Prof. Ndalichako ni kweli Serikali inazifaulisha makusudi shule za Serikali dhidi ya shule Binafsi?

Prof. Ndalichako ni kweli Serikali inazifaulisha makusudi shule za Serikali dhidi ya shule Binafsi?

Tuliongea sana hili kipindi matokeo yanatoka
Sidhani kama inaishia kwenye kushusha shule binafsi, ni juhudi zile zile za kutengeneza wataalam vilaza..chain reaction yake ni mbleleni sio sasa.... hadi nashangaa shule ambazo hasina chochote zinafaulisha sayansi kuliko shule zenye maabara na reagent...

Kuna shule zipo top ten wanafunzi niliwah tembelea hata kiswahil hawajui vizur...

Ni swala la muda tu
Nilichokiandika kinatoka kwa ndugu zetu walioenda kusahihisha. Ni kweli kama ulivyoandika hapo sentensi ya mwisho
 
Hoja yako iko kihisia zaidi kuliko kiuhalisia! Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) ni moja ya Taasisi za Serikali ambazo zinafanya kazi zake kwa weredi mkubwa.

Siku moja nenda kawatembelee ili ujue namna wanavyofanya kazi zao! Naamini baada ya hapo utakuwa Balozi mzuri kama mimi. Zoezi la usahihishaji halifungamani kabisa na upendeleo! Na wanao enda huko ni mashahidi! Maana haki ya Mtahiniwa hulindwa kuanzia hatua ya awali, mpaka ile ya mwisho.

Kuhusu kufeli kwa Watahiniwa wa shule binafsi, kunaweza kuchangiwa na sababu nyingi! Mojawapo kubwa ni ile ya kudhibitiwa kwa vitendo vya udanganyifu kwa baadhi ya Watahiniwa na pia Wamiliki wa hizo shule.

Mfano mzuri ni kwenye suala la Practical kwa Watahiniwa wa masomo ya Sayansi! Siku hizi Baraza limewabana sana Walimu wasio waaminifu kwenye suala zima la Practical. Nenda kawaulize, watakupa majibu. Hakuna janja janja tena za kutoa majibu ya mtihani kama ilivyokuwa huko nyuma.
Tate Mkuu nilichokiandika nimeambiwa na mtu aliyetoka juzi kusahihisha na naamini hawezi kunidanganya maana ni ndugu wa damu. Alikuwa tayari kurudi kacha per diem kuliko kfanya hivyo alivyoambiwa. Na si huyo tu wako wengi.

Haya mambo ni mepesi sema kuya prove, sema nafasi ya kufany hivyo hipo. Ni matter ya kuchukua scripts za shule nzuri zilizofeli na zile za serikali zilizofaulu zikasahihishwa upya neutral ground. Ubishi utaishia hapo.
 
Mh. Prof Ndalichako,

1. Kuna taarifa kuwa Serikali imekuwa kwa makusudi ikijitahidi kuziinua shule za Serikali/kata katika mitihani at the detrimwent of shule za binafsi hasa zinazofanya vizuri.

2. Kwa makusudi kabisa inasemekana shule za binafsi zinazofanya vizuri/zenye historia ya kufanya vizuri watahiniwa wanapunguziwa marks ili shule za serikali/Kata zionekane zinafanya vizuri.

3. Najua si rahisi kulikubali kuwa hilo linatendeka, lakini habari za ndani kabisa zinasema ni hivyo. Kumbuka kuwa wasahihishaji wanatoka kwenye jamii tunayokaa hivyo kunawez kukawa na kaukweli ka aina fulani.

4. Vijana kutoka shule binafsi wanalalamika kuwa haiwezekani wakafeli hivyo kama ilivyoonekana kwenye mitihani ya juzi kidato cha sita na wanachelea kuomba remarking/rufani maana hawana imani tena na usahihishaji.

5. Mh. Prof, unalisemeaje hili?

6. Naamini hili kama linafanyika lazima liwe na Baraka za wakubwa na LABDA wewe ukiwa mmoja wapo? (inawezekana pia hujui), lakini common sense inaniongoza kufikiri kuwa haliwezi kufanyika bila wewe kujua.

KWA NIA NJEMA NALILETA KWAKO
Hii ina ukweli 90% haiwezekani itokee revolution ya miaka 5 tu game ichange hivi!
Swali: serikali imefanya nn cha ziada kuongeza ufaulu kwa shule za serikali kuliko ilivyokuwa awali?
 
