Buseresere iko wilaya ya chato na Katoro iko wilaya ya Geita. Hapo umechanganya
 
Angalia hii

Chato wakaazi 365,127, Geita 1,739,530, Manyara 1,425,131, Kagera 2,458,022, Arusha 1,288,088, Kilimanjaro 1,640,087, Tabora1,717,908, Katavi 564,504. Sensa 2012
Kisha jiulize kwa Nini tunataka kugawa Geita na sio mikoa mingine. Kigezoni kipi
 
Well said bi Kidude, zaidi ya hapo vigezo vya kijiografia na idadi ya watu imezidiwa zaidi ya mara 6 na Mkoa wa Morogoro. No Chato Region, Sukuma Gang sasa mtulie rasilimali zigawanywe sawa. Ova
 
Hivyo vigezo ni vipi?.Kuna mtu yeyote anavifahamu?
 
Bado sio mkoa mtu wa mwisho kutoa au kutotoa hadhi ya mkoa ni Rais,kumbuka hilo ni wazo lililotoka kwa wanachato lakini Kuna mikoa inaathirika Kama kagera,kigoma na Geita yenyewe ambayo inaathirika kwa mipaka yake kubadilika lazima Rais pia ashauriane na wenye mipaka pia.Chato inatuleta hapa ni kwa sababu mtu alikua akipambania na ilipokosa vigezo ndio hiyo Geita.
 
Kama vigezo vipo kwa nini hili suala limekuwa mjadala mkali hadi kumuibua mama wa hela ya mboga ?

Kwa nini Chato wasiambiwe vigezo ambavyo hawajakidhi kuweza kuwa mkoa?
Ofisi ya Waziri mkuu TAMISEMI wanavyo hivyo vigezo!!! Hata kupandisha hadhi ya miji pia hufanywa kwa kutumia vigezo maalum!!
 
Wakikujulisha huvyo vigezo unitaga mkuu. Huu mjadala ni wa hewala hewala na mihemko tu.
Wakiweka vigezo na sifa za kuwa mkoa mtanijulisha maana naona maneno matupu.
 
Kama vigezo vipo kwa nini hili suala limekuwa mjadala mkali hadi kumuibua mama wa hela ya mboga ?

Kwa nini Chato wasiambiwe vigezo ambavyo hawajakidhi kuweza kuwa mkoa?

Bila shaka watakapopeleka hayo maombi yao huko mbele watafahamishwa!
 
Mungu mbariki Tibaijuka
 
Sijaona popote mtu alipotaja vigezo mahususi vya kisheria, taratibu au sera katika kugawa mikoa. Labda uniambie ni posti namba ngapi.
Mkuu Yoda, mada yote hii hujaona popote palipozungumziwa "taratibu na vigezo" ambavyo hutumika (vilikuwa vikitumika) kuanzisha mikoa mipya, kweli?

Hivi mikoa imeanza lini kuanzishwa sehemu mbalimbali Tanzania tokea tupate uhuru? Huwa inafikiriwa tu na mtu mmoja na kuamuru pawepo na mkoa mpya?

Kwenye mada hiihii, ulianzia mwanzo wa mada yenyewe hadi hapa uliponi'quote', na ukakuta kuna baadhi ya mabandiko yakieleza sababu zinazochangia kuanzisha mkoa mpya?
Au unatafuta bandiko maalum linalo orodhesha vigezo vyote kwa pamoja, ndipo ukubali kwamba vimekwishazungumziwa kwenye jukwaa hili?

Sijui kama kuna "sheria" ilitokwisha tungwa kusimamia jambo hilo, lakini najua kuna "taratibu na vigezo" ambavyo hufuatwa katika kukidhi mahitaji ya mahali fulani kuundwa mkoa.

Miaka hii ya karibuni, kama ilivyoelezwa sehemu, hasa katika kuunda mikoa kama Katavi, ndipo taratibu hizo zilikiukwa, na sasa inataka kujirudia na hii Chato.
 
Mkuu umepewa hizo sifa/vigezo/taratibu/sheria zinazotumika kuyafanya maeneo mikoa?
Ukipewa unitag.
Tunaomba orodha ya sifa zinazotakiwa kwa sehemu ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kufuzu kuitwa mkoa. Tukizipata hizo sifa itaturahisishia kujua kama Chato inakidhi vigezo kwa sasa ama la!
 
Kumbe hapa ni changamsha genge tu wala hakuna anayejua vigezo vyenyewe vya eneo kufanywa mkoa.
Bila shaka watakapopeleka hayo maombi yao huko mbele watafahamishwa!
 
Sijaona popote mkuu, labda wewe uniambie posti mmojawapo.
 
Sijaona popote mkuu, labda wewe uniambie posti mmojawapo.
Kuna kurasa 1 hadi 18 sasa hivi. Najuwa ni shida sana kupekuwa moja moja.

Basi tukubali tu kwamba huwa hakuna "taratibu na vigezo" vya aina yoyote ambavyo hutumika ili sehemu ipewe hadhi ya kuwa mkoa!
 
Tuongelee Takwimu za ukubwa wa Mikoa.
Tanzania ina Mikoa 26.
Mkoa mkubwa kuliko yote ni Tabora, wenye ukubwa wa kilomita za mraba, (sq km) 76,171
Wa pili ni Rukwa (75,240 sq km). Wa tatu ni Morogoro (74,139 sq km).
Mkoa wa Geita, wenye ukubwa wa kilomita za mraba 19,592 ni wa 23 kwa ukubwa Nchini mwetu, ukiipita Mikoa ya Mtwara (16,707 sq km), Kilimanjaro (13,209 sq km) na Dar es Salaam (1,393 sq km).
Mwendazake alikuwa Mkabila aliyepitiliza.
Profesa Tibaijuka kasema ukweli.
Hoja ya kuugawa Mkoa wa 23 kwa ukubwa Tanzania, kati ya Mikoa 26, NI YA UKABILA
Kwa nini asiugawe Mkoa wa Tabora, ambao ni mkubwa zaidi ya mara 3 na robo tatu ya Mkoa wa Geita?
Rais wangu Mama SSH ninaamini ataitendea haki Nchi yetu.
Kama kuna haja ya Mkoa Mpya, basi utokee Tabora
 
Ukishapewa hadhi ya mkoa nenda ukatembee pale 2026 tukiwa hai na utaona mabadiliko makubwa.
Mabadiliko gani?!!uyo mrundi wenu marehemu ndio aliwadanganya hivyo?!!haitatokea Nchi kufanya makosa mengine ya kuwapa warundi madaraka fckn kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…