Uchaguzi 2020 Prof. Rwekaza Sympho Mukandala: Hatma ya CCM 2020 bado haijulikani

August 9 2020
Zanzibar, Tanzania

Zitto - Mapokezi ya Maalim Seif, Membe huko Zanzibar, Ni ujumbe tosha kwa watawala wa CCM

WaZanzibari watuma salamu kuelekea October 28 2020 kuwa haki ya waZanzibari haipotei. Hivyo wanaenda tena kumchagua kiongozi wao Maalim Seif.
 
August 10 2020
Ikungi, Singida
Tanzania

WAZEE WA IKUNGI SINGIDA, WAONGEA MAZITO WAKATI WA KUMPOKEA TUNDU LISSU
Wazee wazungumzia walivyoporomosha maombi ili Mungu amponye Tundu Lissu akwepe mauti na pia apone majeraha yake ili arudie hali yake ya uzima wa afya na mwili.
Wazee wakaendelea kusema bado mioyoni mwao Tundu Lissu ni mbunge na huyo mbunge aliyepitishwa katika uchaguzi mdogo ni 'mbunge wa viti maalum'

Wazee tayari wamempa Tundu Lissu baraka za kuelekea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Source : CHADEMA MEDIA TV
 
11 August 2020
Kahama, Shinyanga
Tanzania

TUNDU LISSU, APEWA BARAKA ZA KUGOMBEA URAIS


Mgombea Urais Kupitia CHADEMA,Tundu Lissu amekutana na kuzungumza na Wanachama katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga.
 
Hali ya kisiasa ilivyokuwa mwezi Juni 2020 wakati wananchi wakimpokea mbunge wao akitokea Dodoma bungeni baada ya Bunge kuvunjwa

27 Juni 2020
Tunduma, Tanzania

Mapokezi ya Frank George Mwakajoka


Source : DSS Tunduma
 
13 August 2020
Musoma, Tanzania

TUNDU LISSU APOKEWA NA UMATI WA WATU


Tundu Lissu ameendelea kutembelea maeneo mbalimbali nchini Tanzania kusalimia na kusaka wadhamini kama sheria ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania inavyotamka mgombea adhaminiwe na waTanzanoa wa sehemu zote mbili za Tanzania yaani Tanganyika na Zanzibar.

Leo hii Tundu Lissu aliingia kwa kishindo mkoani Mara, kaskazini mwa Tanzania kutimiza takwa hilo la kisheria na kulakiwa na mamia ya waTanzania.
Source: CHADEMA MEDIA TV
 
17 Agosti 2020
Mikumi, Morogoro
Tanzania

MHE TUNDU LISSU AINGIA JIMBO LA MIKUMI NA KUPOKELEWA NA UMATI MKUBWA WA WANANCHI

Tundu Lissu akumbusha juu ya nasaha za kauli mbiu ya Mwalimu Nyerere iliyosisitiza utu ni UHURU katika kila kitu yaani Uhuru na Kazi pia Uhuru na Maendeleo na Uhuru na Umoja

Tundu Lissu anauliza kwanini Nyerere hakutanguliza Ma-barabara na Maendeleo au Miundo-mbinu na Maendeleo alijua kwanza utu wa mtu kupitia Uhuru kwanza ndiyo kitu muhimu ili kupata Maendeleo ya Kweli.

Tundu Lissu anasema binadamu siyo mifugo ukaamua kuondoa utu wao wa kuwa HURU kwa kisingizio kuwa kwa kuwanyima uhuru wa utu wao, kuwanyanyasa , kuwabeza ndiyo unataka kuwaletea Maendeleo.
source: CHADEMA MEDIA TV
 
17 Agosti 2020
Morogoro Mjini
Tanzania


Source: CHADEMA MEDIA TV
 
17 Agosti 2020
TUNAJENGA VITU KWA MAENDELEO YA WATU, WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA.


Waziri Mkuu aongea katika mkutano wa viongozi wa dini wa kupongeza juhudi

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amejibu hoja ya baadhi ya wanasiasa wanaobeza Maendeleo ya Vitu Tanzania katika ujenzi wa miundombinu na ununuzi wa ndege akieleza kuwa serikali hiyo inajenga vitu kwa Maendeleo ya Watu.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awaonya viongozi kumsema Magufuli tu na kubeza, kutengeneza matukio ili kuonewa huruma. Serikali imesema kampeni na uchaguzi utaenda kwa amani na utulivu ili kuimarisha umoja.

Waziri mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa asisitiza watanzania wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura baada ya kusikiliza sera za nani amesema nini katika ahadi zao za kuwaletea maendeleo.
 
