Prof. Shukrani Manya aapa kuwa Mbunge. Spika Ndugai awataka wabunge wa ACT-Wazalendo nao wakaape

Prof. Shukrani Manya aapa kuwa Mbunge. Spika Ndugai awataka wabunge wa ACT-Wazalendo nao wakaape

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,716
Reaction score
9,051
Mbunge alieteuliwa na Rais Magufuli mapema leo tayari amekula kiapo mbele ya Spika Ndugai kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Prof. Manya anatarajia kuapa tena baadae leo kuwa naibu waziri wa Nishati na madini.

Baada ya kuapa kama Mbunge, Prof. Manya alitoa neno la shukraan

Prof. Manya: Kwanza kabisa napenda kumshukuru mwenyezi Mungu ambae yeye ndie hupanga majira na nyakati katika maisha ya wanadamu. Nasema hivyo kwa sababu Ijumaa inakuwa safari yangu ya mwanzo mpya ambao sikupanga mimi, majaliwa ya Mwenyezi Mungu.

Pili nipende kumshukuru mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa heshma aliyonipa ya kuniteua kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, ninapenda tu kusema kwamba, nitafanya majukumu yangu ya ubunge kwa uadilifu ili kwamba kwa pamoja tuweze kulisukuma gurudumu la maendeleo la nchi yetu na Taifa letu na tukimtanguliza Mwenyezi Mungu, asanteni sana.

SPIKA JOB NDUGAI: Kama nilivyoeleza mapema, sisi kama Bunge hatupendi kuwa kikwazo, lazima tuendane na Serikali yetu na Spidi ya Awamu ya Tano na ndio maana tukayafanya mambo tukikimbia pamoja. Nitoe wito kwa wabunge wengine wowote wale, nafikiri kumbukumbu zangu zinaonyesha tuna wabunge wa ACT-Wazalendo wanne ambao bado hawajaapa, napenda kutoa wito wakiwa tayari kutumikia nchi yao kama kweli waliomba ubunge kutumikia wananchi hawana sababu za kuendelea kuzurula huko waliko.

Watoe taarifa kwa spika haraka, tuwapangie ili wapate kiapo waweze kufanya kazi ya mbunge kama ambavyo wananchi waliwaamini, nadhani ni watatu.
 
Hongera kwake na kamati yake ya ufundi. Hakika kama ipo, ipo tu!! Sasa achape kazi na ajipange kuapa asije akawa kama mtangulizi wake

#so sorry mr ndulane😑
 
Yaani Ndungai hafanyi kazi kama spika bali kama moja wa wateule wa Magufuli anaeogopa kutumbuliwa, mtu ameteuliwa usiku asubuhi ameshaamka Kumuapisha ni kama analala na simu kichwani na kapandisha volume hadi mwisho ili bosi wake akimwamrisha hata saa tisa amkute yupo macho.
 
Yaani ndungai hafanyi kazi kama spika bali kama moja wa wateule wa magufuli anaeogopa kutumbuliwa, mtu ameteuliwa usiku asubuhi emesha amka Kumuapisha ni kama analala na simu kichwani na kapandisha volume hadi mwisho ili bosi wake akimwamrisha hata saa tisa amkute yupo macho.
Ameshakujibu huko.

Kasema anakimbiza haya mavitu ili kuendana na kasi ya Malaika mkuu😂
 
Kwani yeye Ndugai ameambiwa ACT wana haraka gani?

ACT wanasubili vikao vya bunge, wabunge wa ACT wataapa ndani ya ukumbi wa bunge kama katiba inavyotaka.

Asitake kuwatumia ACT kutakatisha makosa yake ya kikatiba.
 
Yaani Ndungai hafanyi kazi kama spika bali kama moja wa wateule wa Magufuli anaeogopa kutumbuliwa, mtu ameteuliwa usiku asubuhi ameshaamka Kumuapisha ni kama analala na simu kichwani na kapandisha volume hadi mwisho ili bosi wake akimwamrisha hata saa tisa amkute yupo macho.
Wagogo ni watu wa hovyo sana ndiyo maana wengi ni masikini wa kutupwa, huyo anaonyesha udhaifu wake kwa jiwe bila kificho.
 
Kwani yeye Ndugai ameambiwa ACT wana haraka gani?

ACT wanasubili vikao vya bunge, wabunge wa ACT wataapa ndani ya ukumbi wa bunge kama katiba inavyotaka.

Asitake kuwatumia ACT kutakatisha makosa yake ya kikatiba.
Sasahivi ana mbembeleza wabunge wa upinzani kwenda kuapishwa lakini huyo huyo alishirikiana na Mahera kufuta upinzani
 
Yaani Ndungai hafanyi kazi kama spika bali kama moja wa wateule wa Magufuli anaeogopa kutumbuliwa, mtu ameteuliwa usiku asubuhi ameshaamka Kumuapisha ni kama analala na simu kichwani na kapandisha volume hadi mwisho ili bosi wake akimwamrisha hata saa tisa amkute yupo macho.
Unaweza kuwa sawa kwa 1000%[emoji1][emoji1][emoji1]
 
Sasahivi ana mbembeleza wabunge wa upinzani kwenda kuapishwa lakini huyo huyo alishirikiana na Mahera kufuta upinzani
Suala la kufuta upinzani mkawaulize wananchi mbona hamuelewi
 
Back
Top Bottom