Profesa Assad: Katiba Mpya sawa ila isitupe mtu ambaye hawezi kumsikiliza mtu yeyote kama ilivyokuwa

Profesa Assad: Katiba Mpya sawa ila isitupe mtu ambaye hawezi kumsikiliza mtu yeyote kama ilivyokuwa

Miaka yote ya utawala mzuri wa Rais Samia, unaweza ukajikuta umeisha la maana ikawa walikuwa wakimsuta Marehemu JPM

Nyie wasomi, fanyeni kazi sasa, achaneni na asiyekuwepo, we mzee na uprof wako kazi yako kutwa nzima, usiku kucha ni kusema viumbe visivyoonekana?

Mnaendekeza ujinga ujinga tuu, mnapata faida gani kukaa mkimsuta asiye binadamu sasa?
 
Utadhani ana PhD ya political science, hadi leo analia lia na nafasi ya CAG? Mbona halilii nafasi yake UD? Nilishamuona ni mtu wa hovyo tu! always comments zake zinazuiliwa na mambo ya kidini. Ni mdini.
Umeongea ukweli mtupu watu wanaogopa kumueleza ukweli huyu mzee ni hovyo
 
Aliyewahi kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Tanzania (CAG), Profesa Mussa Assad amesema ni vizuri kuwa na Katiba Mpya lakini vizuri kuwa na watu wa kutekeleza Katiba hiyo sawasawa.

Amesema hayo alipoenda kutoa maoni yake mbele ya Kikosi Kazi cha Rais, leo Mei 19, 2022 ambapo amesisitiza umuhimu wa kuwa na utawala bora Nchini.

“Tumezungumza namna ya kuongeza utawala bora, Taasisi kama Bunge, Serikali, Mahakama zote ni muhimu kufanya kazi inavyotakiwa, ndio maana miaka hii iliyopita wote tulifika mahala wote tukawa tunaogopa kusema chochote kwa kuwa kulikuwa na mtu ambaye hakuna mtu ambaye anaweza kumsikiliza,” - Profesa Assad.

Watu weengi wanaongelea kuhusu KATIBA MPYA. Lakini tatizo la waTanzania ni moja tu, UTII WA SHERIA. Lazima tuwe wa wakweli, waTanzania hatuna desturi ya kutii sheria bila shuruti. Hili lipo kuanzia ngazi ya familia kuna uasi na watoto kutokutii sheria. Kutofuata na kutozingatia sheria inaonekana ni desturi iliyoenea na kukubalika miongoni mwa waTanzania. Lkn hilo haliongelewi, wanaongelea katiba mpya. Kwa ufupi ni kuwa katiba mpya haiwezi kumbadilisha mtu na kuwa mtiifu. Naomba niishie hapo.
 
Kuna watu wana udhaifu wa kutosamehe waliokufa juu ya mapungufu yao,wataendelea kuyasema tu.

Professa assad ni mtu mzima lakini katika hili naona kila siku vijembe kwa magufuli,kama ana lake moyoni basi haliishi tu tokea alipoanza kumsema ?

Hali ya utawala wa magufuli ulikuwa unafahamika na kila mtu hapa nchini,hakuna haja ya kuanza kupiga vijembe kwa jambo ambalo liko wazi kwa watu.

Profesa aatuli,atoe mawazo aachane na marehemu,inatia kinyaa sana kumzungumzia mtu ambaye ameshakufa
Ni muhimu azungumziwe, bila kuzungumziwa watu watajifunza vipi? Hao akina Hitler au Idd Amin mpaka leo wanazungumziwa itakuwa huyu dictator wa juzi kati hapa ndiyo asizungumziwe?
Goodness udikteka wake ndiyo legacy aliyoiacha na proof ni hivi anavyozungumziwa.
 
Aliyewahi kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Tanzania (CAG), Profesa Mussa Assad amesema ni vizuri kuwa na Katiba Mpya lakini vizuri kuwa na watu wa kutekeleza Katiba hiyo sawasawa.

Amesema hayo alipoenda kutoa maoni yake mbele ya Kikosi Kazi cha Rais, leo Mei 19, 2022 ambapo amesisitiza umuhimu wa kuwa na utawala bora Nchini.

