Prof. Tibaijuka: Mimi nilikataa Kituo cha Mabasi ya Mwendokasi kujengwa Jangwani, Sikuwa na Madaraka ya Kuzuia

Mama Amon ana vituko...

1701213786711.png
 
Mtaalam wa mipango miji ####£&

Mipango miji gani mmeshafanya

Kuhusu jangwani hilo eneo lote

Linafamika kama hazardous area

Kwanini wataalam sijui wasomi walienda jenga hapo?

Kwanini serikali iliwachilia pia watu wajenge maeneo hayo?

Nchi hii ngumu sana

Ova
Mwenzio ni mtaalam wa uchumi mipango miji Iko huko na alihudumu kama mkurugenzi wa UN habitat
 
Prof. Anna Tibaijuka amesema wakati akiwa Waziri wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, hakutoa Kibali cha Ujenzi wa Kituo cha Mabasi Yaendayo Kasi katika eneo hilo lakini ulifanyika kwa maamuzi yasiyo sahihi

Tibaijuka amesema "Jangwani haina kibali changu kuwa pale. Mimi nilikataa lakini sikuwa na madaraka kuzuia na hivyo pakajengwa, nilikataa kabisa Serikali yote inajua. Nilisema mimi kama mtaalamu wa Mipango Miji hamuwezi kuweka Kituo cha Mabasi kwenye eneo la Bwawa. Pale panajulikana ni Bwawa patafurika"

Ameongeza kuwa suala Upangaji Miji ni uamuzi wa Rais si Utaalamu, ujenzi wa eneo la Jangwani ulikuwa na mvutano kwasababu hakukuwa na Utashi wa Kisiasa (Political Will) ambapo kama pangetolewa uamuzi wa juu pasingejengwa Kituo cha Mabasi.
Kuna umuhimu wa kuwafungulia mashtaka viongozi wote wanaokiri kufanya makosa yanayoligharimu taifa. Kama maamuzi yalikuwa ya Rais kwa nini aliyekuwa Rais awamu ya nne na Serekali yake na viongozi wakuu wa chama chake wasifikishwe mahakamani?
 
Prof. Anna Tibaijuka amesema wakati akiwa Waziri wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, hakutoa Kibali cha Ujenzi wa Kituo cha Mabasi Yaendayo Kasi katika eneo hilo lakini ulifanyika kwa maamuzi yasiyo sahihi

Tibaijuka amesema "Jangwani haina kibali changu kuwa pale. Mimi nilikataa lakini sikuwa na madaraka kuzuia na hivyo pakajengwa, nilikataa kabisa Serikali yote inajua. Nilisema mimi kama mtaalamu wa Mipango Miji hamuwezi kuweka Kituo cha Mabasi kwenye eneo la Bwawa. Pale panajulikana ni Bwawa patafurika"

Ameongeza kuwa suala Upangaji Miji ni uamuzi wa Rais si Utaalamu, ujenzi wa eneo la Jangwani ulikuwa na mvutano kwasababu hakukuwa na Utashi wa Kisiasa (Political Will) ambapo kama pangetolewa uamuzi wa juu pasingejengwa Kituo cha Mabasi.
Hawa rais wa Tz ni majanga!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Wote tunajua, Kikwete akiwa rais akitoa sahihi ujenji wa barabara Morocco alisema anashangaa udart wamejenga Jangwani. Kama rais mwenye mamlaka anasema anashangaa unategemea Nini.
Alivyo kigeugeu huyo, hata kama alitoa amri kwenye vikao vya ndani, hadharani atashangaa. Rais asiyejua kwa nini nchi ni masikini! Mchakato wa katiba je, hakuuridhia, akautolea pesa na mwishoni anamruka hadi Mwenyekiti aliyemteua mwenyewe, kuwa ana kwenda kinyume(na nini)?

Back
Top Bottom