Profesa Assad ni muongo, duniani 73% ya ndege zote za biashara hununuliwa kwa pesa taslimu

Profesa Assad ni muongo, duniani 73% ya ndege zote za biashara hununuliwa kwa pesa taslimu

Hivi alikumbuka kuwaambia kuwa mtu ukikopa gharama zinakuwa juu zaidi ya uñunuzi wa hizo ndege kwa cash? Na pia kwa mfano kipindi chote cha corona ndege zilikuwa haziruki, kama zingekuwa zimekopwa hela ya kulipa hayo madeni ingetoka wapi? Pathetic profools, nilikuwa namwelewa lkn kwa hili naona kavuka mipaka. Aache unafki.
Wanafanya kitu kinachoitwa "Debt Rescheduling" and this is acceptable in the event of a Force Majeure.
 
Nimesikitika kuona msomi kama Assad aki-personalize tofauti zake na Hayati Magufuli kwa kusema mtu kichaa tu ndie ananunua ndege kwa cash, profesa akasema mikopo/lease ndio njia sahihi...
Hakimu mfawidhi, Za kuambiwa changanya na za kwako.
 
Umeshawahi kuishi nje au unaropoka tu.
Kuanzia simu,gari,nyumba na n.k kasoro msosi asilimia 90 ni kulipa kodogo kidogo ndio maana unashangaa dada yako wa ulaya kuona kakutupia picha whatsapp hana miliki ndinga kali kumbe kulipa kidogo kidogo tena kwa mkopo
Dunia nzima kwa nchi zilizo endelea hakuna cash na wanaogopa ni kosa
Hivi kwanini ununue cash hali riba ya mkopo ulaya inacheza jirani na sifuri?
 
Nimesikitika kuona msomi kama Assad aki-personalize tofauti zake na Hayati Magufuli kwa kusema mtu kichaa tu ndie ananunua ndege kwa cash, profesa akasema mikopo/lease ndio njia sahihi....
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo anapomwita Professor wa fani yoyote muongo, mwenye akili yeyote ataelewa kwa nini kila masikini mwenye kesi Mahakamani analia kwa kutopewa haki.

Professor alikuwa na maana ndege za abiria hazinunuliwi cash kama Udaga au maandazi ambapo mtu anakwenda kwa muuzaji na pesa yake na kununua kiasi anachohitaji, ndege unatoa order ambayo inaweza kumchukia miaka ndo waanze kushughulikia.

Ndege, bila kutoa malipo yoyote, unatoa order inayoweza kuchukua miaka ili utengenezewe aina unayotaka na zamu ya order ikifika, utaombwa uthibitishe ili waanze kutengeneza na pia ujiandae kulipa.
 
dhamira ya serekali ilikuwa nzuri hilo halina ubishi ila approach yake ni mbovu na lazima ikanwe isikae ijirudie tena. kununua hayo mandege bila kufata utaratibu ni mbaya zaidi kuliko kutokununua kabisa...
Hujui biashara ilivyo ndo maana huelewi unachokisema. Hakuna biashara ya kulala masikini na kuamka tajiri
 
Mkuu, mimi kukataa alichokisema Professa haina maana kua nilikua ama namshabikia Hayati Magufuli.

Tusipende kujumuisha vitu, generalisation syndrome ni ugonjwa wa akili.
Ni kweli wewe hujawahi kumshabikia magufuli kama watu huwa wanafuatilia post za humu kwa umakini, kwa lengo la kuelewa na kujenga. Shida imekuja namna ulivyomkosoa Assad watu hawajakuelewa na wamekuchanganya kwenye kundi la Mataga 😀
 
Huyu Assad anawaza kimaskini, kwahiyo ukikopa ndo unapunguziwa bei ya ndege. Yaan sijui anafikiria kwa kutumia nini? Tangu lini mkopo ukawa cheap? Magu alikuwa anawajua wanafki kama assad ndo maana hakutaka kufanya nao kazi. Tanzania ilikuwa ni kama pori lenye wanyama wakali kama assad, hawa walipaswa kupotezwa kabisa. Magu kaondoka kaacha projects za kibabe, sasa tuone hao wanaoongoza kwa maneno na siyo vitendo kama watazikamilisha. JPM alichokifanya yuko sahihi asilimia mia, katka uongozi wa nchi zetu za kiafrika output ndio kila kitu, haijarishi umetumia njia zipi kupata tangible thing. JPM ni output siyo maneno maneno yenu.
Hatutaki output zenu kwa gharama ya maisha ya watu, Tafuteni nchi yenu nyingine mfanye output kwa gharama za wananchi, siku hao wananchi wakiisha mtajua hizo output zitamfaidisha nani.

Tena unasema kabisa akina Assad walipaswa kupotezwa kabisa, Shame on you! Btw, Wapotezaji mmefikia wapi katika output zenu? 😀 Atake asitake....... Nchi yangu ni afadhali mtu apotee sio pesa ipotee. !!!!!
 
