Profesa Assad: Katiba Mpya sawa ila isitupe mtu ambaye hawezi kumsikiliza mtu yeyote kama ilivyokuwa

Profesa Assad: Katiba Mpya sawa ila isitupe mtu ambaye hawezi kumsikiliza mtu yeyote kama ilivyokuwa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Aliyewahi kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Tanzania (CAG), Profesa Mussa Assad amesema ni vizuri kuwa na Katiba Mpya lakini vizuri kuwa na watu wa kutekeleza Katiba hiyo sawasawa.

Amesema hayo alipoenda kutoa maoni yake mbele ya Kikosi Kazi cha Rais, leo Mei 19, 2022 ambapo amesisitiza umuhimu wa kuwa na utawala bora Nchini.

“Tumezungumza namna ya kuongeza utawala bora, Taasisi kama Bunge, Serikali, Mahakama zote ni muhimu kufanya kazi inavyotakiwa, ndio maana miaka hii iliyopita wote tulifika mahala wote tukawa tunaogopa kusema chochote kwa kuwa kulikuwa na mtu ambaye hakuna mtu ambaye anaweza kumsikiliza,” - Profesa Assad.
 
Serikali ambayo hata mil.10 zinaidhinishwa na Rais na Msemaji wa Ikulu anatoa Press release?
 
Kuna watu wana udhaifu wa kutosamehe waliokufa juu ya mapungufu yao,wataendelea kuyasema tu.

Professa assad ni mtu mzima lakini katika hili naona kila siku vijembe kwa magufuli,kama ana lake moyoni basi haliishi tu tokea alipoanza kumsema ?

Hali ya utawala wa magufuli ulikuwa unafahamika na kila mtu hapa nchini,hakuna haja ya kuanza kupiga vijembe kwa jambo ambalo liko wazi kwa watu.

Profesa aatuli,atoe mawazo aachane na marehemu,inatia kinyaa sana kumzungumzia mtu ambaye ameshakufa
 
Mtu anapotoa ushauri sio lazima utekelezwe.

Kwahiyo kusema mtu hashauriki wakati ana uhuru wa kupokea au kutopokea ushauri ni kumnyima haki ya kufanya maamuzi.

Kama una mrefer jiwe, alishasema hashauriki na ukimshauri umeharibu.
 
Mtu anapotoa ushauri sio lazima utekelezwe.

Kwahiyo kusema mtu hashauriki wakati ana uhuru wa kupokea au kutopokea ushauri ni kumnyima haki ya kufanya maamuzi.

Kama Katiba itakuwa imeiwezesha nchi kuwa na taasisi imara , Rais hatakuwa na nafasi ya kufanya mambo kwa utashi wake. Mfano mzuri ni jinsi Marehemu Magufuli alivyokuwa anakiuka Katiba kwa kutumia fedha nyingi kujenga kiwanja cha Ndege kwao CHATTLE na pia kununua Ndege bila kupata idhini ya Bunge !! Tukiwa na Bunge imara lenye wabunge waliopatikana kwa ridhaa ya wananchi, Rais akikiuka Katiba atakuwa impeached na hata kuachishwa kazi!!
 
Back
Top Bottom