Aliyewahi kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Tanzania (CAG), Profesa Mussa Assad amesema ni vizuri kuwa na Katiba Mpya lakini vizuri kuwa na watu wa kutekeleza Katiba hiyo sawasawa.
Amesema hayo alipoenda kutoa maoni yake mbele ya Kikosi Kazi cha Rais, leo Mei 19, 2022 ambapo amesisitiza umuhimu wa kuwa na utawala bora Nchini.
“Tumezungumza namna ya kuongeza utawala bora, Taasisi kama Bunge, Serikali, Mahakama zote ni muhimu kufanya kazi inavyotakiwa, ndio maana miaka hii iliyopita wote tulifika mahala wote tukawa tunaogopa kusema chochote kwa kuwa kulikuwa na mtu ambaye hakuna mtu ambaye anaweza kumsikiliza,” - Profesa Assad.