Profesa Justinian Rweyemamu (1942-1982): Msomi wetu wa karne

Profesa Justinian Rweyemamu (1942-1982): Msomi wetu wa karne

Usomi wake wa karne umesaidia vipi watanzania?
Unataka faida gani zaidi uzione, umeshaambiwa kawafundisha akina lipumba, jk, ndulu na wengine wengi huoni kama hiyo ni faida wanataaluma wa uchumi waongezeka na wengine wapo waliofundishwa na kina lipumba na wanafundisha vyuo vingine au ulitaka faida mpaka alete hela?
 
Kwa wale wanaomfahamu, je watoto wake nao wamesoma kufikia kiwango cha baba yao? Hao walioko Arusha na New York wanafanya nini? Haya maswali ni muhimu kujua majibu yake ili watu waweze kumpima kama alikuwa resposible parent!! Hapo mwisho wa makala wanasema amemuacha Anna na Joan, was this guy polygamous?
 
Kawafundisha hao watu waliotajwa kama lipumba,Semboja,Beno Ndulu na JK.....
Angesikitishwa sana na utendaji wa mwanafunzi wake aliyetokea kuwa rais wa nchi, asiyejua kwa nini nchi ni masikini na aliyetegemea misaada ya nje kwa maendeleo ya nchi
 
MSOMI WETU WA KARNE.
Kijiji cha Katoma kipo Mkoani Kagera.Tarehe 28/09/1942 alizaliwa kijana mmoja mtanashati wa mwonekano na kichwani.Huyu ni Justinian Rweyemamu, moja wa wasomi hodari kuwahi kutokea kwenye kijiji hicho na Tanzania nzima.

Inasemekana akiwa shule ya Upili Ihungo aliongoza mtihani wa Cambrige kwa Jumuia ya Madola, na kupata ufadhili wa masomo katika Chuo KikuEhu cha Fordham, na baadae kusoma Phd katika Chuo Kikuu cha Havard.

Katika umri mdogo sana, alipata Phd , aliandika vitabu kadhaa kuhusu historia ya uchumi wa Tanzania, kuwa mhadhiri na Mkuu wa Idara ya Uchumi wa kwanza mzawa UDSM, kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mipango na Mshauri Mkuu wa Rais (Nyerere) katika masuala ya uchumi.

Mwaka 1977 alienda kufanya kazi UN kwa kile kinachosemwa kutofautiana na Mwalimu Nyerere kuhusu sera za uchumi.

Profesa Justinian Rweyemamu amewafundisha uchumi akina Prof. Lipumba, Prof. Benno Ndulu, Jakaya Kikwete,Prof.Juma Semboja,n.k.

Alifariki tarehe 30/03/1982 New York akiwa na umri wa miaka 40.
Eh!!! Alifriki akiwa bado kabisa!!!!! 40 kwa miaka hii wewe ni kijana bado!!!!!
 
Nimependa the way watoto wake wote amewaita majina ya kihaya licha ya kwamba kasoma ulaya. Ningekuwa mimi hapo ungekuta wanangu wanaitwa Whiteson, Fitzgerald, Derrick, Jennifer nk
 
MSOMI WETU WA KARNE.
Kijiji cha Katoma kipo Mkoani Kagera.Tarehe 28/09/1942 alizaliwa kijana mmoja mtanashati wa mwonekano na kichwani.Huyu ni Justinian Rweyemamu, mmoja wa wasomi hodari kuwahi kutokea kwenye kijiji hicho na Tanzania nzima.

Inasemekana akiwa shule ya Upili Ihungo aliongoza mtihani wa Cambrige kwa Jumuia ya Madola, na kupata ufadhili wa masomo katika Chuo Kikuu cha Fordham, na baadae kusoma Phd katika Chuo Kikuu cha Havard.

Katika umri mdogo sana, alipata Phd , aliandika vitabu kadhaa kuhusu historia ya uchumi wa Tanzania, kuwa mhadhiri na Mkuu wa Idara ya Uchumi wa kwanza mzawa UDSM, kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mipango na Mshauri Mkuu wa Rais (Nyerere) katika masuala ya uchumi.

Mwaka 1977 alienda kufanya kazi UN kwa kile kinachosemwa kutofautiana na Mwalimu Nyerere kuhusu sera za uchumi.

Profesa Justinian Rweyemamu amewafundisha uchumi akina Prof. Lipumba, Prof. Benno Ndulu, Jakaya Kikwete,Prof.Juma Semboja,n.k.

Alifariki tarehe 30/03/1982 New York akiwa na umri wa miaka 40.
Ihungo Secondary haijawahi kuwa shule ya Upili -Sahihisha.
 
Kufauru Mitihani kwa Watanzania nje ya Nchi tena katika vyuo bora kitu cha kawaida tuu hicho....huyo ni msomi wa karne katika hicho kijiji na si Tanzania nzima...
Ahaaaaaa... Ahaaaaaa
Mdau umenifanya nicheke sana, eti huyo ni maoni wa kijiji chao na sio Tz nzima
 
Huyu ndiye mtanzania wa Kwanza kusoma Havard university (Ph.D ya Uchumi)

Havard university ni chuo namba moja kwa ubora duniani, kwahiyo ukiona mtu amesoma hiki chuo muheshimu sana.

Justinian F Rweyemamu alizaliwa Katoma Bukoba mkoani Kagera tarehe 23/09/1942.

Mwaka 1958 alijiunga na shule ya St Thomas More college Ihungo iliyokuwa chini ya Kanisa Katoliki kwa ajili ya masomo ya shule ya sekondari, ambapo darasani kwao aliibuka kinara wa darasa. Baada ya hapo mwaka 1961 akapelekwa Marekani Fordham University, ambapo mwaka 1965 alihitimu katika chuo hicho shahada ya kwanza (Bachelor degree in economics, applied mathematics & philosophy).

Mwaka 1971 alihitimu shahada ya uzamivu (Ph.D, thesis 'An Industrial Strategy for Tanzania') Havard university akiwa chini ya fellowship ya Rockefeller foundation.

Akiwa Havard walimu wake walikuwa ni Albert Hirschman, Thomas Weisskopf wataalam wa uchumi duniani.

Rweyemamu pia alihudumu katika chuo kikuu cha Dar es salaam, huku baadhi ya Wanafunzi wake wakiwa Jakaya Kikwete Rais mstaafu wa Tanzania, Benno Ndulu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania mstaafu, Ibrahim Lipumba na Delphine Rwegasira mtaalamu wa uchumi.

Justinian Rweyemamu alifariki tarehe 30/03/1982 NewYork Marekani akiwa na miaka 40 tu.

Huyo ndo Rweyemamu, Muhaya na Mtanzania wa kwanza kusoma Havard university.

Mtanzania mwingine aliyesoma Havard university ni Benjamin Ferdinandez mkurugenzi wa Nala.

Chini[emoji116] ni Picha yake.

20220710_010802.jpg
 
Back
Top Bottom