Profesa Kabudi: Katiba tuliyonayo ni madhubuti ndio maana imetuvusha tulipopata matatizo!

Usinilishe maneno mdomoni. Nani kasema hamtambui Rais? Nimesema wabunge walioko hawana sifa za kuitwa wawakilishi wa wananchi.

Mtu anashinda kura ya maoni anaachwa anachukuliwa mwingine kwenda kuomba kura! Na mbaya zaidi, mmoja wa wagombea wa Urais ndiye anateua Mkuu wa Tume ya Uchaguzi na watendaji wake! Yaani timu moja ichague refa na linesmen wanaowapenda wao, na wawambie wasithubutu kuruhusu timu nyingine kufunga goli, kisha useme wamepata ushindi halali?

Wewe ulimsikia Rais aliyepita akiwaambia Wakurugenzi kwamba hawezi kuwateua yeye kisha wamtangaze mtu asiye wa chama chake kushinda. Sasa mbunge anayechaguliwa kihivyo ni mwakilishi wa wananchi? You make me laugh.

Na hao wabunge 19 walioingizwa kwa hila na Spika ni wawakilishi wa wananchi wepi!

You can cheat some of the people some of the time but you cannot cheat all the people all the time. CCM iache sasa mbinu za kudanganya kwani tunaelewa ukweli na haki vikoje.

I have not given up on Mama Samia. Nadhani anasukumwa tu na watu wanaotaka kuhodhi madaraka, ila yeye si thulumati. Tim will tell.
 
Mtu mnafiki kama Kabudi, ni useless kwa Taifa. Watu wanafiki na wachumia tumbo wa namna hii, hawastahili kupewa heshima katika jamii, zaidi ya ule utu wamwanadamu asiye na msimamo wowote.
 
Sikulishi maneno mdomoni. Ninaongea logic ya msimamo wenu. Kwamba huo uchaguzi mkuu wa 2020 mnauita ulikuwa uchafuzi mkuu na kwa hiyo yote yaliyotokana na uchafuzi huo mkuu hamuyatambui. Na yaliyotokana na huo mnaouita uchafuzi mkuu ni pamoja na hao wabunge uliowataja wakiwamo hao 19 na pia rais wa Tanzania. That is the logic of your position.

Kuyapinga matokeo ya uchaguzi huo mahakamani kwa mjibu wa sheria zetu, nayo mlikataa kwa kutokuwa na imani na mahakama zetu kwa kuwa majaji wanateuliwa na rais. Baraza kuu la chama chenu kuitishwa kusikiliza na kuamua rufaa ya hao 19 kwa mjibu wa katiba yenu, nayo mmekataa kwa kisingizio cha kuwa 'it is a waste of time'.

Hivyo logically misimamo yenu inashindwa kueleweka kwa watu makini.
 
Bora hata asingesoma anadhalilisha kweli taaluma yake huyu propesa wa majalalani.
 
Unataja msimamo "WENU". Wa mimi na nani? Si mwanachama wa chama chochote mimi.

Mtu ukisema uchaguzi umekuwa wa kuiba kura haina maana kwamba humtambui aliyetangazwa kuwa Rais. Likatiba lenyewe linasema akishatangazwa basi hakuna ruhusa ya kudai mahakamani kwamba hakuchaguliwa kihalali. Sasa hivi sidhani kama kuna mtu au chama ambacho hakimtambui Mama kwamba ni Rais wa Tanzania. Dr Mwinyi pia ni Rais wa Zanzibar. Sikubali kwamba walichaguliwa na wananchi kushika nafasi hizo lakini natambua walitangazwa kuzishika.

Stop making wild assumptions. I am not a member of Chadema.
 
Kama katiba iliyopo ya sasa ni imara, je, ilikuwaje Kabudi na tume ya jaji Warioba walizunguka nchi nzima kukusanya maoni kwa wananchi?

Waandishi wa habari wanatakiwa, wawe wanatusaidia kuwauliza wanasiasa maswali chokonozi!
 
Tatizo siyo kifo kweli! Lakini kumbuka aliyefariki ni Rais,tena ndiyo yuko Madarakani,Kama kungetokea wale wavamizi wa Mirathi ya Mama unazani saa hizi hali ingekuwaje!?

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
uwe na katiba au usiwe nayo. iwe nzuri au mbaya......wanaoweza kufanya hivyo ni jeshi. ukiwa na jeshi linaloheshimu mfumo hilo haliwezi kutokea hata kama rais na makamu wake wafe. bado litasoma katiba na liifuate. Hizi porojo za kabudi ni za kutetea tumbo tu
 
Mtu mweusi ni Kima aliechangamka.Imagine CCM wanatumia zile ndege za serikali katika shughuli zao za kila siku kana kwamba ni mali ya chama!
 
Kilichotuvusha ni jeshi imara sio katiba, ni afadhali mkashughulikia katiba likiwa bado lina umoja.
 
Supu Ina nzi
 
Kwa mila na desturi za mtu mweusi hairuhusiwi kuongea wakati unakula. Kwa sasa mzee wa jalalani anakula hawezi kuongea. Akiwa mjumbe wa tume ya katiba mpya alikuwa na akili binafsi sasa zimeondolewa na kuingiziwa za ccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…