mtanzania1989
JF-Expert Member
- May 20, 2010
- 4,068
- 6,758
Mayunga ni watu wa Mara, kanda ya Ziwa ni kubwa sana ina mikoa mingi na watu wengi sana too bad wote wanaitwa wasukuma, mikoa yote hii Mwanza, Simiyu, Geita, Shinyanga, Mara, Kagera hawa wote ni kanda ya ziwa, hapo bado Tabora ambayo si kanda ya ziwa ila watu wake wana uhusiano wa karibu sana wa kiutamaduni na kiuchumi na kanda ya ziwa.Mbona huyu jamaa jina kama la kwao na mwendazake? Mayunga??
Vp Pter??Alikuwa jirani mwema sana.
So sad kupoteza jirani kama huyo mzee.
Hongera mzee kwa kula chumvi nyingiVp Pter??
Last week Thurday 15/07/2021 nimesherehekea birthday yangu - nimegonga miaka 72. Hivi mi ni mzee kiasi hicho???!!!
Natania kidogo kuondoa frustration pamoja na ukweli ni babu.
unataka kuleta siasa za kipuuzi kwenye uzi wa tanzia.Mayunga ni watu wa Mara, kanda ya Ziwa ni kubwa sana ina mikoa mingi na watu wengi sana too bad wote wanaitwa wasukuma, mikoa yote hii Mwanza, Simiyu, Geita, Shinyanga, Mara, Kagera hawa wote ni kanda ya ziwa, hapo bado Tabora ambayo si kanda ya ziwa ila watu wake wana uhusiano wa karibu sana wa kiutamaduni na kiuchumi na kanda ya ziwa.
Matusi na kejele za wanasiasa hasa hasa CDM dhidi ya kanda ya Ziwa ni hatari kwa taifa na hatari hata kwa mustakabala wao, kwa mara ya kwanza kuna uwezekano wa kanda ya ziwa wakaungana na kupiga kura za maruhani ( hasira) dhidi ya hizi kejeli mnazofanya.
No. Hujanikwaza technically ... majadiliano ya mitandaoni nayafuatilia siku zote na naendelea kuwa uptodate ... naomba tuwe pamoja kwenye issues kama hizi za misiba.We baba duh kumbe uwa tunabishana na wazee hapa duh I'm sory kama nilishakukwaza kwa lolote
Nami nitajitahidi kuzizuia hisia zanguJF Huwa najitahidi sana nisimjibu mtu vibaya maana kwa ufahamu wangu mdogo tu Kuna watu wazito humu na wanatumia fake ID.
Sasa vijana wanaoporomosha matusi humu unaweza Kuta unamtukana Boss wako kabisa bila kujua.
Utaenda kumzika Classmate wako ?No. Hujanikwaza technically ... majadiliano ya mitandaoni nayafuatilia siku zote na naendelea kuwa uptodate ... naomba tuwe pamoja kwenye issues kama hizi za misiba.
Mbona unanitupa we Babati???Pole mkuu, mkuu na wewe kumbe umekula chumvi haswa? hongera sn
R.I.PMwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Prof. Mayunga Habibu Hemedi Nkunya amefariki dunia leo Julai 20, 2021 katika Hosp ya Taifa, Muhimbili.
Marehemu Prof. Nkunya alikuwa Profesa Emerita katika Idara ya Kemia, Ndaki ya Sayansi Asilia na Tumizi. Alianza kazi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama Mkufunzi Msaidizi mwaka 1976. Alipandishwa vyeo vya kitaaluma hadi kufikia ngazi yaya mwisho kitaaluma ya Profesa, cheo alichokuwa nacho hadi alipostaafu utumishi wa umma mwaka 2012. Baada ya kustaafu Prof. Nkunya aliendelea na utumishi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajira ya mkataba. Mwaka 2020 aliteuliwa kuwa Profesa Emerita kwa kuthamini na kutambua mchango wake mkubwa kitaaluma.
Prof. Nkunya alikuwa msomi na mwanataaluma mbobezi aliyetafiti, kuchapisha na kushauri katika maeneo ya kemia ya onaniki (organic chemistry) hususani katika kemia ya dawa asilia(chemistry of natural products).
