Profesa Justinian Rweyemamu (1942-1982): Msomi wetu wa karne

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
MSOMI WETU WA KARNE.

Kijiji cha Katoma kipo Mkoani Kagera.Tarehe 28/09/1942 alizaliwa kijana mmoja mtanashati wa mwonekano na kichwani.Huyu ni Justinian Rweyemamu, mmoja wa wasomi hodari kuwahi kutokea kwenye kijiji hicho na Tanzania nzima.

Inasemekana akiwa shule ya Upili Ihungo aliongoza mtihani wa Cambridge kwa Jumuiya ya Madola, na kupata ufadhili wa masomo katika Chuo Kikuu cha Fordham, na baadae kusoma PhD katika Chuo Kikuu cha Havard.

Katika umri mdogo sana, alipata PhD, aliandika vitabu kadhaa kuhusu historia ya uchumi wa Tanzania, kuwa mhadhiri na Mkuu wa Idara ya Uchumi wa kwanza mzawa UDSM, kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mipango na Mshauri Mkuu wa Rais (Nyerere) katika masuala ya uchumi.

Mwaka 1977 alienda kufanya kazi UN kwa kile kinachosemwa kutofautiana na Mwalimu Nyerere kuhusu sera za uchumi.

Profesa Justinian Rweyemamu amewafundisha uchumi akina Prof. Lipumba, Prof. Benno Ndulu, Jakaya Kikwete,Prof.Juma Semboja,n.k.

Alifariki tarehe 30/03/1982 New York akiwa na umri wa miaka 40.

Kufahamu zaidi Historia yake, soma hapa chini kama ilivyoletwa na Mwanachama mwezetu BOB OS

 
Very interesting, asante mkuu kwa kutujuza haya.
 
HamnA sehumu niliyosema hii ni biography
Bujibuji ukileta taarifa tunategemea kuna utaratibu wa kuileta "hasa kama hii ambayo unataka kuweka wasifu wa mtu". Unakataa kitu kiko wazi. Mtu akisoma post yako inaonyesha unataka kutoa wasifu-biography ya Rweyemanu .Kama hukubali hili, kwa heri, Jpili njema
 
sijaandika wasifu, ungekuwa ni wasifu ungekuwa na maelezi mapana zaidi, nilichoandika ni kwa jinsi ninavyo mfahamu.
Hii ni mbegu tu, waweza zama kinani kusaka taarifa zake kwa mapana.
 
Hili nalo ni tatizo lingine kwenye elimu yetu, Bujibuji keshatoa mwanga wa huyo prof. Anaetaka kumfaham zaidi ameshapata pa kuanzia. Kila mmoja anapenda amfaham kwa mapana katika nyanja tofauti, wengine wanataka wajue aliandika vitabu vingapi, alioa na alikua na watoto wangapi, kwanini alitofautiana na mheshimiwa. Sasa ukitaka aandike yote hayo atakidhi matakwa ya kila mmoja?

Hata shuleni, somo moja mnaweza kupewa kusoma vitabu kadhaa tofauti tofauti ili kupata uelewa zaidi. Hatupendi kufanya homework.
 
sijaandika wasifu, ungekuwa ni wasifu ungekuwa na maelezi mapana zaidi, nilichoandika ni kwa jinsi ninavyo mfahamu.
Hii ni mbegu tu, waweza zama kinani kusaka taarifa zake kwa mapana.
Hapo sasa nimekuelewa! In a nut shell!
 
And he died so young. R.I.P Prof.
 
Kufauru Mitihani kwa Watanzania nje ya Nchi tena katika vyuo bora kitu cha kawaida tuu hicho....huyo ni msomi wa karne katika hicho kijiji na si Tanzania nzima...
Sijui umeona hiyo miaka aliyosoma? Haikuwa kawaida kwa kipindi hicho. Hakuna haja ya kukosoa mtazamo wa kila mtu kwa vile tu hatuafikiani nao.
 
Ue

Umekupatia raisi wako wa awamu ya nne, mwana uchumi na mpinzani kama Lipumba, au ulitaka agawe pesa bure ndio ujue thamani ya mtu.
ahahaha kweli unachekesha.Nani kakuambia Kikwete alichaguliwa kwasababu ya elimu yake?
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…