusiano wa kimataifa wa Chadema, John Mrema amesema chama kitatoa taarifa rasmi taarifa baada ya kikao na wanafamilia.
"Tunaelekea hospitali ya Muhimbili kukutana na wanafamilia halafu tutatoa taarifa rasmi," amesema Mrema.
Katika ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Twitter Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo amesema, "pumzika kwa amani Profesa Baregu. Mmoja wa wasomi walioamini kuwa huwezi kutenganisha taaluma na siasa. Ulitufundisha baadhi yetu tunaokubali msimamo huo wasomi wanaweza kufanya siasa bila kupoteza sifa zao.’”
Mwingine aliyeandika ujumbe Twitter ni kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe akimtakia mapumziko mema Profesa Baregu.
Profesa Baregu aliyekuwa mhadhiri wa sayansi ya siasa na utawala wa umma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, baadaye alisitishiwa mkataba wake kwa kile kilichoelezwa kuchanganya utumishi na siasa.
Baadaye alihamia Chuo kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT). Alikuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chadema hadi mwaka 2019.
Dhalimu kwako
Nasikia coro imefanya yake kama yule dhalimu wako
Sijui wewe unaongea nini kwani hata mimi namlilia lakini siyo kwa sababu ya alikuwa na political impact yoyote kwangu.Impact yake katika siasa angalia humu wanavyomlilia kila thread. Hakuna atakayekamtwa kwa kushangilia kifo chake.
Sisi ni wa Mungu na kwake tutarejea.
Mungu amsamehe makosa na amlaze pema. Amin.
Asante tumesha poa.Ama kweli duniani tunapita tu!
Poleni wafiwa na wana-CHADEMA kwa ujumla.
Mungu anasamehe watu wanaotubu wakiwa wazima (kabla ya kifo). Mungu hatumii middlemen. Kwamba watu wengine watakuombea toba baada ya kufa na Mungu akakusamehe ni ubatili. Mend your ways before you die.
Wewe unadhani Mungu ni kama wewe usiweza kusamehe kwa kuombwa Msamaha kupitia watu wengine???!!.
Wapo watu wanaoweza kumuombea mtu Msamaha kwa Mungu na Mungu akawakubalia, sisemi kwamba ni lazima apokee maombi ya msamaha bali anayo hiyari ya kupokea au kutopokea tunachofanya sisi ni kumuombea tu kama binadamu mwenzetu kwani sisi sote kifo ni unavoidable isitoshe pia watu tujifunze kuombeana katika jambo la aina hii licha ya kwamba kujitahidi katika mema ndiyo the most Paramount thing.
Hiyo si kweli. Baregu alikuwa Stanford akiwa mwanafunzi.Kwa heri Mwamba
Huyu Gwiji ndie alikuwa Mmoja wa Supervisor wa PhD ya Dr Kondilize Rice (1982) baadae alikuja kuwa Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani
Porojo tu. Baregu alistaafu kwa mujibu wa sheria ya wakati huo ya miaka 55 mwaka 1998. Alikwenda Zimbabwe na kurudi UDSM kwa mkataba 2002-2009, kisha SAUTYule waziri aliyemfukuza kazi baregu pale UDSM , sijui atashangilia ama atalia.
Hajafa kwa corona. Ameugua miaka 2 na nusuNi msomi pekee aliekuwa pale chadema!
.
Corona hii ina mambo sana
Hapana. Usibahatishe. Baregu alikuwa na stroke mbaya miaka 2Yes, ni coro. Hata hivyo, lini utaanza kujadili bajeti?