Profesa Justinian Rweyemamu (1942-1982): Msomi wetu wa karne

Watanzania wengi sana tu wamesoma IVY LEAGUE na vyuo vingine vikubwa tu duniani. Mpaka sasa kuna watanzania wengi wanaendelea kusoma huko. Nadhani siyo sahihi kuwataja majina yao hapa kwasababu ya faragha. Ila wanasiasa wakubwa nitawataja.
  • Mzee Benjamini Mkapa (Columbia University New-York)
  • Prof Kighoma Malima (Yale University and Princeton University)
  • Balozi Emmanuel Mwambulukutu (Princeton University)
  • Prof Bonaventure Rutinwa (Oxford University)
  • Mzee Andrew Chenge (Harvard University)
  • Justice Dr. Gerald Ndika (Cambridge University)
  • Prof Delphin Rwegasira (Harvard University)
  • Dr Salim Ahmed Salim (Columbia University New-York)
  • Prof Matthew Luhanga ( Columbia University New-York)

Watanzania wenye akili wapo wengi tu, sema ndiyo wamejaa Private Sector na wengine hawarudi Bongo. Kuna jamaa yangu tumekuwa naye alisoma ISM baadaye akaenda Marekani na kusoma chuo kikubwa lakini familia yake imemkatalia kabisa asirudi Bongo. Kuna dada mwingine tuliwahi kufanya naye kazi, ana akili balaa. Yeye alisoma ISM baadaye akaenda kusoma chuo kikubwa nchini Uingereza lakini naye ndiyo hivyo...
 
Huyu alisoma Havard na siyo oxford, alikuwa admitted masters & Ph.D.
Kusoma hivyo vyuo siyo mchezo ndugu, mpaka sasa kwa Tanzania, watu waliosoma Havard nawafahamu wawili tu, huyu na Benjamin Ferdinandez.
Kuna mtaalam mmoja hapo umemtaja mwalimu wangu bora kabisa, The Great Prof Delphine Rwegasira mtaalam wa Monetary Economics nae amesoma phD Havard.
 
Upo sahihi mkuu, ila hapa tunazungmzia mtanzania wa kwanza Kusoma Havard university, na mpaka sasa Watanzania waliosoma Havard hawawezi kuzidi watano, hachana na hivyo vyuo vingine ulivyovitaja mkuu.
 
Kuna mtaalam mmoja hapo umemtaja mwalimu wangu bora kabisa, The Great Prof Delphine Rwegasira mtaalam wa Monetary Economics nae amesoma phD Havard.
Aisee kumbe Rwegasira PhD kapiga Havard na yeye. Huyu Justinian Rweyemamu ndiye aliyewafungulia Watanzania kusoma Havard.
 
Nyie Mangi njooni huku, maana kutwa jujimwambafai humu kuwa mumesoma peke yenu Tanzania nzima.
 
Huyu alisoma Havard na siyo oxford, alikuwa admitted masters & Ph.D.
Kusoma hivyo vyuo siyo mchezo ndugu, mpaka sasa kwa Tanzania, watu waliosoma Havard nawafahamu wawili tu, huyu na Benjamin Ferdinandez.
Mtemi...
 
Doh many tanz
Doh many Tanzanians have studied at harvard

But I appreciate the guy though

Prof weiskoff kazaliwa 40' s how was him. His lecture while rweyemamu was born in 42's
 
Upo sahihi mkuu, ila hapa tunazungmzia mtanzania wa kwanza Kusoma Havard university, na mpaka sasa Watanzania waliosoma Havard hawawezi kuzidi watano, hachana na hivyo vyuo vingine ulivyovitaja mkuu.
Labda wewe huwafahamu, lakini binafsi nawafahamu wachache ambao ni zaidi ya watano. Wiki mbili zilizopita nimeenda FEZA International (Salasala) walikuwa wanafunga shule, nikakutana na Bango Kubwa linatoa hongera kwa mwanafunzi aliyepata Scholarship Harvard University. Watoto wengi wa IST, ISM, HOPAC wanaofanya vizuri wanapelekwa IVY LEAGUE.

Kumalizia tu, kuna mtoto wa kigogo mkubwa wizara moja ni jirani yetu mtoto wake amesoma YALE University kwa pesa zake mwenyewe na alikuwa na mpango wa kufanya kazi GOOGLE sasa sikufatilia ilikuwaje. Kuna dogo mwingine niliwahi kukutana naye IFAKARA HEALTH INSTITUTE alisoma Harvard University.

