TANZIA Prof. Nkunya wa TCU afariki dunia

Mbona huyu jamaa jina kama la kwao na mwendazake? Mayunga??
Mayunga ni watu wa Mara, kanda ya Ziwa ni kubwa sana ina mikoa mingi na watu wengi sana too bad wote wanaitwa wasukuma, mikoa yote hii Mwanza, Simiyu, Geita, Shinyanga, Mara, Kagera hawa wote ni kanda ya ziwa, hapo bado Tabora ambayo si kanda ya ziwa ila watu wake wana uhusiano wa karibu sana wa kiutamaduni na kiuchumi na kanda ya ziwa.

Matusi na kejele za wanasiasa hasa hasa CDM dhidi ya kanda ya Ziwa ni hatari kwa taifa na hatari hata kwa mustakabala wao, kwa mara ya kwanza kuna uwezekano wa kanda ya ziwa wakaungana na kupiga kura za maruhani ( hasira) dhidi ya hizi kejeli mnazofanya.
 
unataka kuleta siasa za kipuuzi kwenye uzi wa tanzia.

Kama unataka kuongelea siasa si uanzishe uzi wako ?

Shenzi.
 
JF Huwa najitahidi sana nisimjibu mtu vibaya maana kwa ufahamu wangu mdogo tu Kuna watu wazito humu na wanatumia fake ID.

Sasa vijana wanaoporomosha matusi humu unaweza Kuta unamtukana Boss wako kabisa bila kujua.
Nami nitajitahidi kuzizuia hisia zangu
 
No. Hujanikwaza technically ... majadiliano ya mitandaoni nayafuatilia siku zote na naendelea kuwa uptodate ... naomba tuwe pamoja kwenye issues kama hizi za misiba.
Utaenda kumzika Classmate wako ?
 
Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Prof. Mayunga Habibu Hemedi Nkunya amefariki dunia leo Julai 20, 2021 katika Hosp ya Taifa, Muhimbili.

Marehemu Prof. Nkunya alikuwa Profesa Emerita katika Idara ya Kemia, Ndaki ya Sayansi Asilia na Tumizi. Alianza kazi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama Mkufunzi Msaidizi mwaka 1976. Alipandishwa vyeo vya kitaaluma hadi kufikia ngazi yaya mwisho kitaaluma ya Profesa, cheo alichokuwa nacho hadi alipostaafu utumishi wa umma mwaka 2012. Baada ya kustaafu Prof. Nkunya aliendelea na utumishi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajira ya mkataba. Mwaka 2020 aliteuliwa kuwa Profesa Emerita kwa kuthamini na kutambua mchango wake mkubwa kitaaluma.

Prof. Nkunya alikuwa msomi na mwanataaluma mbobezi aliyetafiti, kuchapisha na kushauri katika maeneo ya kemia ya onaniki (organic chemistry) hususani katika kemia ya dawa asilia(chemistry of natural products).

Prof. Nkunya alitoa zaidi ya machapisho 100 katika majarida yanayoheshimika duniani na katika vitabu. Alishiriki katika kazi mbalimbali za ushauri ndani na nje ya nchi. Aidha alikuwa mwenyekiti/mjumbe katika kamati nyingi za kitaaluma na za ushauri.

Prof. Nkunya alishika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ikiwemo Afisa Taaluma Mkuu cheo (sawa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma sasa) (1999-2006) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(2007-2010); na Katibu Mtendaji wa Baraza la Vyuo Vikuu Afrika Mashariki(2011-2015).

Mpaka anafariki alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania wadhifa aliokuwa nao kuanzia mwaka 2019 na Mwenyekiti wa Baraza la Ujenzi la Taifa kuanzia mwaka 2016. Mipango ya mazishi ya Prof. Nkunya inafanywa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na familia.

Mwili wa marehemu unatarajia kusafirishwa siku ya Jumatano tarehe 21 Julai 2021 kuelekea Tabora kwa Mazishi.

Roho ya Marehemu Ipumzike kwa Amani!