“Tumezungumza namna ya kuongeza utawala bora, Taasisi kama Bunge, Serikali, Mahakama zote ni muhimu kufanya kazi inavyotakiwa, ndio maana miaka hii iliyopita wote tulifika mahala wote tukawa tunaogopa kusema chochote kwa kuwa kulikuwa na mtu ambaye hakuna mtu ambaye anaweza kumsikiliza,” - Profesa Assad.
Profesa mwenye dharau na Kibri ambaye anajifanya ni mjuzi wa kila kitu.Mtu alishafariki dunia lakini bado unazidi kumongeleaongelea.Kama na kuondolewa kile cheo,ni wengi wanaondolewa lakini wanatazama mbele na siyo kuongeaongea mambo ya nyuma utafikiri wazee wa vijiweni.Alishawahi kusema eti tulikuwa na 'Dubwana' hapa.Kejeli na majina yasiyofaa kuwaita watu wengine siyo sifa nzuri katika Uislam na Muislam kama anavyoonekana ila Mwenyezi Mungu ndiye anamjua zaidi.Acha' KIBRI' hiyo ni sifa ya Muumba wako,siyo wewe.
 
Mbona Nyerere anazungumzwa??
Pia napinga kwa wao kuzungumzwa kwa mifano mibaya,sio kwwmba napinga kuzungumzwa magufuli tu bali mpaka nyerere napinga asizungumzwe.
 
Mtu anapotoa ushauri sio lazima utekelezwe.

Kwahiyo kusema mtu hashauriki wakati ana uhuru wa kupokea au kutopokea ushauri ni kumnyima haki ya kufanya maamuzi.
Inategemea na aina ya ushauri kwa sababu, kuna baadhi ya mambo ukishauriwa lazima utekeleze vinginevyo utaumia.

Mfano:
Ukiwa unataka kuwaonyesha watu kuwa wewe ni sugu kwa kushika Kaa la moto kwa mikono mitupu hali ya kuwa huna usugu wowote, then ikatokea ukashauriwa usishike kaa la moto kwa mikono Kwa sababu utaungua, na wewe ukakaidi kutekelza huo ushauri Je, nini kitatokea?

Kumbukumbu Rejea:
Wote tunakumbuka sakata la korosho na hatima yake, wataalamu walishauri kisha wababe wakagoma kutekelza ushauri, eti kwa sababu tu alitaka kuuonyesha umma kuwa wana uwezo wasiokuwa nao.

Kilochotokea hakuna atakae rudia tena, na hata akifufuka akarudishwa pale alupoondokea hato rudia tena Shubaaamit zake Mxieusssszz!!!
 
2025 tungetest mitambo kwa Prof Assad angalau miaka 5 tu. Anaupiga mwingi sana
Unaweza kukuta akaboronga, unajua kukosoa ni rahisi sana kuliko kutenda na hasa wabongo tulivyo na tabia ya kupigania tusiyoyaamini.
 
profesa naye atenganishe muda wa smile na kuuchuna. mimi siku zote namuona akiiuchna tuu!
Assad na mwenzie Ramadhan Dau ukiwaona utafikiri ni watu wa maana kumbe ni wanafiki ambao chini ya ngozi yao umejaa ubaguzi wa kidini uliokithiri!! Kwa wale wanaowafahamu toka wakisoma UDSM mpaka walipoanza kazi nje ya chuo kikuyu watakubaliana na observation yangu!
 
Ni muhimu azungumziwe, bila kuzungumziwa watu watajifunza vipi? Hao akina Hitler au Idd Amin mpaka leo wanazungumziwa itakuwa huyu dictator wa juzi kati hapa ndiyo asizungumziwe?
Goodness udikteka wake ndiyo legacy aliyoiacha na proof ni hivi anavyozungumziwa.
Nani sasa wa kujifunza hao viongozi wa ccm?
 
yule baba kaburini ndiko sehemu sahihi kuweko maana kama angelikuweko mpaka leo hatujui wangapi wangebaki na mavi yao nyumbani
Bila Mungu kuingilia kati hii nchi ingeharibika sana,....in H.Rungwe's voice.
 
Utadhani ana PhD ya political science, hadi leo analia lia na nafasi ya CAG? Mbona halilii nafasi yake UD? Nilishamuona ni mtu wa hovyo tu! always comments zake zinazuiliwa na mambo ya kidini. Ni mdini.
Ni kweli hawa wote ni watu wa brabra tu! Magufuli hakuhitaji watu wajinga wajinga kama huyo mdini! Unashuti ujinga halafu akusikilize! Kwani hawakuwahi kumsikia Makamba anasema alipihiwa simu na Magufuli kuombwa ushauri lakini Magufuli baada ya kuusikiliza ushauri ile akamwambia ushauri wako sio mzuri! Sasa huyu nae anasema alikuwa hataki ushauri kivipi? Stupid Professor!
 
Back
Top Bottom