Mzee Pius Msekwa alianza kazi kama katibu wa bunge. Katibu wa bunge ni mtumishi wa umma. Samuel Sitta aliwahi kuwa DG wa TIC kabla ya kuwa Spika; mfanyakazi wa TIC ni mtumishi wa umma Job Ndugai aliwahi kuwa mtumishi wa TANAPA, hii nayo ni taasisi ya umma.
Huyu profesa auze vision yake akiwa spika, atafanya nini na bunge ataliendeshaje ili maadui watatu umasikini, ujinga na maradhi viondoke kwa haraka.
Kuna adui mwingine ukosefu wa ajira na mitaji au dhamana ya kupata mitaji ili wawe sehemu ya kuzalisha kwa kutumia elimu na nishati waliyonayo.
Suala la Tz haijawahi kutoa spika ambae ni mtumishi wa umma ni nyepesi sana, kwani wapiga kura wa spika sio watumishi wa umma, na hata ingekuwa spika anachaguliwa na Watz wote, bado number ya watumishi wa umma ni ndogo sana kumfanya mgombea ashinde kiti cha uspika.
Otherwise, kulikuwa na hoja ya James Mbatia kwenda mahakamani kusimamisha mchakato wa kinyang'anyiro cha uspika kwa kuwa barua ya aliekuwa spika ilikuwa addressed kwa mamlaka nyingine na sio katibu wa bunge. Jim Mbatia kafikia wapi??