Prof. Safari: Kwenye usafiri wa umma, wazungu husoma vitabu na magazeti, watanzania wanatafuna mahindi ya kuchoma na mayai ya kuchemsha

Ha ha ha Wabongo kwa kujitetea.
 
sababu ya uwepo wa uislamu tanzagiza ndiyo maana labda hali iko hivyo, wazungu ni Christian au wana chimbuko la ukristo atleast …
Iran na Turkiye na Malaysia na Indonesia ni nchi za kiislam ila zina wasomi wakubwa duniani.
Point yako ya kipumbavu,usiingize udini haufai.
 
Issue si kununua, kusoma.

Unafanya nini ukiwa kwenye usafiri wa umma?

Kwa kuwa issue ni kusoma, unaweza kutembea na kitabu hard copy au soft copy ili kila upatapo nafasi usome badala ya kupiga soga.
Hukuwa na ulazima wa kunijibu kwa sababu hujanielewa
 
Hizo basi za Umma zenye convenience ya kusoma au hata mtu kupata fikra za kusomea kwenye hilo basi zinatoka wapi..., kabla haujafungua kurasa unaambiwa sogea tukae....

Kama ni suala la safari ndefu kitabu ni lazima...., mara nyingine mtu hauchukui kitabu ili usome bali jirani yako asikupigishe story zisizo na mwisho hivyo unajifanya busy kwenye usomaji... Pia usisahau hata chakula ni utalii sasa kama upo kwenye basi masaa ya kutosha alafu unafika Dodoma kwenye Zabibu utakuwa haulitendei haki tumbo lako kupata kitu from the Source..., Au kwa waliopanda treni Kuku wa Salanda....
 
Point ya profesor ni kuwa hatuna utamaduni wa kusoma
Hivi mabasi yanavyojazana na kulundikana watu kama nyanya kwenye tenga wakijambiana
Watasoma vitabu kweli

Ova
 
Kichwa cha habari kizuri ila tu umeharibu ulipo anza kukichambua, sasa mambo ya meya yanatoka wapi ktk headline yako. Acha ufisiemu kwanza ndio urudi kukielezea alichosema professor.
 
Mzungu anaustaarabu mzuri sana, mkiwa mnasubiria usafiri wa umma mnapanga foleni na anaingia mmojammoja haijalishi babu kijana au mtoto, ukikuta mtoto amekaa hata kama umemzidi umri subiri gari lingine.. hapo kariakoo kama unakuja tegeta siku moja bado kidogo nikanyagwe skio na mtu aliyeingilia dirishani kwenye usafiri huo wa umma..
 
Huo usafiri haukuruhusu hata kusoma kwa mbanano huo
 
Profesa Safari anajua hiace za Moshi mjini - Machame? Pale mbele wanapotakiwa kukaa abiria na dereva huwa wanakaa abiria watatu na dereva. Hilo gazeti unasomaje? Au coaster za Arusha - Moshi ambapo lazima majibizano kati ya abiria na kondakfa kuhusu nauli yatokee huku dereva naye akiingilia kati. Utakuta hapo ndo mko kwenye kona kali daraja la mto Kikavu ila dereva anatazama nyuma kupambana na abiria kuhusu nauli.
 
.......Wajapani wanalala
 
Prof siku atest apande na mavitabu yake ataona mziki
Mule ndani 😄

Ova
 
sababu ya uwepo wa uislamu tanzagiza ndiyo maana labda hali iko hivyo, wazungu ni Christian au wana chimbuko la ukristo atleast …
Wasukuma wa Mwanhuzi Maswa na Wabarabaig nao ni Waislam?
 
Iran na Turkiye na Malaysia na Indonesia ni nchi za kiislam ila zina wasomi wakubwa duniani.
Point yako ya kipumbavu,usiingize udini haufai.

mbona hakuzitolea mfano hizo nchi za kiislamu huyo profesa? isitoshe kwani udini una shida gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…