Profesa Janabi apuuzwe!

Profesa Janabi apuuzwe!

Uzuri ni kwamba, Prof Janabi huwa anatoa ushauri. Na wala siyo shurti kuufata ushauri wake kwa muda huo.

Ila ikifika wakati, utalazimika tu. Kwa sasa wala usiwaze, ila muombe Mwenyenzi Mungu akuepushie na magonjwa.

Ukiyapata, utafika hospital na mara moja utalazimika kuyaacha baadhi ya mitindo ya maisha huku ukiwa umeshachelewa zaidi.

Ukiwa unaneemesha mwili wako basi neemesha na akiba kwa ajili ya matibabu hapo baadae.
We mzee kumbe una uchawa pia?

Nimesikitika.
 
Prof Janabi wala si wa kupenda kuonekana. Ila majukumu yake yanamuweka front.

Lakini umaarufu wake si kwa sababu ya uprof wala Ukurugenzi, bali ni kwa sababu ya ushauri usioyumba. Wabongo hawapendi uwaambie waache wanachokipenda.
Tanzania tuna Madaktari wa Moyo wangapi?
Unafikiri kwanini Kina Dr makubi,Kina Dr Ntuli Kapologwe na kuna Ma "CMO (Chief Medical Officer)" kibao Tanzania imeshawahi kuwa nao,umewahi kuwasikia wapi wakijitia umaarufu...

Tukubali kwamba kuna Maproff na Madaktri wanapenda kuonekana mitandaoni na kwenye habari na hii haikubaliki kwani ni kinyume cha ethics za kitabibu... (Hippocroatic Oarth)

Huenda ameamua kuwa upande wa kisiasa na sio upande wa kidaktri..

UKihitimu udaktari Kiapo cha Tano Ni kuapa Kutokujitangaza au Kuapa Kutokubali kutangazwa kwa manufaa ya Kada nzima.....
IMG-20231120-WA0000(1).jpg
 
Tafsiri ya Uchawa ni nini dogo?
Huusisha na andiko langu kuonyesha kuwa mimi Chawa.
Ushabiki maandazi.

Nakuona unamkingia anavopondwa na kusifia mafanikio yake....

Mtu mzima anaejali afya yake hasubiri kuambiwa ale vipi, atafanya due diligence, na ukitakiwa ushauri wa wataalam atafuata taratibu maalum(ataenda hospitali)

Anachokifanya huyo celeb wako ni kuchanganya watu tu. Apuuzwe.
 
Ni wapi? Mm najua Njiro nayo hii ukinitoa nje ya Tsunami nimepotea, Sakina kidogo, Kiserian kidogo, mjini kati kwa sana.

Najua ni kubwa.. na huwezi ijua yote.
Ni mtaa katika mitaa ya kata ya Unga Ltd.Kata ya kati utakuwa unafanya biashara au shughuli nyingine za kiofisi.
 
Ushabiki maandazi.

Nakuona unamkingia anavopondwa na kusifia mafanikio yake....

Mtu mzima anaejali afya yake hasubiri kuambiwa ale vipi, atafanya due diligence, na ukitakiwa ushauri wa wataalam atafuata taratibu maalum(ataenda hospitali)

Anachokifanya huyo celeb wako ni kuchanganya watu tu. Apuuzwe.
Ok, uchawa una malipo yake, hujarelate mimi napata malipo gani kutoka kwa Prof Janabi. Mtu ambaye hata hanijui kwa lolote.

Tuachane na hayo;

Prof Janabi hajiamkiagi tu na kuanza kuzungumza. Bali anapoalikwa na kutakiwa kutoa maoni hufanya hivyo bila kusita.

Kama hufahamu, moja ya majukumu ya msingi ya Wahudumu wa afya ni kutoa ushauri elekezi juu ya namna bora ya kujitunza. Na hili si lazima pawe katika kituo cha huduma za afya, popote pale anapohitajika kufanya hivyo.

Kuna watu wanafanya mitindo fulani ya maisha pasipokuwa na uelewa wa athari zake hapo baadae. Mathalani, wewe unavyonyonya nyuchi za warembo, unafanya kwa kuongozwa na hisia. Baadae unakabwa na saratani ya koo, unaanza kuja kutia huruma. Eti,laiti ningelijua!.

Sasa wataalam wa afya (akiwemo Prof Janabi) wanafanya majukumu msingi kuwasanua ninyi vijana na rika zote ili mchukue tahadhari. Tena ni ushauri bila ya shurti.

Unapenda kusikia ukiambiwa kula kupita kiasi? Lewa ugaregare ndiyo ujue kuwa hakuchanganyi? Ukiambiwa fakamia junk foods, ndiyo utajua huyu ndiye mtaalam sasa? Huo ni ujuha.

Tengua kauli yako kuwa mimi ni Chawa.
 
Prof Janabi wala si wa kupenda kuonekana. Ila majukumu yake yanamuweka front.

Lakini umaarufu wake si kwa sababu ya uprof wala Ukurugenzi, bali ni kwa sababu ya ushauri usioyumba. Wabongo hawapendi uwaambie waache wanachokipenda.
Na ile 17/03/2021 ilimpaisha
 
Back
Top Bottom