R.I.P
 
Mayunga ni watu wa Mara, kanda ya Ziwa ni kubwa sana ina mikoa mingi na watu wengi sana too bad wote wanaitwa wasukuma, mikoa yote hii Mwanza, Simiyu, Geita, Shinyanga, Mara, Kagera hawa wote ni kanda ya ziwa, hapo bado Tabora ambayo si kanda ya ziwa ila watu wake wana uhusiano wa karibu sana wa kiutamaduni na kiuchumi na kanda ya ziwa.

Matusi na kejele za wanasiasa hasa hasa CDM dhidi ya kanda ya Ziwa ni hatari kwa taifa na hatari hata kwa mustakabala wao, kwa mara ya kwanza kuna uwezekano wa kanda ya ziwa wakaungana na kupiga kura za maruhani ( hasira) dhidi ya hizi kejeli mnazofanya.
Hahahaha kweli wewe hamnazo,kipindi kile Kayafa na chawa wake wakina Herri James, Bashite wakihubiri chuki,udini,ukabila na ukanda ulikuwa kiziwi au kipofu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lembariti alikuwa mwalimu wangu MUHAS. Usiage mkuu. Mungu ndiye anajua siku ya mtu. Mzee wetu Mwinyi yupo anaikimbilia 100 lakini wajukuu wake wanaondoka. Ni Mungu tu.
So sad. On 20/12/2020 my classmate at Old Moshi sec 1970/71 form iv/vi passed away - Prof. Bakari Lembariti - MUHAS.

Leo college mate UDSM Prof. Mayunga Nkunya 1972 - 1975 tuliyekuwa naye hapo mlimani.

So sad. Najiandaa kuagana nanyi wana jf. Hii ndiyo reality.
 
Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Prof. Mayunga Habibu Hemedi Nkunya amefariki dunia leo Julai 20, 2021 katika Hosp ya Taifa, Muhimbili.

Marehemu Prof. Nkunya alikuwa Profesa Emerita katika Idara ya Kemia, Ndaki ya Sayansi Asilia na Tumizi. Alianza kazi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama Mkufunzi Msaidizi mwaka 1976. Alipandishwa vyeo vya kitaaluma hadi kufikia ngazi yaya mwisho kitaaluma ya Profesa, cheo alichokuwa nacho hadi alipostaafu utumishi wa umma mwaka 2012. Baada ya kustaafu Prof. Nkunya aliendelea na utumishi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajira ya mkataba. Mwaka 2020 aliteuliwa kuwa Profesa Emerita kwa kuthamini na kutambua mchango wake mkubwa kitaaluma.

Prof. Nkunya alikuwa msomi na mwanataaluma mbobezi aliyetafiti, kuchapisha na kushauri katika maeneo ya kemia ya onaniki (organic chemistry) hususani katika kemia ya dawa asilia(chemistry of natural products).

Prof. Nkunya alitoa zaidi ya machapisho 100 katika majarida yanayoheshimika duniani na katika vitabu. Alishiriki katika kazi mbalimbali za ushauri ndani na nje ya nchi. Aidha alikuwa mwenyekiti/mjumbe katika kamati nyingi za kitaaluma na za ushauri.

Prof. Nkunya alishika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ikiwemo Afisa Taaluma Mkuu cheo (sawa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma sasa) (1999-2006) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(2007-2010); na Katibu Mtendaji wa Baraza la Vyuo Vikuu Afrika Mashariki(2011-2015).

Mpaka anafariki alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania wadhifa aliokuwa nao kuanzia mwaka 2019 na Mwenyekiti wa Baraza la Ujenzi la Taifa kuanzia mwaka 2016. Mipango ya mazishi ya Prof. Nkunya inafanywa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na familia.

Mwili wa marehemu unatarajia kusafirishwa siku ya Jumatano tarehe 21 Julai 2021 kuelekea Tabora kwa Mazishi.

Roho ya Marehemu Ipumzike kwa Amani!

RIP Prof...
 
Back
Top Bottom