Hii ina ukweli 90% haiwezekani itokee revolution ya miaka 5 tu game ichange hivi!
Swali: serikali imefanya nn cha ziada kuongeza ufaulu kwa shule za serikali kuliko ilivyokuwa awali?
Mushaijamukulu, mugulusi, haya niliyoandika ameniambia ndugu yangu aliyetoka kusahihisha
 
Historia inaonesha kuwa rufani zote huwa zinapigwa chini(matokeo hayabadiliki). Ikitokea ni kama 0.000001% so to say!
Ni kwasababu rufaa inakatwa kwa huyo huyo aliyesahihisha mwanzo si kwa Mamlaka nyingine na kiuhalisia hata kuiita ile kuwa ni rufaa nao ni usanii mwingine tena.
 
Duh!
Ila baraza waangalie CONTINUOS ASSESMENT
(CA) zinazowasilishwa,
Wakuu wengi wa shule hushirikian na walimu wanaondaa hizo CA kuhujumu,
alama za mitihani ya ndan,
Huwa zinaongezw na kumpa mwanafunzi alama 15%, za bure.
Ushahid upo,


Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Ni kwasababu rufaa inakatwa kwa huyo huyo aliyesahihisha mwanzo si kwa Mamlaka nyingine na kiuhalisia hata kuiita ile kuwa ni rufaa nao ni usanii mwingine tena.
uko sahihi..........
 
Ukweli halisi hata Waziri mwenyewe hajui Vigezo gani vinatumika kutangaza mkoa uliiongoza. Huwa ni Siasa tupu ndio maana utaona wanatangazia hata Zanzibar siku hizi.
 
Tate Mkuu nilichokiandika nimeambiwa na mtu aliyetoka juzi kusahihisha na naamini hawezi kunidanganya maana ni ndugu wa damu. Alikuwa tayari kurudi kacha per diem kuliko kfanya hivyo alivyoambiwa. Na si huyo tu wako wengi.

Haya mambo ni mepesi sema kuya prove, sema nafasi ya kufany hivyo hipo. Ni matter ya kuchukua scripts za shule nzuri zilizofeli na zile za serikali zilizofaulu zikasahihishwa upya neutral ground. Ubishi utaishia hapo.
Nitakubaliana na wewe kwenye upangaji wa matokeo! Hapo naweza kukubaliana na wewe huenda kuna siasa zinafanyika za kuzibeba baadhi ya shule za Serikali kushika nafasi za juu kwa kuchezesha mfumo wao wa kugredi! Maana kuna shule nyingine unakuta imeingiza wanafunzi 10 bora kitaifa zaidi ya watatu, au wanne! Lakini haimo kwenye shule zilizofanya vizuri zaidi. Hapa ndipo baadhi ya wadau hulalamikia.

Ila kwenye usahihishaji, nitapinga mpaka mwisho. Hakuna shule/Mtahiniwa anaye pendelewa na NECTA! Na kama kuna mtahiniwa anayehisi kuonewa, bado kuna nafasi ya kukata rufaa! Na mara nyingi Msahihishaji wa huo Mtihani wa Mkata rufaa, huwa ni walimu wengine tofauti na wale walio sahihisha awali!

Still NECTA wanashirikiana na wakaguzi wa ndani ya Taasisi yao na pia wa nje, kuhakikisha haaki inatendeka! Sasa huyo Mdogo wako alienda kusahihisha Mtihani gani huo mpaka akaja na hayo maelezo?

NECTA kwa sasa wanajitahidi kupambana na vitendo vya udanganyifu, hivyo isije ikawa wadau wanalalamika baada tu ya mianya ya kufaulu kwa wepesi zaidi kuzibwa.
 
Guys kwa ALEVEL SERIKALI WAKO VIZURI KWANI WANACHUKUA WALIOFAULU KUTIKA HIZO PRIVATE NA UNAKUTA WAZAZI WENGI WAMEGAHARAMIA OLEVEL PRIVATE HARAFU A LEVEL WANAWAACHIA KWENDA SERIKALI HARAFU WALE WALIOFAURU KIDOGO OLEVEL NDO WANAKWENDA ALEVEL ZA PRIVATE. MATOKEO NDO HAYO..FUATILIANE MUONE
Hoja yako ina logic sana kwani watoto wanaoenda advance wanatoka hata huko private na wanakuwa wale walioperform vizuri dv 1 au 2 na wakifika huko lazima wafaulu vizuri na tayari wanajielewa wanajua nini kimewapeleka huko shule tofauti na olevel kumshape mtoto mpaka aanze kuelewa masomo kwa lugha ya malkia ni music wengine unakutana nao hata kiswahili tu mgogoro .Walimu wanaofundisha olevel ni wa kuwashukukuru sana kwani wanafanya kazi nzito sana
 
Hii nchi ya watu walalamishi hii..huna ushahidi, hisia tu ushalalamika
 
Back
Top Bottom