Prof. Nkunya alitoa zaidi ya machapisho 100 katika majarida yanayoheshimika duniani na katika vitabu. Alishiriki katika kazi mbalimbali za ushauri ndani na nje ya nchi. Aidha alikuwa mwenyekiti/mjumbe katika kamati nyingi za kitaaluma na za ushauri.
Prof. Nkunya alishika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ikiwemo Afisa Taaluma Mkuu cheo (sawa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma sasa) (1999-2006) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(2007-2010); na Katibu Mtendaji wa Baraza la Vyuo Vikuu Afrika Mashariki(2011-2015).
Mpaka anafariki alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania wadhifa aliokuwa nao kuanzia mwaka 2019 na Mwenyekiti wa Baraza la Ujenzi la Taifa kuanzia mwaka 2016. Mipango ya mazishi ya Prof. Nkunya inafanywa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na familia.
Mwili wa marehemu unatarajia kusafirishwa siku ya Jumatano tarehe 21 Julai 2021 kuelekea Tabora kwa Mazishi.
Roho ya Marehemu Ipumzike kwa Amani!
Duh!!!
RIP my college mate UDSM July 1972 - March 1975.
Yes, he a real gentleman.
Bila shakaUtaenda kumzika Classmate wako ?
Duu hii kitu sio
Hahahaha kweli wewe hamnazo,kipindi kile Kayafa na chawa wake wakina Herri James, Bashite wakihubiri chuki,udini,ukabila na ukanda ulikuwa kiziwi au kipofu?Mayunga ni watu wa Mara, kanda ya Ziwa ni kubwa sana ina mikoa mingi na watu wengi sana too bad wote wanaitwa wasukuma, mikoa yote hii Mwanza, Simiyu, Geita, Shinyanga, Mara, Kagera hawa wote ni kanda ya ziwa, hapo bado Tabora ambayo si kanda ya ziwa ila watu wake wana uhusiano wa karibu sana wa kiutamaduni na kiuchumi na kanda ya ziwa.
Matusi na kejele za wanasiasa hasa hasa CDM dhidi ya kanda ya Ziwa ni hatari kwa taifa na hatari hata kwa mustakabala wao, kwa mara ya kwanza kuna uwezekano wa kanda ya ziwa wakaungana na kupiga kura za maruhani ( hasira) dhidi ya hizi kejeli mnazofanya.
So sad. On 20/12/2020 my classmate at Old Moshi sec 1970/71 form iv/vi passed away - Prof. Bakari Lembariti - MUHAS.
Leo college mate UDSM Prof. Mayunga Nkunya 1972 - 1975 tuliyekuwa naye hapo mlimani.
So sad. Najiandaa kuagana nanyi wana jf. Hii ndiyo reality.
Ndio uzuri wa JF, mtu akileta za kuleta hata kama ana kinga ya kutoshtakiwa, we mrapue tu!JF Huwa najitahidi sana nisimjibu mtu vibaya maana kwa ufahamu wangu mdogo tu Kuna watu wazito humu na wanatumia fake ID.
Sasa vijana wanaoporomosha matusi humu unaweza Kuta unamtukana Boss wako kabisa bila kujua.
Duh!!!.!Heshima yako, mkuu. Wakati unaingia chuo ndio mimi nazaliwa. Na sasa nimeezeka. Can you imagine that?
Duh!!!.!
Ya kweli haya Omusolopogasi???
Siku zote nakufuatilia kama mzee mwezangu...hasa kwa jina lako la ki SA🤣🤣
Enzi zetu za kuliberate kusini mwa Africa
Nadhani mmejifunza kitu leo. Kuna watu humu ni bab zenu lkn mnawatukanaYaani hizi fake ID zinatudanganya sana,kweli jitahidi kuwa positive unapomkosoa mtu tumia maneno ya staha bila kumvunjia heshima
RIP Prof...Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Prof. Mayunga Habibu Hemedi Nkunya amefariki dunia leo Julai 20, 2021 katika Hosp ya Taifa, Muhimbili.