Profesa Assad amkabidhi ofisi CAG mpya, hakuona haja ya kupiga danadana

Huyu jamaa ni mfano wa kuigwa kwa viongozi wote, wangekua diligent kama huyu jamaa nchi ingekua mbali sana, viongozi wa bongo wangeamua kuchapa kazi hii miaka mitano tungekua tumefanya double au triple ya tuliyofanya leo, ila wengi wamekalia kufuatilia wanaume wanaoishi na wadada ambao hawajawaoa, wengine ni kamatakamata, wengine wanatembea na camera men kila siku kuuza sura mjini kujionyesha kua wanafanya kazi, wengine wanavamia vituo, wengine wanawaambia watu wazima kua watawachapa viboko, wengine wanakamata mtu kisa kabadilisha kichwa chake na rais kwenye picha (comedy), ujinga mtupu, nyani tu.
 
Profesa Asad umuhimu wake utakuja kufahamika kuanzia mwaka 2025 watakao bahatika kufika muda huo watakiri. Hata wale waliomdhihaki watamwomba msamaha japo kwa dhihaka ila Mungu ataisukuma mioyo ya wale wakosaji ili kumwinua huyu profesa asiye na mawaa. Mungu ibariki Tanzania na kawaangushe wale wanafiki wachumia tumbo
 
Hiki ni kitendo kilichofanyika bila kuchelewa , hajataka kuleta longolongo ili waseme kuna mafaili yametoroshwa .

Kila la heri Profesa Assad
******

Prof. Assad:
"Hii ni taasisi na makabidhiano ya taasisi yanaenda kwa maandishi, kwa hiyo makabidhiano kwa maandishi yatafanyika Dodoma kwa sababu ndiyo kule makao makuu yetu yalipo"

"Kazi ya CAG ni kusaini ripoti lakini ripoti unachukua wajibu wa kazi ya watu wengi sana, ambao waliifanya maeneo mbalimbali hapa Tanzania, kwa hiyo nukta yangu ni kuwatazama vizuri sana watu hawa"

"Kama kuna yeyote nilimkosea kwenye utendaji wetu wa kazi basi anisamehe na mimi kuna kuna mambo alinikosea nimemsamehe."

"Baada ya hapa mimi nitafanya kazi ya kulima kwa sababu miezi 2 iliyopita nilianza kuwekeza kwenye kulima, wakinihitaji watu wa Mjini nitakuja, kuhusu changamoto ni nyingi nimepitia mnataka niseme hapa nitatia ukakasi hakuna haja ya kutia ukakasi."

"Nimepokea ofisi hii kutoka kwa Uttoh miaka mitano iliyopita naamini sikufanya uharibifu wowote mimi naamini mabadiliko yanaweza kutokea, lakini yatokee kwenye namna ilivyopangwa vizuri."

CAG Kichere :
"Kama kutakuwa na mabadiliko yatafanyika kwa umakini mkubwa ili tusiharibu mfumo wa utendaji kazi."

"Nimefanya kazi TRA najua ugumu wa kukusanya mapato, nimekuja kulinda mapato, tena nitalinda kwa wivu mkubwa sana, sitakuwa na simile kwa watu wanaotumia mapato ya Serikali vibaya."

"Kama kulikuwa na mahusiano hafifu nitaimarisha mahusiano kati ya Ofisi ya CAG na Bunge."
Hawa MaCAG wote waungwana sana.
Mungu awabariki!
 
CAG amestaafu kwa mujibu wa sheria

Kama wapinzani wanampenda wamwajiri maana kila mwaka wanapata hati chafu ya ubadhirifu wa pesa

CAG apumzike aache kutafuta huruma ya Wananchi yeye sio wa kwanza kushika hicho cheo Kila mtanzania mwenye sifa alistahili kuwa CAG

Muda wake umeisha apumzike amefanya kazi yake

Aache kutumika na wanasiasa wasaliti wa nchi
Hazikutoshi! Kasome uelewe, amestaafu kwa vipi?
 
Jamaa muungwana na akili kubwa pia.Nimemwangalia huko kwa millard
 
Assad kaiharibu na kuivunjia heshima sana hiyo ofisi.

Zitto kamuharibu huyu mzee..akalime sasa Unguja.

Viva Magufuril

Profesa Assad ni muadilifu aliyekutana kwa bahati mbaya na wachafu wanaoigiza uzalendo.
 
Jiwe la wahashi limekataliwa tz Sema jiwe limetokelezea

Hiki ni kitendo kilichofanyika bila kuchelewa , hajataka kuleta longolongo ili waseme kuna mafaili yametoroshwa .

Kila la heri Profesa Assad
******

Prof. Assad:
"Hii ni taasisi na makabidhiano ya taasisi yanaenda kwa maandishi, kwa hiyo makabidhiano kwa maandishi yatafanyika Dodoma kwa sababu ndiyo kule makao makuu yetu yalipo"

"Kazi ya CAG ni kusaini ripoti lakini ripoti unachukua wajibu wa kazi ya watu wengi sana, ambao waliifanya maeneo mbalimbali hapa Tanzania, kwa hiyo nukta yangu ni kuwatazama vizuri sana watu hawa"

"Kama kuna yeyote nilimkosea kwenye utendaji wetu wa kazi basi anisamehe na mimi kuna kuna mambo alinikosea nimemsamehe."

"Baada ya hapa mimi nitafanya kazi ya kulima kwa sababu miezi 2 iliyopita nilianza kuwekeza kwenye kulima, wakinihitaji watu wa Mjini nitakuja, kuhusu changamoto ni nyingi nimepitia mnataka niseme hapa nitatia ukakasi hakuna haja ya kutia ukakasi."

"Nimepokea ofisi hii kutoka kwa Uttoh miaka mitano iliyopita naamini sikufanya uharibifu wowote mimi naamini mabadiliko yanaweza kutokea, lakini yatokee kwenye namna ilivyopangwa vizuri."

CAG Kichere :
"Kama kutakuwa na mabadiliko yatafanyika kwa umakini mkubwa ili tusiharibu mfumo wa utendaji kazi."

"Nimefanya kazi TRA najua ugumu wa kukusanya mapato, nimekuja kulinda mapato, tena nitalinda kwa wivu mkubwa sana, sitakuwa na simile kwa watu wanaotumia mapato ya Serikali vibaya."

"Kama kulikuwa na mahusiano hafifu nitaimarisha mahusiano kati ya Ofisi ya CAG na Bunge."
Duniani likiwa linang'aa
IMG-20191105-WA0040.jpeg
 
Back
Top Bottom