16 August 2020
Mwanza, Tanzania

Katibu Mkuu John John Mnyika akizungumza katika Mkutano wa BAVICHA


Katibu Mkuu CHADEMA John Mnyika leo amekutana na Baraza la Vijana BAVICHA wakati wa uzinduzi wa sera mbadala ya vijana wa Tanzania bara na Zanzibar, uzinduzi umefanyikia Mwanza.
Source: Millard Ayo
 
Political scientist Dr. Aikande Kwayu, kuna uoga wa kuchambua siasa na maendeleo hapa Tanzania hivyo kuna ombwe kubwa la taarifa


Dr. Aikande Kwayu, mtanzania ambaye ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa hasa katika maeneo mawili ya Sayansi ya Siasa na pia Mahusiano ya Kimataifa (Political Science na International Relations) , Dr. Aikande anasema Siasa inagusa maeneo mengi mfano Siasa katika Makampuni, Siasa za Kimataifa, Siasa ktk Jamii, Siasa ktkn Mgawanyo wa Rasilimali, Siasa za Chama (party politics) n.k hivi karibuni aliyeonekana akihojiwa na chombo cha habari kimataifa cha Al Jazeera.

Hapa nyumbani Tanzania kuna ombwe la uchambuzi hakuna uchambuzi au kusema vitu kuhusu vinavyotokea ndani ya nchi yetu, hivyo historia na mambo yaliyotokea Tanzania yanaandikwa na watu wa nje au kusimuliwa kwa undani na waandishi wa habari kutokea Nairobi, Johannesburg au ktk BBC , VoA, Aljazeera, DW n.k

Jamii ya Tanzania ina haiba tofauti kwa kulazimisha watu wafiche kusema wanachofikiri hasahasa katika kutoa mitazamo yao, inaonesha hakuna walio tayari kutoa mawazo yao kwa kuheshimu tofauti za mitizamo yao na mwisho kukubaliana kutofautiana baada ya kushindanisha hoja. Ukisoma maoni / comments za waTanzania ndani na nje ya nchi kunaonekana mbinyo wa jamii kulazimishwa kukubaliana kwa lazima lakini siyo kwa hoja anamalizia maoni yake Dr. Kwayu.
Source : Global TV online
 
JAMAA AJITOSA KUMDAI HELA MAGUFULI "ACHIA FEDHA, MAISHA MAGUMU"

27 Nov 2019
Baada ya msafara wa rais Magufuli kusimama Igunga mkoani Tabora alipokuwa akizungumza na wananchi, mmoja amejitokeza na kumtaka rais Magufuli aachie pesa kwasababu maisha magumu... lakini pia rais magufuli amejibu hi
Source : MwanaHALISI TV
 
Magufuli, a bogus prophet who predicted the demise of the opposition parties towards the year 2020 but that has miserably failed to pass...!!!

Now, it's the time for the people to ignore him in the ballot box by choosing his main rival to take over as, throughout his five year tenure, he has been busy tormenting and persecuting his critics at the expense of implementing his party's development programme.
 
CCM muda wao wa kupumzika ushafika, hata ambao huwa hatupigagi kura mwaka huu saa 11 alfajiri kwa foleni..

CCM kwisha habari yao!! Wakikataa kukabidhi nchi inaingia katika ntiani nkubwa!!
 
Washington D.C
Tundu Lissu alivyoacha simulizi mjini Morogoro, watoa ushuhuda

Ujio wa Tundu Lissu ulikuwa na shamrashamra na wananchi wa mkoa na mji wa Morogoro hawajawahi kuwa na furaha na matumaini makubwa kama kuona Tundu Lissu akija kufufua matumaini yao.

Mji wa Morogoro ulikuwa na viwanda vingi vikubwa vilivyotoa ajira rasmi mfano kiwanda kikubwa cha Tumbaku kimekufa na ajira 6,000 rasmi yaani wafanyakazi kupoteza ajira mwaka jana mwishoni.

Viwanda vingine vikubwa vya ngozi, canvas, ceramics, kusindika matunda kwa kutaja kwa uchache vyote vimekufa.
Source: Swahili Villa
 
18 JULAI 2020
Viwanja vya MwembeTogwa
Iringa, Tanzania

AITAKA SERIKALI KUACHA VITISHO UCHAGUZI HUU WA 2020

Tundu Lissu awapa nasaha serikali na wasimamizi wa uchaguzi kuwa hali imebadilika, dunia nzima inaitazama Tanzania hivyo hakuna nafasi watu wasiojulikana wasijulikane.
Source : CHADEMA MEDIA TV
 
Kudo's and big up!
Natumaini Jiwe ataperuzi kwene Ukrasa huu na atatafakari kwa kina....!!!!🤣🤣
 
19 August 2020
Mbeya, Tanzania

WaTanzania wapo tayari kufanya maajabu


Source : CHADEMA MEDIA TV
 
19 Agosti 2020
Moshi, Tanzania

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AMTAKA DC SABAYA KUMPA TAARIFA MSAFARA WA LISSU KUSHAMBULIWA


Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, ametoa kauli rasmi ya serikali kuhusiana na vurugu zilizotokea katika mji wa Bomang'ombe wilaya ya Hai wakati mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Tundu Lissu alipofika wilayani humo kutafuta wadhamini.

Katika taarifa hiyo rasmi aliyoitoa leo Agosti 19, 2020, mkuu huyo wa mkoa ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo, amemtaka mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, kumpatia taarifa ya maandishi ya namna alivyoshughulikia suala hilo.
Source : Mwananchi digital
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…