Prof. Palamagamba Kabudi: Vikwazo vipate baraka ya Umoja wa Maraifa


Kwa hiyo hili la vikwazo linafahamika kwa watawala wetu? Waziri anazungumza kwa unyonge na kulalamikia mabeberu. Bullies do not want to be bullied!
 

Kama waziri unatakiwa kutatua matatizo sio kutoa maoni ambayo hayatafanyiwa kazi. Jitahidi kututoa kwenye list hizi na tuongeze watalii achana na kushinda kuongea na watu ambao hawasaidii kitu na kupiga makofi kinafiki
 
Hawa Jamaa walidai kuwa tunapigana VITA VYA KIUCHUMI na MABEBERU ..... Mbona wanaanza kulia mapema!!
 
Ama ni wakati muafaka wa kujitafakari na kujisahihisha kwa makosa yote ambayo ccm mmeyafanya. Siyataji kwani yanajulikana! Serikali ilishapokea maonyo matatu kutoka UE na USA lakini hayakufanyiwa kazi na kusahihisha makosa yaliyotajwa mle! Kama kweli wizara na serikali inaongozwa na watu wasomi waliopitiliza basi wangetumia busara kukaa na waliowatuhumu ili kuyajua makusudi yao badala ya kujimwambafai huku ikihitaji misaada na mikopo yao! Wafunge Safari ya kwenda EU na USA kusaka suluhu kwani kibano Chao siyo Cha kitoto, unless serikali iseme kuwa ni ajenda yake ya Siri ya kuwaumiza wananchi wake kwani wao ndio watakaozuiliwa kusafiri nchi hizo! Waziri mhusika jiuzulu tu kwa hili.
 
Marekani ndio top baba.. Usijidanganye Kuna mwingine juu. Akiamua kupiga Bomu popote anapiga, akiamua kuweka vikwazo Hakuna wa kutengua....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Kabudi apambane kuhakikisha hatuwekewi vikwazo kama wanavyotishia USA. Hayo ya Wazimbabwe awaachie wenyewe
 
Afrika mtapewaje kura ya veto wakati hata chakula chenu wenyewe hamjitoshelezi! Na mkifanya fyoko kuwa mnajitoa UN, vikwazo mtakavyowekewa hata Marais wenu watatembelea baiskeli.

Ili nchi iwe na kura ya veto lazima iwe na nguvu za kiuchumi na kijeshi.
 
He was supposed to be in Mwl. Nyerere 'a cabinet...
 
Jinga huyo ndo katufikisha hapa kwa kumshauri Jiwe Ujinga, asubiri Travel ban yake..

Na aamue sasa atabeba mzigo wa Zimbabwe ama Chato
 
Ni jambo la kusikitisha sana waziri anapoamua kuonyesha alivyo mjinga (Ignorant) wa maswala ya kidiplomasia.

Wakati nchi zile tano za kiafrika, Tanzania ikiwemo, zilizokuwa mstari wa mbele kwenye kupinga ukoloni na ubaguzi wa rangi kusini mwa Afrika wao uamuzi wao huo uliridhiwa na Baraza gani la umoja wa mataifa na kwa azimio namba ngapi.

Kabudi hajui kuwa kuna vikwazo ambavyo nchi moja inaweza kabisa ikaiwekea nchi nyingine pasipo kuhitaji idhini ya UN security council.

Nakumbuka kuna kipindi wakati wa Mkapa Tanzania ilitishia kuiwekea vikwazo Burundi pale nchi hiyo iliposusa usuluishi wa Mwl. Nyerere, sijui yeye Kabudi alikuwa wapi wakati huo, au alikuwa bado na akili ndogo.

Lkn sasa maoni ya Kabudi hayana msingi make sasa ni Tanzania ndio inajiandaa kuanza kupambana na hivyo "Vikwazo" kama Marekani ilivyodokeza ambayo kwa wote wapigania haki ni hatua chanya sana.
 

Hakuna Marekani kusikiliza hiki chama cha wahuni, tena waongeze vikwazo zaidi. Hivi vyama vikongwe vinaleta tabia ya kutawala kimabavu bila ridhaa ya umma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…