Profesa Assad: Katiba Mpya sawa ila isitupe mtu ambaye hawezi kumsikiliza mtu yeyote kama ilivyokuwa

Profesa Assad: Katiba Mpya sawa ila isitupe mtu ambaye hawezi kumsikiliza mtu yeyote kama ilivyokuwa

Kwa lugha nyepesi "je uwezo wa Watu Kuisimamia katiba mpya upo?" Kama tunao uwezo tutafaidika sana na katiba mpya, lau kama hatuna watu wa kusimamia na kuitekeleza kinaweza kuwa kiroja!
waliopo madarakani ambao ndio wenye political will na fedha je wanataka hiyo katiba mpya ambayo itawabana wasiibe?
 
hivi rais anaweza kuwa na washauri wangapi zitto anataka kuwa mshauri profesa assad anataka kuwa mshauri nnape naye makufuli atatashauriwa na watu wangapi kweli angewasikiliza hawa angeweza kufanya makubwa kama alivyofanya, ona mama anawashauri wengi maendeleo hakuna
 
Aliyewahi kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Tanzania (CAG), Profesa Mussa Assad amesema ni vizuri kuwa na Katiba Mpya lakini vizuri kuwa na watu wa kutekeleza Katiba hiyo sawasawa.

Amesema hayo alipoenda kutoa maoni yake mbele ya Kikosi Kazi cha Rais, leo Mei 19, 2022 ambapo amesisitiza umuhimu wa kuwa na utawala bora Nchini.

“Tumezungumza namna ya kuongeza utawala bora, Taasisi kama Bunge, Serikali, Mahakama zote ni muhimu kufanya kazi inavyotakiwa, ndio maana miaka hii iliyopita wote tulifika mahala wote tukawa tunaogopa kusema chochote kwa kuwa kulikuwa na mtu ambaye hakuna mtu ambaye anaweza kumsikiliza,” - Profesa Assad.
Mpaka sasa hakuna aliyeweza kufuata katiba vizuri kama Jk. JPM na huyu mama ndio wanoongoza kuibaragaza katiba
 
yule baba kaburini ndiko sehemu sahihi kuweko maana kama angelikuweko mpaka leo hatujui wangapi wangebaki na mavi yao nyumbani
Na huyu mama asiobadilika shauri yake manabii tumeshanena
FB_IMG_16530413371179364.jpg
 
Nyie tulishawajua miaka mingi sana hamtusumbui tena

prof Lipumba wakati anamsifia JPM anakuwa kahongwa pesa, akimsifia Samia anakuwa Mdini

ila James Mbatia akimsifia JPM kwa demokrasia na akimponda Samia kwa utawala mbovu hawi mdini

Zitto akimponda JPM kwa kukiuka demikrasia na akimsifia Samia kwa kuboresha Demokrasia anakuwa Mdini japo maneno hayo hayo yakitamkwa na Mbowe inakuwa sawa

Ananile Nkya na kina kijokisimba walimponda JK kwa demokrasia wakaufyata kwa JPM hawawi wadini

Bakwata wakimsifia JPM wanakuwa wamehongwa ila wakimsifu Samia wanakuwa wadini

hata wale waislam oya oya wameanza kuwaelewa na ndio sababu lawama zenu hazina impacts hata kama mna hoja mnaonekana mna agenda ya siri
Utadhani ana PhD ya political science, hadi leo analia lia na nafasi ya CAG? Mbona halilii nafasi yake UD? Nilishamuona ni mtu wa hovyo tu! always comments zake zinazuiliwa na mambo ya kidini. Ni mdini.
 
Hii inchi inafaa kutawaliwa kidikteta tu , full stop,

Hizi vimaneno maneno zenu ndiyo zinatudisha nyuma na kutuchelewesha
 
Huyu mzee anasononeko la moyo mpaka linamkereketa.huyu Mzee anatakiwa kukubali Rais ni cheo kikubwa Sana na anakuwa anajidhalilisha kuzungumzia kitu kinachomtesa.
Sasa hapa umeongea nini? Au ni chuki kwa Profesa ama ni mada isiyokufurahisha?

Kama anasononeko, kitaalam njia pekee ya kumwepusha na madhara makubwa yatokanayo na sononeko hilo ni kulisema linalomsononesha kwa uwazi na kulitafutia ufumbuzi.

Kwa hoja yako hiyo ukajielimishe tena
 
Sasa hapa umeongea nini? Au ni chuki kwa Profesa ama ni mada isiyokufurahisha?

Kama anasononeko, kitaalam njia pekee ya kumwepusha na madhara makubwa yatokanayo na sononeko hilo ni kulisema linalomsononesha kwa uwazi na kulitafutia ufumbuzi.

Kwa hoja yako hiyo ukajielimishe tena
Sisi tunaangalia maudhui ya hoja ya profesa. Huyo anaeona ni masononeko akafukue shimo Chato amshitaki pofesa.
 
Mtu anapotoa ushauri sio lazima utekelezwe.

Kwahiyo kusema mtu hashauriki wakati ana uhuru wa kupokea au kutopokea ushauri ni kumnyima haki ya kufanya maamuzi.
Kwa mujibu wa katiba ya URT. halazimiki kufuata ushauri wa mtu yeyote yule! Pigia mstari halazimiki
 
Back
Top Bottom