Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Prof. Shemdoe ametoa shukrani hizo kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akitoa neno la utangulizi, wakati ya hafla ya ufunguzi wa Soko Kuu Jipya la Kariakoo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Februari 9, 2026.
Prof. Shemdoe ameongeza kuwa, Soko la Kariakoo ni kitovu cha biashara ndani ya Jiji la Dar es Salaam na Taifa kwa ujumla, hivyo ofisi yake kwa kutambua hilo itahakikisha soko hilo linatoa huduma bora na kwa ufanisi ili kuleta tija na kuakisi thamani ya fedha iliyowekezwa na Serikali.
Sanjali na hilo, Prof. Shemdoe amesema kuwa, Serikali inaendelea na utaratibu wa kuhakikisha barabara zote zinazozunguka Soko la Karikakoo na maeneo jirani zinafunguliwa ili ziweze kupitika wakati wote na kulifanya soko litoe huduma kwa wananchi masaa 24.
Aidha, Prof. Shemdoe ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteu kuwa Waziri anayesimamia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na kumuahidi Mhe. Rais kwamba atafanya kazi kwa bidii na uadilifu mkubwa.