Mpaka kufika mwaka 2018 kulikuwa na watanzania wasiopungua 13 wanasoma Harvard University, sasa wewe hiyo ya tano sijui umeitoa wapi na unazidi kukomaa nayo. Kuna watanzania wana akili nyingi sana, shida ni kwamba watu wenye akili nyingi huwezi kuwakuta wanafanya siasa za Tanzania hata siku moja. THEY HAVE LOTS OF ISSUES GOING ON IN THEIR LIVES..
 
Aisee kumbe Rwegasira PhD kapiga Havard na yeye. Huyu Justinian Rweyemamu ndiye aliyewafungulia Watanzania kusoma Havard.
Haswaaa moja ya mabingwa wa uchumi pale mlimani nadhani amestaafu kwa sasa.

Akinifundisha Monetary Economics huku akishika kijichupa cha maji aina ya Cool Blue akizunguka nacho pale ATA na ATB.

Nilikuwa siwezi kosa muhadhara wake na nilikuwa nakuwa makini mno kuanzia mwanzo wa kipindi hadi mwisho huku nikinukuu kila analosema iwe ni mifano iwe ni hadithi nanukuu vyote kwenye diary yangu.

Hadi leo ninayo diary yangu hii huwa naipitia kujikumbushia.

Nilifaulu vizuri sana somo lake Semister one nikapiga Banda(A) na Semister two nikapata B+

Huyo ndio The Great Prof Delphine Rwegasira msomi kutoka havard akihudumu World Bank, IMF na Africa Development Bank ADB Makao makuu abdijan Cote devoire kabla ya kurejea tena kufundisha mlimani.
 
Prof Justinian Rweyemamu ni moja kati ya watanzania wenye akili sana. Niliwahi kumsoma kipindi tunafundishwa kuhusu THE BRANDT REPORT, utafiti ambao ulidhaminiwa na Benki ya dunia (WORLD BANK) ili kuchunguza tabaka la kiuchumi lilipo baina ya nchi zilizoendelea (Northern Industrialized Countries) na ambazo zinaendelea (Southern Less Industrialized Countries). Huu utafiti unatumika mpaka leo hii na wasomi mbalimbali kama moja ya rejea muhimu zaidi inayoonyesha taswira ya dunia yetu. Kiufupi huwezi kumaliza kusoma uchumi, sheria, historia au sayansi ya siasa kutoka chuo chochote kile bila kuisoma THE BRANDT REPORT.

Sasa basi, kamati iliyofanya huu utafiti wa The North-South Economic Divide, ilihusisha wachumi wenye uwezo mkubwa duniani kama Willy Brandt aliyekuwa waziri mkuu wa Ujerumani. Prof Justinian Rweyemamu na Amir Jamal nao walikuwemo kwenye hii kamati na mchango wao ulikuwa mkubwa sana. Walitoa ushauri mzito sana mwishoni, hasa ni vitu gani nchi za Afrika zifanye ili kuweza kuendelea kiuchumi.

Mzee Nyerere angewasikiliza watu kama Prof Rweyemamu nadhani Tanzania ingefika mahali pazuri mno, lakini ndiyo hivyo. Kama ambavyo marehemu Horace Kolimba aliwahi kusema kuhusu Mwalimu Nyerere, "Msimamo kwanza , Maslahi Baadaye"
 
Aisee!
 
Usomi wake wa karne umesaidia vipi watanzania?
Ungesaidia sana kama mwalimu angemsikiliza Profesa sababu yeye ndiye alikuwa mshauri wake mkuu. Mwalimu alisomea lugha siyo uchumi.
 
Huyo ndo Rweyemamu, Muhaya na Mtanzania wa kwanza kusoma Havard university.

Mtanzania mwingine aliyesoma Havard university ni Benjamin Ferdinandez mkurugenzi wa Nala.
..bila kusahau mh. Andrew Chenge!
Wapo wengi tu
 
Kuna mtaalam mmoja hapo umemtaja mwalimu wangu bora kabisa, The Great Prof Delphine Rwegasira mtaalam wa Monetary Economics nae amesoma phD Havard
Ulalae usingizi wa amani mwalimu wangu bora kabisa Prof Reegasira.

Hakika nimeumia mno kusikia kuhusu kifo chako tarehe 30/05/2024
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…