Uchaguzi 2020 Prof. Rwekaza Sympho Mukandala: Hatma ya CCM 2020 bado haijulikani

Uchaguzi 2020 Prof. Rwekaza Sympho Mukandala: Hatma ya CCM 2020 bado haijulikani

Mkandala namfahamu vizuri alinifundisha siasa Mlimani miaka mitatu nikawa nashangaa Professa anakuja lecture na tshirt na shingoni kavaa cheni na alikuwa anapenda sana sifa na kujidai!! nami leo napingana nae bila uoga!

1. Magu ni mtani wake na jirani yake kikabila hawezi mkubali hata mumuue!! yeye huona wahaya ni wasomi kuliko kabila lolote nchini na wanajua kila kitu zaidi kuliko mtu yoyote

2.Dhana yake Mkandala ni ile ile ya kati ya kuku na yai nini kilianza?? yaani anajifanya hajui kwa nchi maskini zenye income kiduchu Rais hubaki njiapanda kuchagua watu wawe na hela ila kusiwe na miundombinu au kinyume chake sababu lazima uchague kimoja pesa haitoshi kufanya yote mawili , je tujiulize kipi huendeleza kingine? welfare or infrastructure? ukiendeleza watu hakuna SGR wala Stiegler wanabaki maskini na maisha ya tabu na mahangaiko milele, ukijenga reli barabara vituo vya umeme vivuko kununua meli na ndege unatumia kodi yote na kuondoa mzunguko wa pesa mitaani watu wanakufa njaa je kipi cha kufanya?

3. Mukandala anakazia hoja ya Nape alipoongea bungeni huku akifurahiwa na Mr February pembeni kuwa Ilani ya uchaguzi ya kijani haisemi Rais apambane na miundombinu pekee bali inataka pia hali za maisha ya raia ziboreshwe na kuwa wanavyomaanisha miaka yote mitano Rais amefeli kwa kutofuata ilani ya chama! yaani amepuuza kuhudumia watu!!Mh Nape alisema wanamsubiri Rais kwenye kikao chama kumhoji kila kipengele cha ilani yao alikitekelezaje!!!

my take!
Mkandala ni debe tupu, litavuma siku zote hadi siku akipewa uteuzi! namsihi amuache Rais ajenge nchi sisi raia ni sugu tushazoea shida amuache Rais afanye yake tuumie sasa ili baadae tuishi kwa raha na wajukuu zetu wafurahie nchi yao!

Rais yuko sahihi hakuna muda sahihi wala shuruti katika ilani ya chama ya kujenga miundombinu na watangulizi wake hawakutoa kipaumbele sana katika miundombinu ambayo inapokamilika huleta neema na kurudisha furaha ya watu!!

Watu maskini wamezoea shida anawapigania ila wala hawako nae na hawajui maana ya furaha ni nini na wala hawajali Rais anawatesa na maisha magumu , furaha anaijua yeye na usomi wake!

Samahani sana my teacher Mkandala we are now equal , we now think differently na huwezi kunitishia kunipiga sup wala kunidisco tuko level moja kwenye elimu mitaani dot com!!
 
Hehehehehehehhehehehe loooo

Mkandala anawauliza Watanzania...
are you happy?/mna furaha??

Mi sina furaha (lakini sio kwa sababu ya ishu za siasa)-ni mengine tu
 
13 Julai 2020
Dodoma, Tanzania

Polepole : Mabango au Vipeperushi viwe vya ktk nguzo au mtandaoni haviruhusiwi na CCM Mpya...
Hua napata changamoto sana kuwasikiliza hawa watu naona bora Mbs zangu niangalie XXL
 
LAZARO NYALANDU ARUDISHA FOMU YA KUTIA NIA URAIS 2020 KUPITIA CHADEMA
Azungumza hali aliyoiona kutafuta udhamini kote Tanzania na uhai wa chama
 
