Prof. Ndalichako ni kweli Serikali inazifaulisha makusudi shule za Serikali dhidi ya shule Binafsi?

Prof. Ndalichako ni kweli Serikali inazifaulisha makusudi shule za Serikali dhidi ya shule Binafsi?

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
44,629
Reaction score
83,056
Mh. Prof Ndalichako,

1. Kuna taarifa kuwa Serikali imekuwa kwa makusudi ikijitahidi kuziinua shule za Serikali/kata katika mitihani at the detrimwent of shule za binafsi hasa zinazofanya vizuri.

2. Kwa makusudi kabisa inasemekana shule za binafsi zinazofanya vizuri/zenye historia ya kufanya vizuri watahiniwa wanapunguziwa marks ili shule za serikali/Kata zionekane zinafanya vizuri.

3. Najua si rahisi kulikubali kuwa hilo linatendeka, lakini habari za ndani kabisa zinasema ni hivyo. Kumbuka kuwa wasahihishaji wanatoka kwenye jamii tunayokaa hivyo kunawez kukawa na kaukweli ka aina fulani.

4. Vijana kutoka shule binafsi wanalalamika kuwa haiwezekani wakafeli hivyo kama ilivyoonekana kwenye mitihani ya juzi kidato cha sita na wanachelea kuomba remarking/rufani maana hawana imani tena na usahihishaji.

5. Mh. Prof, unalisemeaje hili?

6. Naamini hili kama linafanyika lazima liwe na Baraka za wakubwa na LABDA wewe ukiwa mmoja wapo? (inawezekana pia hujui), lakini common sense inaniongoza kufikiri kuwa haliwezi kufanyika bila wewe kujua.

KWA NIA NJEMA NALILETA KWAKO
 
Binafsi niliwahi hisi huenda shule za Serikali zinabebwa sana miaka hii.

2020 mdogo wangu alihitimu kidato cha nne shule ya Serikali na alikuwa ni zero brain kabisa ila cha kushangaza eti kapata division two, ukweli niliumia sana na kujiuliza ni wapi kuna tatizo.
 
Nimeongea na msahihishaji mmoj akaniambia nilichokiandika hapo.
 
Kwani huwa hawana miiko ya kutokutoa siri kama kazi zingine?
Miiko ipo sana tena sana, mbona magenerali wanapindua serikali na wamekula viapo na miiko? Wasahihishaji ni watu ambao wana watoto kwenye shule hizo hizo, hawapendezwi na yanayotokea. Ukiwa ndugu yake wa damu atakwambia.... with great anonymity!
 
Serikali ya CCM Ina Mambo mengi ya ajabu. Kama wanaweza kubambikia watu kesi za ugaidi, kuiba kura etc wanashindwaje kutoa matokeo ya upendeleo?
exactly Bujibuji, la mitihani ni rahisi sana kulifanya. asante umetoa mfano mzuri sana. Ilianza wakati wa Jiwe kuziinua shule za kata! Kila kitu kilikuwa uongo uongo...
 
Basi awamu ya tano ilishapita sasa tupo awamu ya sita kwa hapo unapozungumzia je hilo ?
Kwani si kuna mambo mengi tu yamerithiwa kutoka awamu ya tano yakaletwa awamu ya sita kama vile kupora chaguzi(refer chaguzi ndogo zinazoendelea nchini),kubambikizia watu kesi,kugandamiza vyama vya upinzani,kuzuia uhuru wa kujieleza,kuteka,kutumia polisi kwa manufaa ya CCM na kadhalika?Sasa ni ajabu hili la mitihani kurithiwa?
 
Kwa hiyo lawama nazo ni sahihi kuzitumia kwenye awamu ya tano?
 
Back
Top Bottom