Wanafanya kitu kinachoitwa "Debt Rescheduling" and this is acceptable in the event of a Force Majeure.
Sasa shida zote hizo za nini wakati hela ipo. Tununue tu. Sisi ni nchi tajiri na sio masikini tuanze kukopa kopa kila siku.
 
Hy assad nae hana maana mbona kipindi yupo serekarini Tanzania bd ilikuwa masikinii
 
Nimesikitika kuona msomi kama Assad aki-personalize tofauti zake na Hayati Magufuli kwa kusema mtu kichaa tu ndie ananunua ndege kwa cash, profesa akasema mikopo/lease ndio njia sahihi....
Ita waandishi zungumza mbele yao ujinga wako huu
 
Nimesikitika kuona msomi kama Assad aki-personalize tofauti zake na Hayati Magufuli kwa kusema mtu kichaa tu ndie ananunua ndege kwa cash, profesa akasema mikopo/lease ndio njia sahihi...
Hakuna shirika linanunua Ndege kwa cash kote wanakopa isipokuwa Tanzania kulikuwa na wizi mkubwa magufuli na kikundi chake wakapiga 10% cha juu kwa cash kwani Bei halisi ya Ndege ni tofauti na bei waliyoitangaza na ndiyo maana magufuli hakutaka CAG asogee kwenye ununuzi wa Ndege kwa sababu alijua ataumbuka haraka
 
Na kuhusu "compensation credits provided by Boeing to settle estimated damages" unaizungumziaje?
Southwest disclosed that it received $428 million in initial compensation from Boeing.
Hiyo ni compensation kuwa ndege ziliagizwa tangu mwaka jana lakini boeing hawakudeliver hawakudeliver muda wote kutokana na matatizo yaliyokuwapo.

Hata sisi tuliwahi kupata compensation ya dola elfu kadhaa walipochelewesha ile dreamliner kwa siku sijui nne- sina uhakika. Ni kwa sababu wanakuwa wameshalipwa ndiyo maana wanalazimika kulipa comnsation hiyo
 
Walioko subuleni kwa baba yako,pumbafu ww.Ni lini bunge lilipitisha budget ya kununua mindege,ambayo haikufuata utaratibu wa manunuzi?Nyie ni mazombie yake,endeleeni kuabudu huo mzimu wenu maana hata muubiriwe vipi sio riziki kwakua aliwapa ulaji mmefutuka mithili ya mighulube ya Mbeya
Ununuzi wa Ndege umejaa ufisadi mkubwa na mojawapo wa dalali ni Bashite na wengine ni waziri wa uchukuzi kipindi kile
 
Unajua cash weka basi mfumo na utaratibu ulioutumia kununua hizo ndege Kwa cash
Kwa nn unauficha?
Walinunua kwa cash ili wapige chao 10% kwa cash na ndiyo chanzo cha Doto kuwa tajiri mkubwa mpaka sasa
 
Nadhani concept ya kununua ndege kwa mkopo vs kununua kwa cash wewe huijui ama hujaielewa.

Issue iko hivi.
1. Ununuzi wa ndege za kibiashara (airline) ni jambo la gharama na uwekezaji wa kibiashara. Hivyo badala ya kwenda kukopa benki pesa taslimu (cash) ili ukawalipe wauza ndege kwa cash, wao wauzaji wanabeba dhamana ya kibenki kwa kukupa ndege kwa mkopo. Hii ni njia bora, rahisi na cheaper zaidi kuliko kukopa benki...
Ununuzi wa Ndege za Tanzania kwa cash lengo lake ilikuwa kupiga kuiba Yaani ufisadi ndiyo maana ununuzi wake una utata hauna baraka za bunge wala wananchi, kuna 10% kila idara na hata bei halisi ya Ndege ni tofauti na cash waliyodai kulipia, kuna udanganyifu mwingi kwenye hayo manunuzi
 
Usidandie gari kwa mbele , nimekuambia kulikuwa na upigaji Je hujui kuwa aliwahi kiwa mjumbe pale NSSF (as it then was)? Ujenzi wa majengo ya ovyo ovyo ambayo hayawezi kurudisha ghalama haraka , hivyo poteza pesa za wafanyakazi. Yeye Assad wakati wa tenure yake alifanya nini? The guy has no clean hands , akae kimya , aache siasa , Kama ni kadi yake ya CUF basi aendeleze tujue. Aache kushutumu marehemu ambaye hawezi kuja kujitetea Sasa hivi.
Usikariri, gari ikiwa inarudi nyuma unatakiwa udandie mbele, na ikiwa ianenda mbele dandia nyuma... Ukikariri kudandia ni nyuma tu siku utakutana nayo inarudi nyuma ufe..

Wakati akiwa huko, kuna pahala panaposema yeye ndo kaiba?
 
Back
Top Bottom