19 Julai 2020
WAKILI SIMBA ARUDISHA FOMU YA KUTIA NIA KUGOMBEA URAIS WA JMT
Aongelea umuhimu kubalance Maendeleo ya Vitu dhidi Maendeleo ya Watu kwani CCM Mpya imewasahau watu, demokrasia na mashirikiano kimataifa
 
20 Julai 2020

7 warudisha fomu za kutia nia Urais CHADEMA



Watia nia kugombea urais sasa wamebaki 7 kati ya 11 waliochukua fomu. Ni baada ya 4 kutorudisha fomu ofisi ya Makao Makuu CHADEMA na miongoni mwa ambao hawajarudisha fomu ni Mh. Freeman Mbowe na Mch. Peter Msigwa.

Mkutano mkuu wa CHADEMA utafanyika tarehe 29 Julai 2020 kupitia na kuchagua miongoni mwa watia nia 7 wanaowania kubeberusha bendera ya CHADEMA ngazi ya Urais hapo Oktoba 2020.
Hapo kwenye "kubeberusha" hapo wasije wakabeberusha kweli....!
 
19 Julai 2020
MHE ISAYA MWITA CHARLES AKIRUDISHA FOMU YA KUTIA NIA KUGOMBEA URAIS KATIKA OFISI ZA MAKAO MAKUU
Meya Isaya Mwita aliyemaliza muda wake azungumzia alichokiona ktk kuzunguka nchini kote na ameona uimara wa CHADEMA mikoa yote ktk Zanzibar na Tanganyika
 
MTIA NIA NAFASI YA KUGOMBEA URAIS WAKILI GASPAR NICODEMUS MWANALYELA AKIRUDISHA FOMU
CHADEMA ni msingi nimeiona kwa uhalisia, nimeulizwa maswali mengi na wananchi. WaTanzania tunahitaji furaha na watu waofikiri sawasawa kwa kufahamu haki za kiuraia. Furaha ndiyo msingi wa mafanikio na kuondoa hofu ...
 
19 Julai 2020

MHE LEONARD MANYAMA MTIA NIA NAFASI YA URAIS AKIRUDISHA FOMU MAKAO MAKUU YA CHAMA
Kuzunguka nchi nzima nimeona kero na changamoto zinazowakabili wananchi kwa upana na undani. CHADEMA ni imara kipo mpaka vijijini
 
19 Julai 2020
DKT MAYROSE MAJINGE ARUDISHA FOMU YA KUTIA NIA KUGOMBEA URAIS WA JMT
Mayrose nimeona waTanzania wapo tayari kuingia Ikulu kupitia CHADEMA nimeona ..
 
20 Julai 2020

7 warudisha fomu za kutia nia Urais CHADEMA



Watia nia kugombea urais sasa wamebaki 7 kati ya 11 waliochukua fomu. Ni baada ya 4 kutorudisha fomu ofisi ya Makao Makuu CHADEMA na miongoni mwa ambao hawajarudisha fomu ni Mh. Freeman Mbowe na Mch. Peter Msigwa.

Mkutano mkuu wa CHADEMA utafanyika tarehe 29 Julai 2020 kupitia na kuchagua miongoni mwa watia nia 7 wanaowania kupeperusha bendera ya CHADEMA ngazi ya Urais hapo Oktoba 2020.
 
Unguja, Zanzibar

Takwa la kisheria limetimizwa na watia nia wote kupitia CHADEMA

 
Uchaguzi huru ndani ya chama

Breaking News !


Dr. Faustine Engelbert Ndugulile ashinda kura za maoni za ndani ya chama cha CCM jimbo la Kigamboni jijini Dar es Sakaam.

Kura za maoni za wajumbe halali zilikuwa 399 hakuna kura iliyoharibika na Dr. Faustine Engelbert Ndugulile amefanikiwa kupata kura 190 za wajumbe hao wa mkutano wa wilaya ya Kigamboni..

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kutumbuliwa kwa kilichoitwa 'tamaa' isiyokubalika ndani ya CCM Mpya Bw. Paul Christian Makonda amepata kura 122.
 
Back
Top Bottom