Prof. Tibaijuka: Kwa sheria ya Mipango Miji ilitakiwa Viwanja 4 vya high density viunganishwe mbele na nyuma kujenga ghorofa Kariakoo!

Prof. Tibaijuka: Kwa sheria ya Mipango Miji ilitakiwa Viwanja 4 vya high density viunganishwe mbele na nyuma kujenga ghorofa Kariakoo!

Rushwa rushwa rushwa

Rushwa rushwa rushwa

Ova
 
Mwenye gorofa hana hatia, angeelimishwa, aliyeruhusu ndie mwenye hatia, labda alikuwa mhandisi bandia au wale wanaonunua mitihani.
 
Kwa miji inayokuwa kwa kasi kama Dodoma hili alilosema lifanyike kabla hali haijawa mbaya,hasa pale katikati ya mji maana nimeona kuna vigorofa vya walafi vinasimama kwa speed ya SGR......
 
Mbobezi wa Makazi duniani Prof Tibaijuka amesema pale Kariakoo Kwa mujibu wa sheria ya Mipango Miji ilitakiwa Viwanja 4 vya High density viunganishwe mbele na nyuma Ili Kujenga ghorofa

Nimeogopa sana Kwa yale maghorofa ya Kikinga yaliyojaa Kariakoo na Manzese

Baadae Mlale unono 🐼

----
POLENI WAHANGA WA GHOROFA lililoanguka ila Ujenzi wa maorofa Kariakoo. NI JANGA KAMA LA JANGWANI.
Kwa sheria za mipango miji ilitakiwa viwanja 4 vya high density viunganishwe mbele na nyuma kipatikane kiwanja kimoja kikubwa cha kujenga orofa imara yenye basement kubwa kupaki magari. Orofa inayofunguka kwenye mtaa wa mbele na nyuma.

Awali katika awamu ya Tatu Ushauri huo wa watalaamu wa mipango miji ulishapuuzwa na viongozi kwa presha ya wawekezaji kwa hiyo maorofa Kariakoo na kwingineko yanajengwa kiholela kwenye viwanja visivyokidhi vigezo. Pamoja na madhaifu ya usimamizi wa UJENZI KIUHANDISI Ni vigumu majengo kuwa imara bila kuwa na eneo la kutosha kujenga kitako yaani base foundation stahiki. Naendelea kuhimiza kurekebisha kosa hilo.

Sasa tunavuna hasara kubwa ya upotevu wa mali.. na maisha na fursa za ajira na aibu ya kushindwa kusimamia viwango vya ujenzi Miaka 63 baada ya uhuru.. Tuwaombee wahanga auheni na waliopoteza maisha pumziko la milele.

Naendelea kushauri viwango vya vertical development vizingatiwe kuanzia sasa. Tujisahihishe.
Rekebisha Kiswahili, sio wahanga ni waathirika
Ufafanuzi
1. Mhanga ni mtu anayepatwa na tatizo licha ya kufahamu madhara ya yeye kuwepo, kutenda au kufanya kitu fulani lakini anaamua binafsi kufanya, kwenda mahali kisha anapatwa na janga alilioonywa mwanzo
2. Mwathirika ni mtu ambaye amekutana na janga bila onyo wala taarifa za madhara ya kuwepo mahali fulani au kufanya shughuli fulani.

Walioumia au kupoteza maisha katika tukio la kuporomoka na kufunikwa kifusi cha ghorofa hawakujitakia wenyewe kwa hio sio wahanga ni waathirika.
Acheni kubananga Kiswahili.
 
Prof.Tibaijuka aliyewahi Kuna Waziri wa Ardhi amesema wao walitoka ushauri wa Kitaalamu na miongozo ya ujenzi wa magorofa Kariakoo lakini Ilipuuzwa na Serikali ya Hayati Mkapa Kwa sababu ya pressure ya wawekezaji.

Aidha ikumbukwe Tibaijuka amewahi nukuliwa akisema awamu ya 4 walipuuza ushauri waliipewa kujenga karakaba ya BRT Jangwani panapojaa maji enzi hizo Waziri wa Ujenzi akiwa Mwendazake Magufuli.

View: https://x.com/Jambotv_/status/1858745478529057002?t=1vfuy_Qns5aALVwPT7s_FA&s=19

My Take
Tutarajie magorofa maeneo mengi ya Nchi hasa huko Kariakoo kuendelea kuporomoka kadiri ya mda unavyoenda.

Na tunapojifanya kulia sijui maombilezo na hatujifjnzi basi tuendelee kulia sana na kumsingizia Mungu na shetani Kwa ujinga wetu.
 
Na hakukuwa na haja ya kuunda tume nyingine ya watu 19.. Wan at I kuna tume ilishaundwa na EL na zile findings zote za ile tume hazijawahi kufanyiwa kazi na ndio hizohizo za sasa
Wangeanzia na tume ya EL kama kweli wani serious
Akili hiyo wanayo sasa? One if the thing nilijifunza wkt baddo sijatoka huko ni kwamba most of gov institution hazifanyii kazi past data. Due t political influence wataanza upya.
 
Inabidi iundwe tume ya kuchunguza hizi tume zinazoundwa kuchunguza matukio halafu matukio hayo yanajirudiarudia
 
Na wahusika inawezekana bado wapo kwenye ofisi za umma kana kwamba walifanya vizuri.
 
Back
Top Bottom